POTOSHI Ni kweli Lyanco alifika mazoezini akiwa na majeraha

POTOSHI Ni kweli Lyanco alifika mazoezini akiwa na majeraha

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Lyanco temp.jpg

1773132911604.png
 
Tunachokijua
Machi 09, 2026 katika mchezo wa timu za Brazil zilitolewa kadi nyekundu 23 baada ya ugomvi mkubwa kuibuka uwanjani. Timu zilizokuwa zikicheza ni Cruzeiro pamoja na Atletico Mineiro kwenye fainali ya Campeonato Mineiro.

Madai

Baada ya tukio hilo, machi 10 zikasambaa picha zinazomuonesha mchezaji wa timu ya Atletico Moneiro, Lyanco Evangelista akiwa mazoezini huku usoni akiwa na majeraha na kuelezwa kuwa amerejea mazoezini akiwa na majeraha hayo.

Uhalisia: Potoshi

Baada ya ufuatiliaji JamiiCheck imebaini kuwa picha hiyo imehaririwa kwa Teknolojia za kidigitali kutoka katika picha halisi ya mchezaji huyo.

Picha hiyo inayomuonesha Lyanco akiwa na majeraha usoni imeaririwa kutoka katika picha yake halisi ambapo vyanzo mbalimbali vilichapisha vikimuonesha akiwa na mazoezini.

Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa hata picha halisi haihusiani na tukio la Machi 10, 2026, Mathalani tovuti moja ya ilichapisha taarifa pamoja na picha hiyo katika makala yake ya Machi 03, 2026 wakieleza kuwa Lyanco amerejea mazoezini baada ya majeraha aliyoyapata.
Back
Top Bottom