Ni kweli Luteni Urio alitoa taarifa ya tukio au baada ya kushtukiwa mpango wake akawageuka?

Urio yaliyomkuta anayajua yeye na Mungu wake !! kifupi ni wa kumhurumia - usifikiri anafika hatua ya kumkana Baba yake mdogo kwa bahati mbaya.
Hivi ni kweli alimkana baba yake mdogo,, kwaninj kibatala hakumkomalia hapo?
 
Inawezekana
 
Wewe ukweli unaujua? Acha tabia za kidikiteta. Zama zimebadilika
 
Dalili za ujinga unazo
 
Conspiracy theory...kwa mwenendo wa Shauri mahakamani hauko mbali sana na dhahania yako.

Time will tell soon.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna Mchagga asiye na Kadi ya chadema
 
Sio kweli
Mwaka 1995 hakuna Mchagga ambaye kiuwazi au kisiri hakuwa kwa mrema, na mwaka 2015 hakuna mchagga hakuwa mwanachama au mpenzi kiuwazi au kisiri wa chadema
 
Yule alikuwa dalali wa kuunganisha mbowe apate walinzi sema alipodakwa (walikuwa wanafuatiliwa kimtandao)ndio akaamua kubadilishia gia angani kwa kupangwa aseme mbowe ni gaidi ila yeye kama yeye mpaka sasa yuko chini ya ulinzi mkali tena sana.
Na baada ya kesi kuisha au kufika muafaka yeye kama yeye huenda akashtakiwa kijeshi vile vile na kazi huenda akakosa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nina hasira na goodluck Kingai jumanne swila Mahita na msekwa. Hawa wameua ndugu zetu hawawezi kujikausha hivi hata kwa shiriki wajue tupo front kwa mparange tutawafikisha
Kingai , Mahita na Jumanne hawataiona Mbingu
 
urio anapofanya uhai wake kufa au kupona
 
General Lengai Ole Sabaya
 
Hivi ni kweli alimkana baba yake mdogo,, kwaninj kibatala hakumkomalia hapo?
Huwezi kukomalia swali moja alilokwisha likana. Unaendelea kuuliza maswali mengine. Mahakamani siyo kukomaliana, ni kuuliza maswali kwaajili ya kujenga doubts. Maswali mengine ni kumuonesha shahidi kwamba tunajua mengi juu yako. Huko mbele kwenye zamu ya mashahidi wa utetezi, haya maswali ya sasa yanakua yamejenga msingi kwa ushahidi wao.

Kibatala anaposema "Acha ikae hivyo" anajua ameweka akiba huko mbele. Urio kumkana baba yake mdogo na mambo mengine aliyoyakana, yatawekwa sawa na mashahidi wa utetezi.
 
Huyu alikuwa anaatoa maelekezo tu
Kingai, Jumanne, Mahita, Goodluck, wote walikua ni kutoka polisi Arusha ambako Sabaya ndiyo base yake iliko. Sabaya ndiye aliye organise huu mchongo, na hakutaka kutumia polisi wa Moshi kwa sababu hakuwa na good terms na Polisi Moshi (Kilimanjaro).

Kumbuka yule RPC aliyekua Kilimanjaro ambaye sasa ni Mkurugenzi wa TAKUKURU, alimkatalia wazi kabisa juu ya tuhuma alizozitunga Sabaya kwa wamiliki wa mabasi ya Lim Safaris na Machame Safaris, kuhusu kuharibu miundo mbinu ya Reli. Ulikua ni mchongo wa Sabaya kuwatuhumu uongo wafanyabiashara wale.

Kutokana na kutokua vizuri na Polisi Kilimanjaro, aliamua kutumia polisi wa Arusha ambako yuko nao vizuri na ndiko vilikua viwanja vyake na amekulia huko akiwa UVCCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…