Ni kweli kwamba China iko kinyume na mwelekeo?

Ni kweli kwamba China iko kinyume na mwelekeo?

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111335088885.jpg
Juhudi za China ndani ya jamii ya kimataifa haziwezi kupingwa, lakini lengo la nchi za Magharibi kutaka kuongoza dunia linadai kuwa, China, kama nchi yenye ushawishi mkubwa isiyo ya magharibi, ni kitu cha kigeni.

Ikiwa ni mfumo tofauti kabisa wa kisiasa, China, kuanzia karne ya 19, imekuwa ikilengwa na nchi zinazotafuta kueneza tamaduni za kimagharibi duniani. Mafanikio ya nchi hiyo katika kupinga uvamizi wa kimagharibi katika zama za ubeberu zimeongeza zaidi hasira za wale waliojipa haki ya kuamua hatma ya binadamu. Na hii ndio sababu kuu ya vita ya kiitikadi kati ya China na nchi za Magharibi.

Baadhi ya wanasiasa na vyombo vya habari vya Magharibi wanaishutumu China na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa pande zote, n ahata kutaka kuwatenganisha wananchi na chama hicho. Lakini hii haimaanishi kuwa CPC ni kitu kibaya.

Miaka michache iliyopita, kitabu kilichoitwa ‘China Dhidi ya Mwelekeo’ kilipata umaarufu sana kwenye vyuo kutokana na historia ya siasa nchini China. cha kushangaza, mwandishi wa kitabu hicho, Marc Blecher aliielezea China kwa njia inayokinzana na jina la kitabu hicho: Nchi ya Kijamaa inayoongozwa na CPC haijawahi kujaribu kujitenga na dunia nzima. Sio mchochezi wa mfumo wa sasa wa uhusiano wa kimataifa. Ndio, China inaongozwa na ujamaa, lakini jambo hili halikinzani na maslahi ya watu ama kumaanisha upinzani kwa fikra za kisasa.

Tangu karne ya 19, fikra mbalimbali, kama mfumo wa soko katika uchumi, utaratibu wa uwakilishi katika siasa, kuheshimiana kama nchi huru katika uhusiano wa kimataifa na fikra za kisayansi, zilienea duniani. Kama hizi ni mwelekeo wa kisasa, China, inayoongozwa na CPC, pia inaendana, na sio kupingana na fikra hizo.

Jamhuri ya Watu wa China ilitambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa mwaka 1971, na kuruhusiwa kujiunga na Shirika la Biashara Duniani (WTO) mwaka 2001, na kuwa nchi ya pili kiuchumi duniani. China imefika hapa ilipo kwa sababu chini ya uongozi wa CPC, China imefungua njia ya maendeleo inayoendana na mazingira halisi ya ndani.

Kwanza, ni njia yenye msingi wa uhalisia wa China. ikikataa kufuata kama kipofu nyayo za wengine, China imebadilika kuendana na mabadiliko ya wakati, kufuata busara ya ustaarabu wake na mafunzo kutoka nchi nyingine.

Pili, ni mjia inayotanguliza mbele maslahi ya watu wake. Kwa kufuata nadharia ya maendeleo ambayo msingi wake ni watu, Chama cha Kikomunisti cha China kimejikita katika kuboresha maisha ya watu wake. Kinasisitiza kuwa serikali inapaswa kuwa kwa ajili ya watu, ya watu, na kwa faida ya watu. Kuhakikisha watu wake wanapewa kipaumbele imekuwa ufunguo muhimu wa mafanikio ya CPC katika mapinduzi, ujenzi, na mageuzi.

Tatu, ni njia inayofuata uvumbuzi kwa kufuata fikra za kisayansi. Changamoto ni kitu cha kawaida katika njia ya maendeleo ya China, lakini chini ya uongozi wa CPC, nchi hiyo imetafuta kivitendo utatuzi wa kiuvumbuzi, huku ikifanyia mageuzi njia za kifikra na vitendo halisi. Kwa kufuata kanuni za kisayansi, China inayoongozwa na CPC imeleta uhai mkubwa wa jamii, na kuongeza kasi yake ya maendeleo.

China iko katika njia ya kujenga uchumi wa wazi, na inapinga vitendo vya kujilinda kibiashara, pia imekuwa ikishikilia kanuni za uhuru na zinazofuata sheria katika biashara zake na nchi nyingine. Katika kufanya hivyo, imekuwa mshiriki muhimu na mchangia wa usimamizi wa uchumi duniani.

Matendo ya china kuhusuana na hili, yanaendana, na sio kupingana na mwelekeo wa sasa, nah ii inafafanua muujiza wa maendeleo ya China. Pia ni mchango wa China katika usimamizi wa dunia. Licha ya upendeleo wan chi za Magharibi dhidi ya Ujamaa na vyama vya Kijamaa, CPC imetafuta maslahi ya pamoja kati ya nchi mbalimbali. Lengo la China na kuwa na jamii ya binadamu yenye hatma ya pamoja linahusisha majadiliano ya kina, michango ya pamoja, na kunufaishana katika usimamizi wa dunia. Na mambo haya ndio yanahitajika katika zama hizi za sasa.

Kama China bado inaonekana kwenda kinyume na mwelekeo husika kwa sababu tu inaongozwa na chama cha kikomunisti, basi ni muda mwafaka sasa wa kuuliza kigezo hicho katika kufikia suluhisho.

Itikadi haiwezi kuwa msingi wa kukosoa nchi kama taifa la kishetani.
 
Back
Top Bottom