Ni kweli maziwa ya 'FORMULA' yana madhara?

Ni kweli maziwa ya 'FORMULA' yana madhara?

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
70,916
Reaction score
141,437
Habari za asubuhi wapendwa.

Kuna mtoto wa jamaa yangu ameugua kama wiki tatu hivi, vipimo vilionesha ana uvimbe kwenye ubongo.

Hivo anatakiwa aende India kwa matibabu, siku walioanza kufanya process za kuandaa safari bahati mbaya mtoto akafariki kesho yake rest in peace baby boy, inauma sana alikua ana miaka 7 tu.

Baada ya msiba kuisha wazazi wakarudi kwa daktari kuuliza nini kinaweza kuwa chanzo cha huo ugonjwa. Wakaambiwa ni maziwa ya formula, huwa yana chemicals ambazo zinaweza kusababisha infection na ndio yamemsababishia infection kwenye ubongo.

Nimehisi ganzi kusikia chanzo cha ugonjwa nikiangalia makopo niliopanga hapa ndani Mungu asaidie, wataalamu wa afya naombeni kujua.

Haya maziwa yanatengenezwaje? Ni maziwa kweli au ni mchanganyiko tu wa vitu hadi wanapata hiyo kitu, na madhara yake? Na pia yaweza kua chanzo cha hilo tatizo kweli?

Cc: gorgeousmimi, Karucee, asakuta same na jf doctors

NB: Kama madaktari wanalijua hili kwanini sasa wanashauri tutumie?
 
Mimi mtoto wangu wa 4 months tulimuanzishia S26 aliharisha kwa siku kama 3 hivi na alivyoenda kliniki mwezi ule alidrop grams kadhaa!wakashauri lactogen no 1 nimenunua lakini mama yake anayaogopa hata hayo!
 
Mi niliambiwa lactogen imechakachuliwa sana, natumia hiyo S26, na sijaona shida yoyote ila hii habari imenishtua kwakweli
maziwa ya ng'ombe nlisoma mahali not recommended kwa umri chini ya mwaka, studies inasemekana kuna uwezekano mkubwa wa kusababisha kisukari kwa mtoto baadae
 
Kwa kweli mimi na ndugu zangu Mara nyingi tunatumia S26 sijawahi pata shida yoyote au kusikia tatizo lolote kwao,nakumbuka mwezi 4 iliyopita Dada yangu alijifungua na day one tulimpa huyo mtoto maziwa hayo maana alikuwa analia sana sababu ya njaa na mamaye maziwa yalikuwa hayatoki mpaka Leo yuko vizuri. Pia niko orphanage center fulan Mara nying ndo hayo yanatumika.Sijawah ona shida yoyote.

Kikubwa ni nikuangalia expire date yake,pia kujua brand original yake ni ipi,Mara nyingi tumejikuta tumetumia vitu fake bila kujua,Ngoja wake wataalam watujuze zaidi.
 
Kuna duka moja nilinunua, nikakuta yameandikwa kiarabu tu nami nlizoea yaloandikwa kiswahili
muuzaji akasema hayo ndo mazuri sababu ndo na wao wanatumia yenye lugha ya kiswahili wanachakachua
hainiingi akilini, hayo ya kiarabu yanauzwa bei rahisi kulinganisha na hayo mengine, lugha nayo ni kipimo cha ubora kweli?mi nadhani lugha ni kuleta uelewa tu kwa watumiaji
 
Rahisi aghali......yanauzwa rahisi ila gharama zake ndo kama hivyo kwa mtoto,Haya yenye lugha ya kiswahili ndo yako recommended,japokuwa hospitalini wanakataza mtoto mchanga kupewa maziwa lakini doctor akiona mtoto anateseka sana na Njaa anakwambia mpe maziwa , na haya ndo wanashauri yatumike na pia yamethibitishwa na mamlaka Husika, sasa hayo ya kiarabu sidhani hata kama yanamethibitishwa na TFDA na TBS.
 
Habari za asubuhi wapendwa.....
kuna mtoto wa jamaa yangu ameugua kama wiki tatu hivi, vipimo vilionesha ana uvimbe kwenye ubongo
hivo anatakiwa aende India kwa matibabu, siku walioanza kufanya process za kuandaa safari bahati mbaya mtoto akafariki kesho yake rest in peace baby boy, inauma sana alikua ana miaka 7 tu.
baada ya msiba kuisha wazazi wakarudi kwa daktari kuuliza nini kinaweza kuwa chanzo cha huo ugonjwa. Wakaambiwa ni maziwa ya formula, huwa yana chemicals ambazo zinaweza kusababisha infection na ndio yamemsababishia infection kwenye ubongo....
nimehisi ganzi kusikia chanzo cha ugonjwa nikiangalia makopo niliopanga hapa ndani Mungu asaidie...wataalamu wa afya naombeni kujua
haya maziwa yanatengenezwaje? Ni maziwa kweli au ni mchanganyiko tu wa vitu hadi wanapata hiyo kitu, na madhara yake? Na pia yaweza kua chanzo cha hilo tatizo kweli?
Cc: gorgeousmimi, Karucee, asakuta same na jf doctors

NB: kama madaktari wanalijua hili kwanini sasa wanashauri tutumie?
Infant formula milk huwa basically yanatengenezwa from cow's milk; from cow's milk wanaongezea some nutrients ili ziwe easily digestible kwa mtoto, na pia huwa wanaongeza chemicals for preservation purposes(preservatives) ili yasiharibike(hii ndio aina ya maziwa ambayo inapatikana kwa wingi katika maduka yetu); Kuna pia soy milk ambayo yenyewe hutengenezwa from protein za mimea; hivyo huwafaa watoto ambao wana allergy na cow's milk au lactose(carbohydrate inayopatikana kwenye maziwa ya ng'ombe).
Kwa upande wa madhara yake, labda tuyaseme kwa kuyalinganisha na maziwa ya mama; kwamba formula milk hayatoi protection ya antibodies ambayo inapatikana kwenye maziwa ya mama, na kwamba maziwa ya mama yanameng'enywa kwa urahisi zaidi,tusisahau pia the possibility ya maziwa haya kuwa na sumu au chemicals ambazo zinakwenda kumdhuru mtoto,kwa sababu yanatengenezwa na binadamu,na binadamu huyo pia ana makosa na mukusudi yake pia(mnakumbuka ishu ya ile batch fulani ya maziwa ya lactogen iliyokamatwa kwamba ina contain a harmful chemical na yale maziwa kuharibiwa?)--This is even more important katika nchi zetu za dunia ya tatu ambazo ni jalala ya kila bidhaa zenye ubora na zile zisizo na ubora. kiufupi all factors in check.... maziwa ya mama is the best option kwa mtoto.
Now the million dollar question...... Kwanza from your story ni ngumu kujua nini hasa lilikuwa tatizo la mtoto wa jamaa yako.... was it uvimbe kwenye ubongo au infection kwenye ubongo??(uvimbe kwenye ubongo na infection kwenye ubongo ni vitu viwili tofauti). Nitajaribu kujibu swali lako kwa assumption kwamba ilikuwa ni uvimbe kwenye ubongo; Mpaka sasa hakuna evidence yeyote ambayo inaonyesha uhusiano kati ya formula milk ingestion during infancy na kupata uvimbe kwenye ubongo(brain tumours), baada ya kusoma story yako nilijaribu kupitia research database tofauti tofauti on the issue, but sikupata any research au article ambayo inaonyesha uhusiano wa aina hiyo; ISIPOKUWA, pale ambapo maziwa hayo yalikuwa contaminated na dawa za kuua wadudu wa mashambani (pesticides). Having said so, risk factors ambazo zimekuwa associated na uvimbe kwenye ubongo kwa watoto generally zimekuwa classified katika ma group mawili; Na katika nchi zetu za dunia ya tatu ni ngumu sana ku point katika kitu kimoja na kusema kwamba it was this or that.
The first group of risk factors ni GENETIC FACTORS-Hapa tunakutana na vitu kama hisstory ya any cancer in aparticular family(great grandfathers/parents/siblings)-maana some cancers zinakuwa na familial tendency na zinakuwa carried over vizazi na vizazi, Lakini pia baadhi ya watoto huwa wanakuwa na vinasaba(genes) ambazo zinawafanya wawe more likely kupata aina fulani ya kansa. Wanasayansi wame identify genes(vinasaba) kadhaa ambazo ziko associated na kansa za aina tofauti tofauti za utotoni; Na mwisho kabisa ni mutations ambazo zinaweza kutokea katika our genetic make up(mabadiliko katika vinasaba ambayo yanapelekea mtu kuwa na chance kubwa ya kupata cancer)
Group la pili sasa la risk factors hizi ni ENVIRONMENTAL FACTORS, hapa tunakutana na vitu na kemikali tofauti tofauti katika mazingira yetu ambazo zinaweza kupelekea mtoto kupata cancer kama ifuatavyo....
-Exposure ya mtoto kwa dawa za kuulia wadudu mashambani(pesticides)-hii inaweza kutokea kupitia kwa mama wakati wa ujauzito hasa kama mama akinywa maziwa ya ng'ombe ambae amekula majani yaliyokuwa contaminated na baadhi ya pesticides kama heptachlor, mfano mwingine ya exposure hii ni kupitia air pollution, especially kama mtoto anaishi karibu na kiwanda kinachotengeneza pesticides hizo
-Unywaji wa vinywaji vitamu vya kwenye makopo;soda,juice-- vinywaji hivi vina kemikali inayoitwa ASPARTAME ambayo inasemekana kusababisha cancer
-Exposure to ionizing radiation rays-- through x rays, radiotherapy.
Sijui kama nimejibu maswali kiufasaha na kama ulivyotaka;Ishu ya uvimbe wa kwenye ubongo kwa watoto bado vitu vingi vinaendelea kujulikana na wanasayansi as days go by, it is still a growing field na bado vitu vingi havijulikani vizuri. Nisamehe kwa kuchanganya lugha. Kama kuna mtu anahitaji ufafanuzi zaidi au hajaelewa anakaribishwa kwa swali au addition au substraction yoyote Evelyn Salt
 
huyo daktari aliyewaambia hivyo ni wa wapi?
study za kuhusisha visababishi vya kansa vinachukua hata miaka 50-100 na mimi sijawahi kusikia hiyo study.
naweza kusema ni uongo huo mpaka hapo nitakapoiona hiyo study au kuisikia.
Japo ni ukweli uliowazi kuwa maziwa ya mama yanafaida kubwa sana kwa mtoto.
 
Rahisi aghali......yanauzwa rahisi ila gharama zake ndo kama hivyo kwa mtoto,Haya yenye lugha ya kiswahili ndo yako recommended,japokuwa hospitalini wanakataza mtoto mchanga kupewa maziwa lakini doctor akiona mtoto anateseka sana na Njaa anakwambia mpe maziwa , na haya ndo wanashauri yatumike na pia yamethibitishwa na mamlaka Husika, sasa hayo ya kiarabu sidhani hata kama yanamethibitishwa na TFDA na TBS.
Mmh na kweli sioni hata ile nembo ya TBS kwenye kopo
 
Ahsante kwa maelezo yako daktare Dr. Wansegamila
hayo ni maelezo ya mama wa mtoto, kuwa huo uvimbe ni infection na ni kwasababu ametumia sana hizo formula na cerelac
 
Last edited by a moderator:
Ahsante kwa maelezo yako daktare Dr. Wansegamila
hayo ni maelezo ya mama wa mtoto, kuwa huo uvimbe ni infection na ni kwasababu ametumia sana hizo formula na cerelac
Eti we uko Dar? Na kama ni yes unanunua wapi Formula? Kuna sehem mwenge formula 2 shs 14,000 . Na kuna sehem supermaket Tbt hiyo hiyo shs 19,000. Niko njia panda
 
mwanangu ameanzaga ya ng'ombe akiwa na mwezi mmoja wakati naenda chuo nilikuwa nakamua yakiisha wanampa kidogo ya ngombe km sijarudi, miezi mi3 baadae nikamnyonyesha hadi miezi 6 bila kumpa maziwa mengine, hivi atapata Shida ukubwani au?? ee mola mlinde mwanangu... mhhh naogopa
 
Eti we uko Dar? Na kama ni yes unanunua wapi Formula? Kuna sehem mwenge formula 2 shs 14,000 . Na kuna sehem supermaket Tbt hiyo hiyo shs 19,000. Niko njia panda
Sipo dar, ila huwa nayaagiza dar formula tsh 14000? Hayo hapana kwakweli....s26 ilikua elf 28 mwanza na Dodoma, Arusha sh 31000 dar kuna duka kariakoo bei ya jumla ni 26....from July 1st yamepanda bei ni 31000 sasa hayo ya elf 14 duuuh
 
mwanangu ameanzaga ya ng'ombe akiwa na mwezi mmoja wakati naenda chuo nilikuwa nakamua yakiisha wanampa kidogo ya ngombe km sijarudi, miezi mi3 baadae nikamnyonyesha hadi miezi 6 bila kumpa maziwa mengine, hivi atapata Shida ukubwani au?? ee mola mlinde mwanangu... mhhh naogopa
Kila kitu tunaambiwa kina madhara sa sijui tusionyonyesha inakuaje
 
sina uzoefu na maziwa ya kopo. mtoto wangu alitumia makopo mawili tu ya lactogen akiwa na miezi 6 baada ya hapo mpaka leo anatumia ya ng'ombe' ila daktari hawezi kusema moja kwa moja chanzo cha uvimbe ni maziwa ya kopo. Vipi kuhusu maziwa ya watoto ya soya kusababisha watoto hasa wa kiume kuota manyonyo? Niliskia shemeji yangu akimkataza mkewe kuyatumia. Siku moja nikasoma mahali kuwa matumizi ya muda mrefu ya soya kwa wanawake husababisha vivimbe/fibroids na kuvuruga homoni za uzazi kwa sababu huchochea homoni niliyoisahau jina. Nikajaribu kuhusianisha madhara ya soya kwa wanawake na zile athari za soya kwa watoto wa kiume nikahisi kuna ukweli. Mwaweza kugugo kujihakikishia.
 
Sipo dar, ila huwa nayaagiza dar formula tsh 14000? Hayo hapana kwakweli....s26 ilikua elf 28 mwanza na Dodoma, Arusha sh 31000 dar kuna duka kariakoo bei ya jumla ni 26....from July 1st yamepanda bei ni 31000 sasa hayo ya elf 14 duuuh
kwa hiyo je haya ya formula yatakua kwenye shs ngapi roughly?
 
kwa hiyo je haya ya formula yatakua kwenye shs ngapi roughly?
Formula si ndio maziwa ya watoto kwa ujumla, then ndo kuna aina.
we unaulizia yapi? Hayo nliokuambia yanaitwa S26 gold ndo bei yake hiyo
 
Back
Top Bottom