Ni kweli maisha ya Messi wa Simba yako hivi?

labda nikusahihishe mshahara wake ni milioni moja na nusu aliongezewa ndio pale panaleta mgogoro maana simba wanasem,a walipo mbadilishia mshahara na mkataba uliongezwa inawezekana kuna watu wanapiga pesa kupitia mgongo wake na ndio hao wanachochea utambi
 
Mkuu, kuna thread nyingi sana zimeanzishwa kuhusu uhalisia wa ile mikataba, na mimi sijataka nizungumzie mambo ya mikataba kwani yameshazungumzwa sana. Hapa nazungumzia kipato cha Messi vs picha alizopiga gheto na jinsi alivyojielezea kuwa 'maskini'. Ni vyema ukajikita katika mada kama unalo la kuchangia
 
Kama ni 1.5 M basi ni kwamba unazidi kuchochea mada, maana kwa mujibu wa habari picha ya ile blog, ni kwamba Messi ana kipato kidogo sana
 
huyu bwna mdogo pia inawezekana hajielew.. elimu ndogo au anauswahili mwingi sana asije akadanganywa then baadaye akajikuta anapotea ktika soka. kama simba wamemfanyia uhuni kwenye mkataba wake hili si jembo jema hata kidogo na siwezi liunga mkono. la msingi sasa wakae watatue jambo hili wakishindana kuna mtu ataathirika...
 

Simba hawana pesa ya kuwalipa wachezaji kama mtoa mada alivyo ainisha wengi wao wanajitolea kwa mapenz yao binafsi na klab. Kama kweli hzo pesa zote zilizoainishwa hapo juu angekuwa analipwa vizr hata muonekano wake ungekuwa nadhifu sasa anaonekana kama mchezaji wa mchangani, viongozi wa simba wangepinga kwa hoja na ushahidi kama kweli messi haishi ktk mazngira hayo,sasa mbn wapo kimya na hawapingi hlo jambo halafu watu wanataka eti waisapoti simba wakati wanawapa wachezaji ahadi hewa.
 
Sakata kama la mesi ndio mambo yanayoharibu mpira wa tanzania.

kitu chochote unapokiendesha kwa mifumo isiyo na usawa hauwezi kupata mafanikio. kuwa na viongozi wababaishaji katika sekita yoyote ndio mwanzo wa sekita husika kuporomoka.

kanuni ya mshahara kwa mfanyakazi au mchezaji ni lazima mshahara uendane na mchango wa mwajiriwa katika kuingiza mapato hasa kwa biashara ambayo juhudi za mtu ndizo zinazoteka soko.

unakuta mchezaji ni tegemeo katika timu lakini kwa kuwa yeye hakuwa mjanja wakati wa kuingia mkataba basi analipwa kidogo huku kuna mchezaji ambaye mchango wake ni hafifu analipwa vizuri sana. kiongozi anayeweza kulea tofauti kama hizo katika timu yake ajue hajui maana ya uongozi maana tofauti kama hizi ndizo hupelekea wachezaji kuwa na uwezo mkubwa lakini kwa tathmini ya jinsi wanavyolipwa wanafanya migomo baridi kwa kuacha kujituma.

kama timu inataka kupata mafanikio itaboresha maslahi ya mchezaji yeyote anayejituma ili yaendane na hadhi ya kiwango chake na hilo huhamasisha wote kwenye timu kuongeza juhudi ili waongeze vipato.

lakini timu zikianza kuona eti huyu tulimsaidia kitu fulani huko nyuma hivyo tunatakiwa kumlipa kidogo hao hawajui wanachokifanya. timu inapofanikiwa kutengeneza star ni kutafuta mbinu zote za kumtumia kufanya biashara kupitia kwake uwanjani na nje ya uwanja lakini ukisikia haya tunayoyasikia basi unajua tuna safari ndefu.

yawezekana yaliyosemwa hayakuwa sahihi lakini kwa kuangalia ni wazi kuwa huyo alitaka kufikisha ujumbe na ujumbe wenye haukueleweka ila yeye alitaka kusema malipo ambayo timu inamlipa mchezaji huyu hayaendani na mchango wake kwenye timu wakilinganisha na jinsi inavyofanya kwa baadhi ya wachezaji wengine.

 
Kama kweli hzo pesa zote zilizoainishwa hapo juu angekuwa analipwa vizr hata muonekano wake ungekuwa nadhifu sasa anaonekana kama mchezaji wa mchangani, ...
Mkuu, suala la unadhifu kwa wachezaji wa bongo sio kipaumbele kwao, wala lisikufanye upate taswira halisi ya maisha yake. Kama wewe ni mpenzi wa jukwaa la michezo humu, bila shaka utakuwa umeisoma thread moja humu iliyokuwa inamzungumzia golikipa Shabani Kado jinsi alivyovaa hovyo huku akijua anaenda kupokea tuzo muhimu sana kwa kumbukumbu ya maisha yake ya soka, yaani tuzo ya golikipa bora wa VPL 2014/2015. Picha za kumbukumbu zitaendelea kuonekana na mavazi hayo ya hovyo, huku akina Ronaldo, Messi, Etoo, Diouf na wengineo huwa wanatupia suti ya nguvu siku ya kupokea tuzo ya mchezaji bora.

Unataka kusema Kado hana kipato cha kununua suti? Unataka kusema Rama Singano Messi hana uwezo wa kununua walau nguo chache nadhifu za kuvaa kiofisi anapoitwa TFF au maeneo mengine ya wadhamini wake mbalimbali? Mbona watu wengi tu wanapoanza ajira, mshahara wao wa kwanza au hata ile hela ya kujikimu huwa tunaitumia kununulia mavazi nadhifu?

Wachezaji wengi (sijasema wote) wa bongo hawajipendi. Timu zao na ya Taifa zinaposafiri nje ya nchi kwa ajili ya mashindano au mazoezi huwa zinawapa suti lakini hawazivai kwenye matukio ya kiofisi, badala yake wanavaa kama Singano, pensi na T-shirt iliyofubaa
 
Dah hii aione shafii Dauda, hapa ndipo tunapowapima waandishi wetu, hawabalansi stori yaani apelekewe hii mada na atupe majibu yasiyo shaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…