WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
JADILI..
Hii ni mada inayojadiliwa Star TV. Mawazo yanayotolewa yanatisha..
Hii ni mada inayojadiliwa Star TV. Mawazo yanayotolewa yanatisha..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MAISHA YANGEKUWA YANA ''AJUA'' , UNGEMUOA MKE ULIYENAYE SASA/ UNGEKUBALI KUOLEWA NA MUME ULIYENAYE SASA?
....nice one WoS, ...unajua mimi ningeulizaje?
Tena ningeweka na kura, Jibu la NDIO au HAPANA.
....nadhani kura zitafungana.
AM
....nice one WoS, ...unajua mimi ningeulizaje?
Tena ningeweka na kura, Jibu la NDIO au HAPANA.
....nadhani kura zitafungana.
AM
Si kweli WOS wengine waliingia kwenye ndoa kwa sababu ya fashions na wao waonekane wanandoa :A S-rose:
Wengine waliingia kwenye ndoa kwa kujilazimisha
Wengine walibeba mimba ikawalazimu kuingia kwenye ndoa
Wengine wamefata pesa au mali ndani ya ndoa
Wengine wanajiegesha jua litulie kisha waendelee na safari
Wengine wapo kwa ajili ya heshima ya wazazi.
wengine ni kweli wanapendana..:A S-rose:
NK. Nk.
Mkuu Mbu binadamu tunapokuwa kwenye mapenzi mara nyingi huwa ni raha tupu. Binadamu tunazijua kasoro zretu ambazo wapenzi wanaweza kuzikubali na nyingine ambazo hawatakuwa tayari kuzikubali hivyo kipindi hicho cha mapenzi moto moto ni nadra sana kuzijua kasoro za umpendaye. Sasa unapoamua kuolewa naye au kumuoa basi ndiyo sasa anaanza kuonyesha makucha yake na kama nilivyosema kuna kasoro nyingine zinavumilika kabisa maana hakuna binadamu ambaye yuko perfect. Kwangu binafsi sipendi uongo, uchafu, wizi, uhuni, ulevi, dharau, kutokubali makosa na kusema samahani , kutojua kupika, uvivu wa kupita kiasi. Hizi kwa kweli si rahisi kuvumilika kabisa ukiuingia mkenge kama huu ni bora kujinasua haraka sana kabla ya kukumbana na matatizo utakayoyajutia kwa miaka mingi baadaye.
Kama alivyosema FL1 kila mtu aliingia kwenye ndoa kwa sababu zake binafsi. lakini wapo walioingia kwa mapenzi makubwa lakini kumbe hawakujua tabia halisi za wapenzi wao na ndio chanzo cha machungu mengi kwenye ndoa.
Kama hujafunga ndoa...angalia machungu mwenzio anayokupa kabla hamjaoana...tafakari uyawaze..jiulize mkishaoana utaweza kuyavumilia?
Ikiwa unaona utaweza kuyavumilia ( tamaa ya pesa/mali,lugha mbaya, ulevi, uongo, kutokua mwaminifu, uchafu, uvivu,kutokuwa na huruma, kutokuwa na kauli nzuri/tamu, kutokusema samahani, kutokujua kubembeleza, ubinafsi,uchoyo, ) BASI KAFUNGENI NDOA na hii ni kwa wote wanawake kwa wanaume.
ni ngumu sana kujua tabia halic ya mpenzi wako mpaka mtakapoanza kuishi pa1, hapo ndio utauona uhalisia wa mtu!...lakini kuna vile vitu vya kuweza kuonekana kaam ulevi kupindukia/uchafu nk lakini bado hapo hapo anaweza ku petend kwamba amebadilika kwa nia ya kukupata mkishaingia ndani vyote vnajirudia kama awali...heee
Kabla sijamuoa huyu mama matesha wangu nilikuwa na mpenzi wangu niliyekuwa nampenda sana. Ki ukweli tulipendana sana. Na tuliachana bila kujua kimetokea nini. Niliumia sana, nilitaabika sana. Sikuwa nahitaji kuwa na uhusiano na mwanamke mwingine awaye yote. Nilitamani kuwa padre.
Mpaka alipotokea huyu rafiki yake nu huyo mpenzi wangu wa zamani. Alikuwa ananionea huruma sana, alikuwa ananifariji na kunipa moyo. (Tulipoachana na mpenzi wangu, mpenzi wangu huyo alitokomea kubeba mabox na mpaka leo hajarudi -RIP kama ameshakufa). Huyu rafiki yake ndio huyu mama matesha wangu.
Nadiriki kusema nashukuru niliachana na mpenzi wangu yule wa zamani kwa kuwa huyu mke wangu wa sasa ndio ulikuwa mpango wa Mungu awe mke wangu. She is beautiful, loving and caring. Sitajuta kuonana naye (sijawahi kujuta miaka yote 15 ya kufahamiana toka urafiki, upenzi, uchumba mpaka ndoa.
Hivi thread inasemaje?? Oooh Yes.... Mimi na mke wangu Tunapendana sana. Ndani ya ndoa yetu tunapendana. Period!!!
(Am sore leo sina hangover ya kutosha)
Mila na desturi lazima zienziwe. Mila zinaleta uzoefu na mbinu mpya katika pafomensi ya kudumisha ndoa...... Askofu unatakiwa kanisani mida hii,....:mmph:..Zile Mila za nini sasa
Wewe uko kwenye ndoa / utakuwa kwenye ndoa kwa sababu gani?jibu: hapana
wengine wapo kwenye ndoa kwa sababu wanahisi ni wajibu wao kwa jamii
wengine wako kwenye ndoa kwa sababu wanataka watoto na wangependa kupata mwenza wa kuwasaidia kulea
wengine wako kwenye ndoa kufuatia maslahi binafsi
wengine wako kwenye ndoa kwa manufaa ya wazazi
wengine wako kwenye ndoa kwa kuwa ameona labda inaweza kuleta mabadiliko katika maisha yake yaliyokuwa yamedorora
wengine wako kwenye ndoa ili kukimu mahitaji ya mwili
wengine wako kweenye ndoa kwa kukidhi mahitaji ya kiroho
nakadhalika na kadhalika