Jamani,mimi ni mwanafunzi wa shule moja hapa nchini.Niko na rafiki yangu darasa moja,sasa ameingia mgogoro na mkuu wa shule sasa amemuahidi kwamba atamharibia matokeo.Naombeni msaada,ni kweli matokeo yanaweza kuharibiwa na mkuu wa shule?
Ndio anaweza na mwambie huyo dogo nazi haishindani na jiwe kamwe mkubwa atabaki kuwa mkubwa tu... Akitaka ajue Degree inapatikanaje mwambie akifika chuo kikuu azinguane na profesa kama alivyozinguana na huyo headmaster yake ndo atajua Degre inatafutwa au inachukuliwa.
Mwambie asithubutu kuna Kijana wangu alimzingua head moshi tech akakimbia kwa mipango kuwa mwaka unaofuata atafanya paper kama PC lakini siku alivyorequest necta akawa rejected akaambiwa arudi mosh tech akatatue tatizo lake.
Hapo kwenye entry form na photo entry ni pagumu sana, mifumo ya necta iko makini sana kugundua makosa, pia ikitokea kuna tatizo mzigo utamwangukia mkuu wa shule coz yeye ndo anatakiwa kuwa makini kwenye uhakiki wa taarifa za watahiniwa ni pamoja na kuwapa watahiniwa wahakiki taarifa za usajili wao.
Mkuu wa shule anaweza mharibia mwanafunzi kwenye CA, pia kwenye sel-form anaweza recommend vibaya kwa mwanafunzi husika.