Ni kweli kuwa watu wote walioko kwenye ndoa au waliooana wanapendana?


Naomba utueleze mfano wa hizi tabia ambazo sio rahisi kuzijua kabla ya kuoana..........
 
sababu zenyewe ni

mapenzi
kutimiza mahitaji yangu ya kiwiliwili ( muhimu sana hili kwa sababu siwezi kutenda zinaa)
Kutimiza mahitaji ya kiroho ( ndoa ni stara......dini inasema)
heshima kwa jamii ........
heshima kwa wazee .....
kutaka watoto...
na kadhalika na kadhalika
 

Je, kuna umuhimu wa wapenzi kukaa pamoja (under one roof) kwa muda fulani, say, mwaka mmoja au miwili kabla ya kufunga ndoa, ili waweze kufahamiana tabia zao?
 
Wengi wanaoa au kuolewa kwa kutimiza wajibu kuwa na mm sasa nimeoa au nimeolewa.
Baada ya kipindi kifupi ndo moto unaanza kuwaka ndani ya ndoa.
 
Naomba utueleze mfano wa hizi tabia ambazo sio rahisi kuzijua kabla ya kuoana..........

Ni pale atakapoanza kukurudia home maucku ya manane, lakini mwanzo alikuwa hana hiyo tabia, pale utakapoona mwenzio ana katabia ka kutopenda ndugu/jamaa zako nk, kuna vijimambo tu lazima wote wawili mtakuja kuviona mkiingia ndani...eg yeye ananiambiaga alinijua mie ni kichaa lakini hakujua kama ni cha kiwango cha juu kihivyo, ukichaa nilikuwa nao kuanzia mwanzo lakini nilivyoingia ndani kutokana na ishu za kifamilia tena ukichaa ukaongezeka tofauti kabla cjaingia ndani...yaani ucmtegeee huyu wa leo ndio atakuwa wa kesho.umenielewa hapo Charity?
 
Nimeikubali hiyo moja tu kwenye red. Nyingine zilizobakia unaweza kuzipata hata kama hauko kwenye ndoa.
 
Wewe uko kwenye ndoa / utakuwa kwenye ndoa kwa sababu gani?

Kwa sababu ninashiba. Ndo maana nampenda kwani mkate anaonipatia unanitosha, ingawa sijui kama kipimo ninachompimia kinakidhi haja zake!!! Kwa hiyo mie nampenda kwa hilo na mengine mengi ila kwa upande wako siwezi kumsemea. Moyo siyo transparent kwa hiyo jibu lake alijua mwenyewe.
 

Dah! Nimekuelewa sana sijui dadangu au mdogo wangu!!!!!!!!!!!......
Inavyoelekea kupata ndoa iliyotulia asilimia 90 tuseme ni bahati.(hizi 10% naziacha kwa kelele za ndugu na marafiki)
 
Je, kuna umuhimu wa wapenzi kukaa pamoja (under one roof) kwa muda fulani, say, mwaka mmoja au miwili kabla ya kufunga ndoa, ili waweze kufahamiana tabia zao?

Wengi hawapendi hivyo mana nayo ina hasara zake, unaweza akakuchenjia ghafla tu, bora akianza hayo mabadiliko lakini mmehalalishana, kuliko kuanza mabadiliko then ukaona hakufai ukawa umepoteza muda wako, na utaishi na wangapi kwa mtindo huo?
 
Dah! nimekuelewa sana sijui dadangu au mdogo wangu!!!!!!!!!!!......
Inavyoelekea kupata ndoa iliyotulia asilimia 90 tuseme ni bahati.(hizi 10% naziacha kwa kelele za ndugu na marafiki)

Ukishatoa hiyo 10 ya mazagazaga, basi inawezakana kupata ndoa ya hivyo lakini ukijumlisha na vi ups& downs kibaooooo hapo, mnavisawazisha siku zinasonga!
 
ukishatoa hiyo 10 ya mazagazaga, bac inawezakana kupata ndoa ya hivyo lakini ukijumlisha na vi ups&downs kibaooooo hapo, mnavisawazisha cku zinasonga!
We mdanganye mwenzio tu....
 

Walioolewa/oa na ambao bado wote tuna heshima kwenye jamii/wazee wetu.....cku hizi vwengi waliopo kwenye ndoa ndio wamepoteza hiyo heshima kwenye jamii na mifano hai ninayo....kwingine tupo sambamba.
 
Nimeikubali hiyo moja tu kwenye red. Nyingine zilizobakia unaweza kuzipata hata kama hauko kwenye ndoa.

Mapenzi naweza kupata lakini si na huyo aliyenioa ...........sasa nimekubali ndoa na huyo kwa sababu ya mapenzi yangu kwake.

Mtoto pia siwezi kupata nje ya ndoa ....(rejea sababu uliyoikubali ya rangi red)
Heshima ya jamii pia ina mgogoro kama hujaolewa ...........na hasa ukizaa bila kuolewa ( kwa jamii iliyonizunguka)

So ukicheki kwa u deep .................sababu zinaingiliana hapo mkuu
 
Ingependeza sana kwenye hii mada kwa walioko kwenye ndoa kujizungumzia na kuacha kunyooshea ndoa za watu vidole .......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…