Ni kweli kwamba Mbowe amelazimishwa na mfumo kugombea Uenyekiti CHADEMA?

Ni kweli ni maarufu ila hata akishindwa bora apambane humohumo, akihama atakuwa kama alivyokuwa Lyatonga. Chama kinambeba kwa kiasi kikubwa mno licha ya umaarufu alionao.
Tatizo mwenye saccos yake hataki. Si unaona Lema ameamua kurudi zake Canada baada ya kuona manyokanyoka ya mwenye saccos?!!
 
naunga mkono Chadema

Hao wote wanaotajwa hapo wanawania nafasi ya mwenyekiti Taifa wa chama


Je unamuunga mkono nani kati yao kwa ajili ya mafanikio na ustawi zaidi wa hiyo CHADEMA unayoiunga mkono?


Mbona unajiuma uma mzee tatizo nini?
 
asali sasa imekuwa kahawa, hakuwa akijuwa kwamba itafika siku kama leo mambo yk yote yataanikwa hadharani
 
Hao wote wanaotajwa hapo wanawania nafasi ya mwenyekiti Taifa wa chama


Je unamuunga mkono nani kati yao kwa ajili ya mafanikio na ustawi zaidi wa hiyo CHADEMA unayoiunga mkono?


Mbona unajiuma uma mzee tatizo nini?
Wakianza kampeni nitasikiliza sera zao na kuamua
 
Ameyaongea wapi hayo? Nilichogundua una uelewa mzuri sana , ila lijapo swala la Lissu huwa unamsikiliza vizuri tu, halafu unaamua kumuelewa vile utakavyo siyo kwa ule uelewa wako mzuri bali uutakao kulingana na agemda yako
 
Na harakati zimeanza uko kura feki, akishinda mbowe wameshinda kina wenje
 
Nyie ndiyo mnajitekenya na kucheka. Leo hii Lissu akiamua kutoka CHADEMA basi itakufa rasmi. Mbowe amechokwa mpaka basi. Miaka 20 kwenye madaraka kiongozi hata uwe mzuri gani ni lazima utachosha watu na watakuchukia. Ni kweli Mbowe atakuwa amejenga mtandao wake ndani ya chama lakini hawa ni watu wachache sana. Chama siyo mtandao wa mwenyekiti bali chama ni wanachama na wapenzi. Akijidanganya na kukubali kusaidiwa na CCM kupora uchaguzi basi atabaki yeye mwenyewe na wafuasi wachache kama Lipumba. Haya mambo hayahitaji ujanja ujanja wa kibongo kama unavyotaka kuleta hapa.
 
Yaani hapo Mbowe anaona namna anavyokataliwa,hata watu wake wa karibu pia wanaona,tatizo ni mfumo.Atapewa na anapewa kilakitu ahakikishe Lissu hashindi.
 
Mbona hilo lipo wazi kabisa. Lisu akiwa mwenyekiti ataisumbua serikali ya Puerto Rico katika jumuiya ya kimataifa na ukizingatia hawapendi kuchafuka. Maana Lisu anaweza kuwa anaitisha matamko na maandamano hata peke yake ilimradi akamatwe atengeneze habari jumuiya ya kimataifa.

Ingekuwa ni Uganda kwa Museveni, wala asingemuogopa Lisu, lakini kule Puerto Rico, unafiki mwingi hawapendi kuonekana wabaya jumuiya ya kimataifa, hivyo Lisu anaweza kuwachafua bure!
 
Sipati picha Mbowe akirudi madarakani, sijui atakuwa anawaambia nini wanachama wake ambao kwa asilimia kubwa wamemchoka tu automaticale, na siyo kwamba amefanya kosa, la hasha, ni hali ya kuchokwa tu baada ya miaka 20.

Huko Zito na ACT wenyewe wanataka Mbowe ashinde uenyekiti ili ACT kiwe chama kikuu cha upinzani mana CHADEMA itaenda kujifia kwa sababu ya Mbowe kuwa mwenyekiti
 
Mkuu wewe uko mbele ya wakati ktk fikra na upeo. Umepita mule mule.
 
Hivyo tunaita ramli chonganishi.
 
Whatever the case.. Kuna mkono wao juu ya hili
 
 
Vitu 2, kwanza mfumo, pili familia kwa sababu Chadema ni saccos ya familia ya Mbowe.

Malengo yake ni kupiga ruzuku tu na pia mfumo kuntumia kama chombo chao cha propaganda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…