Ni kweli maprofessa hawataki kuwa matajiri?

Jay2525

Member
Joined
Mar 5, 2014
Posts
68
Reaction score
120
Ni kweli maprofesa wengi hawataki utajiri?

Binafsi nimekuwa nikijiuliza swali hili kwa muda mrefu sana. Kwani nakumbuka nikiwa mdogo mama aliniambia ukitaka maisha mazuri fanya bidii katika masomo yako,faulu vizuri ili uende chuo kisha utapata kazi nzuri na kuwa na maisha mazuri.

Kauli hii iliniaminisha kuwa elimu ndo kila kitu katika mafanikio.Lakini cha ajabu sasa nipo mwaka wa tatu chuoni na wakufunzi wangu walio wengi ni maprofesa lakini cha ajabu maisha yao ni ya kawaida saana. Hata usafiri wanao tumia hauna tofauti na tax zinazo randa randa mitaani.

Hili lilinifanya nivunje ukimya nu kumulliza mmoja wa wakufunzi wangu ambae ni profesa kwamba mbona yeye sio tajiri ijapokuwa anaelimu kubwa na kazi nzuri ya uhadhili? akanijibu amejitolea kuhudumia jamii.

Utajiri sio kipaumbele maishani mwake. Jibu hili ndio msingi wa swali langu wanajanvi naomba majibu.

Je ? ni kweli maprofesa hawataki utajiri . kwani hata matajiri wengi niwa juao sio wasomi wakubwa
 
Si kweli kwamba kajitolea kusaidia jamii mbona mshahara haachi kuchukua?Kimsingi mleta mada kuna mambo umechanganya.

ELIMU NA UTAJIRI NI VITU VIWILI TOFAUTI.Elimu ya maisha hao maprof hawana hata kidogo.Unaweza ukaanzisha mradi mdogo tu wa kukuongezea kipato,ukimpa profesa ausimamie huenda mradi huo ukafa ndani ya mwezi mmoja.

Mimi mdogo wangu aliacha shule darasa la pili akaingia kwenye biashara.Sasa biashara yake anaenda china na dubai.Mimi nimesoma mpaka chuo kikuu nimeajiriwa lakini sina chochote cha maana zaidi ya haya mavyeti!

Yeye leo anamiliki mjengo mbezi beach,mimi bado nimepanga.Ni kwamba mtaala wa elimu hautufanyi tuwe wabunifu hasa katika maisha.

Janga lingine ni kuamini katika kazi ya kuajiriwa ambayo humfanya mtu awe mtumwa milele wa mwajiri wake ambaye humlipa malipo kidogo ukilinganisha na muda alioutumia kumzalishia mwajiri wake!Ndiyo maana kama ikitokea leo prof.akafukuzwa kazi si ajabu ukasikia amekufa baada ya muda mfupi kwani walio wengi ajira ndiyo kila kitu!
 
Ukiweza kuitumia vyema elimu ulyoipat waweza kuw tajir vinginevyo utakuwa utakuw profesa af maskini au ukawa tajiri..SO USEMI HUO CO WA KWELI
 

Projesa wa CHEMISTRY anashindwa na DK MWAKA kuchanganya dawa na chemical kumpa mgonjwa, Profesa wa PHYSICS anashindwa na ADAM ametengeneza HELKOPTA yeye amebaki na roho mbaya ya kumzuia asitengeneze. Profesa wa KISWAHILI atauza nini??
 
maprofesa wanafanya risk analysis nyingi kabla hawajawekeza...

biashara haitaki uoga... ndio maana wasioenda shule wana win sana sabab hawana uoga....
 
Projesa wa CHEMISTRY anashindwa na DK MWAKA kuchanganya dawa na chemical kumpa mgonjwa, Profesa wa PHYSICS anashindwa na ADAM ametengeneza HELKOPTA yeye amebaki na roho mbaya ya kumzuia asitengeneze. Profesa wa KISWAHILI atauza nini??
Nimeipenda
 
Ulisomea nini yawezakuwa ni degree ya international relationship
 
We umeshaambiwa utajiri sio kipaumbele chake hili ndilo la msingi maana muda mwingi anautumia kufanya machapisho badala ya kuwaza madili ya hela
 
nikisoma list ya matajri,iwe local au ya kimataifa hakuna tajiri hata mmoja aliyeajiriwa hivyo utajiri na kuajiriwa ni vitu viwili tofauti labda mtu achanganye maana ya utajiri na kuwa na maisha mazuri

pili utajiri unataka mawazo kuyafanya kuwa vitu halisi,ma professa wanauwezo wa kuwa na mawazo na kuyarithisha kwa wengine kwa kuyafundisha na sio kuyafanya vitu halisi.hivyo wanabaki kuwa watu wa theory zaidi

utajiri kwa ujumla wake hupatikana ktk biashara,sasa hao ma profesa na wasomi kwa ujumla wanaleta usomi sana when it comes to risks,siri namba moja ya wafanyabiashara ni kutoogopa hatari,wao wanaikabili na kucheza nayo kadri inavyokuja,msomi atasitisha mambo...Msomi sasa hivi ukimpa mtaji millioni 100 afanye biashara kwa utawala huu wa hapakazi tu anaweza kwenda kuiweka fixed deposits mpaka 2020 asome upepo,wakati mkinga mmoja hajaenda hata shule ukimpa millioni 20 tu mpaka 2020 atakuwa anamiliki billioni kadhaa!!
 
Kaka prof gan Engenieer mwenye fedha Tanzania
 
Hakika umesema mameno kuntu yanayo nifanya nijiyafakali kwa kina kuhusu kukabili hatari na sio kuziogopa
 
Kwani huko kwa wenzetu maprofesa maisha yao yakoje ?
 
Nimeipenda

Nchi haina Prof wa ukweli kaka nakwambia, maprofesa wengi wanaroho mbaya afadhali shetani, sasa utajiuliza mtu mwenye elimu kiwango hicho na kama kweli amefanya tafiti za nguvu na zenye aana duniani rohombaya anaitolea wapi??? utasikia prof anamwambia mwanafunzi safari hii lazima upate karai kwenye kozi yangu. huyu anatakiwa afungwe kabisa.

Nenda idara ya Physics, UDSM, hahahahahahaha jamaa wanabaniana hatari. ROHO MBAYA.
 
Ukisoma sana unapishana na mkwanja, wanaishia kupata hela ya nyanya na vitumbua tu
 
Projesa wa CHEMISTRY anashindwa na DK MWAKA kuchanganya dawa na chemical kumpa mgonjwa, Profesa wa PHYSICS anashindwa na ADAM ametengeneza HELKOPTA yeye amebaki na roho mbaya ya kumzuia asitengeneze. Profesa wa KISWAHILI atauza nini??
[emoji33][emoji43][emoji43][emoji43][emoji43][emoji43]
 
[emoji13][emoji8][emoji8][emoji115]
 
Biashara ni kipaji pia kumbukeni na sio kila mtu kufanya fanya tu hata kama hana morali na biashara, yes there are people who are born to work for others, infact watu wote hawawezi jiajiri ( who will work for other one?) hivyo society lazima iwe na watu wa aina zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…