Ni nadra sana kunikuta najadili maisha ya mtu binafsi. Lakini kama mjadala huo utakuwa unahusiana na jambo lolote linalogusa public interests, basi huwa sina budi kujadili
Wiki zaidi ya moja iliyopita kumeendelea kuwepo kwa mvutano wa Ramadhan Singano aka Messi wa Simba na klabu yake. Katika hali ya kushangaza, blogger mmoja maarufu nchini (nadhani mtakuwa mnamjua tu) amemshawishi mchezaji huyo wa Simba kuonyesha hali ya maisha yake anayoishi, pengine kwa lengo la kuuonyesha umma kwamba mchezaji huyo amekuwa ananyonywa na klabu yake kiasi kwamba maisha yake yamekuwa duni ukilinganisha na ukubwa wa jina lake. Mchezaji huyo alipigwa picha akiwa ndani na nje ya nyumba yake na kuonyesha vitu vichache anavyomiliki katika gheto alilizamia kwa kaka yake
Nimejiuliza maswali mengi kuhusu kipato alichonacho Messi na hali ile iliyoonekana. Baadhi ya vipato hivyo ni:
1. Hela ya usajili sh. milioni 13 yaani 13,000,000/= aliyopewa mwaka 2013
2. Mshahara kutoka Simba sh. 700,000/= kwa mwezi take home usioguswa na kodi yoyote
3. Gari aina ya Suzuki Carry 4WD la kubeba mizigo alilopewa mwaka 2013 bure na shabiki wa Simba Musley Luwah wa Oman, (kadiria mwenyewe kwa siku 'hesabu' yake ni shilingi ngapi anayoletewa na dereva. Kwa uthibitisho wa hili gari, soma hapa:
Messi wa Simba azawadiwa gari - Global Publishers
4. Posho za klabu yake ambazo hubadilika mara kwa mara (mapato mtakadiria wenyewe)
5. Posho alizokuwa anapata wakati akiwa mchezaji wa timu ya Taifa - kila siku ya kuwepo kambini sh. 50,000/= pamoja na posho nyingine za kucheza mechi
6. Tangazo la biashara analofanya ITV la magodoro ya Dodoma maarufu kama kwa mzee Mangungu (mapato mtakadiria wenyewe)
7. Hela anazookoa katika matumizi anapokuwa kambini na Simba na Taifa Stars (gharama za Hotel malazi na chakula ni juu ya timu). Jaribu kufikiria ni asilimia ngapi ya muda wake katika mwaka anakuwa yupo kambini akila na kulala bure
8. Hili lingine ni personal sana sitalizungumza kwa undani, ila kwa ufupi hana watoto, familia wala wazazi wategemezi so hela nyingi anabaki nazo yeye
Sasa wenye akili mjiulize, ungekuwa wewe ndio kijana unapata mapato hayo, maisha yako yangekuwa ya kichovu vile?
-Vijana wangapi wanahangaika lakini hivyo hivyo wanajitahidi kujitegemea na si kuishi kwa kaka zao?
-Messi kusema ana maisha duni, huku sio kumkufuru Mungu?
-Kama amejibana kwa kaka yake kwenye single room na kuna TV na kitanda na viti vichache, ina maana kaka yake alikuwa hana fenicha yoyote kabisa isipokuwa alikuwa anamiliki chumba tu kitupu?
-Ni kweli pale ndipo anapoishi Messi au ana makazi mengine?
Maswali hayo nawaachia, akili mlizoambiwa za huyo mmiliki wa blogu inabidi mchanganye na zenu, halafu muone kama huyu Messi amefanya usanii wa kutuonyesha chumba feki au ndio chumba chake halisi