Ni kweli kwamba nafasi za polisi zimetoka?

Ni kweli kwamba nafasi za polisi zimetoka?

TANGAZO LA AJIRA
Jeshi la Polisi liko katika mchakato wa kuajiri vijana kujiunga na Jeshi kupitia mashuleni.
Tumeamua kuurudia utaratibu ambao ulikuwepo zamani wa kuajiri moja kwa moja toka mashuleni ambao ulikuwepo siku za nyuma kutokana na mahitaji halisi ya Jeshi la Polisi kwa sasa.
Hivi sasa Jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazotokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, ongezeko la uhalifu mpya kama vile wizi wa kutumia mtandao, usafirishaji haramu wa binadamu na kadhalika. Wahalifu wanaohusika na matukio kama hayo, wamekuwa wakitumia mbinu mpya na utaalamu wa hali ya juu.
Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea na Programu yake ya maboresho. Maboresho haya yanalenga kulifanya Jeshi kuwa la Kisasa zaidi ambalo litatelekeza majukumu yake kwa Weledi huku likiwa karibu zaidi na raia katika utendaji wake wa kila siku.
Kutokana na changamoto hizo, Jeshi la Polisi linahitaji kuajiri, vijana wasomi, wenye utashi, ari na nia ya kufanya kazi za Polisi na wenye fikra na mtazamo unaoendana na dunia ya sasa.
Vijana hawa watakuwa viongozi na chachu katika kuleta mabadiliko yanayokusudiwa ndani ya Jeshi la Polisi.

A: – SIFA/VIGEZO VYA MWOMBAJI
1. Mwombaji awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
2. Awe na afya njema iliyothibitishwa na Daktari wa Serikali.
3. Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.
4. Awe na tabia njema na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
5. Awe amemaliza Kidato cha sita mwaka 2012 na kufaulu.
6. Awe na umri kati ya miaka 18 na 25.
B: MASHARTI KWA MWOMBAJI
1. Kila mwombaji awe tayari kufanya kazi mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2. Kila mwombaji awe na ari,utashi na nia ya kufanya kazi ya Polisi.
3. Kila mwombaji aandike namba yake ya simu na anuani yake ya kudumu kwa usahihi ambayo itatumika wakati wa kuitwa kwenye usaili.
C: FOMU ZA KUJIUNGA ZINAPATIKANA:
• Ofisi ya Mkuu wa shule
• Ofisi za Makamanda wa Polisi Mikoa/Wilaya zilizo karibu
• Pata fomu hapa(sel-form)

hapo kwenye red kwani kidato cha sita wameshamaliza 2012:lol:
 
nadhani kutakuwa na makosa kwenye tangazo hili. Kwa uelewa wangu hapa naona sasa hivi polisi watakuwa wanachukua candidates kuanzia form 6 na kuendelea juu badala ya form 4, ambapo f6 watakuwa ni wale watakao kula mbavu/vumbi and then graduates wataanza na nyota 1 (assistant inspector) kwenda juu. Nina uhakika na ninachokiandika
 
Jamani kazi hii ya polisi ni ya kweli "search 'Tanzania police force" kuna tangazo pale.

Nimejaribu kuulizia kwanini wanataka kidato cha sita tu, nimejibiwa kuwa ktk masuala ya usalama ni vizuri zaidi ukipata vijana ambao hawako exposed sana na mambo ya mtaani (esp. jeuri, utii, utapeli, n.k) ukilinganisha na hao wanaotoka shule (they are believed to be loyal and submissive). Nilishindwa kuendelea kuuliza sababu jibu niliona kama limejitosheleza kidogo. Na hao form six wanasubiliwa wamalize kwanza shule ndio maana baadhi ya fomu za kujiunga zipo huko mashuleni kwao.
 
Umeniacha hoi graduate hana cha zaidi ! Dah labda wewe huja-graduate ndo maana huwezi kutambua utofauti ! Na kama ume-graduate basi ni vyuo vya kariakoo!
 
Back
Top Bottom