Ni kweli mwanafunzi akisoma Shule binafsi hatapewa mkopo akifika chuo?

Umemalza Bro,advance ni ww mwnyw tu ata akipelekwa wapi.Government ni nzur zaidi kulko prvate na misuli mirefu inahtajika zaidi kwa yy,maana apo tokeo lake litachza kwny div 2- 3 kwa f6 km asipoangalia vzur.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kweli boss,muache asome ahakikishe anafanya vzur tu advance.
Heslb lazma wamkumbuke by default

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkopo wenyewe wa HESLB ni Debt Trap sijui kwanini watu huwa mna shobo nayo.

Kopa HESLB Utalipa Mpaka Unastaafu Na Kimshahara Chako Cha Laki 5
 
Ushauri wa hovyo kabisaa! Huko shule za serikali wapo watoto wanapata daraja la kwanza..kwa nn wasiwe wa kwako!?? Yaani unahangaika kumpeleka mtoto private kwa mtaala huu huu,wewe una akili kweli!??

Kama una uwezo peleka mtoto private kwenye shule ambazo hawatungiwi mitihani na necta..kama unapeleka private halafu mtihani anafanya huu wa necta wewe mzazi ni mjinga na unachangia kumfanya mtoto mjinga.

Mtoto wangu amesoma Mbagala secondary o-level na akapata daraja la kwanza..!! Kaenda advanced shule ya serikali tanga,napo kafaulu. Mjengee uwezo wa mtoto wa kujitambua..pesa hazitamfanya ajitambue!! Mtoto km anajitambua anafaulu shule yoyote...
 
Issue ni global compettition Mzazi anayejielewa hamsomeshi.mtoto serikalini ili apate division one watu wanapeleka watoto shule zinazofundisha sio kiingereza tu wanataka mtoto asome international language zingize Kama French ili awe marketable kimataifa.French Necta mtihani wa primary,form four na six huwa wanatunga
 
Hii ni mbaya sana aisee.
Priority haipo Siku hizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mtoto kuwa marketable kimataifa anatakiwa ajue lugha mbili za kimataifa kingereza na kifaransa na Necta hutunga mitihani Yake kuanzia shule za msingi na sekondari wewe nadhani uko usingizi I unakoroma hata huelewi NeCta Ni kitu gani na inafanya Nini utakuwa vile vizee vijinga jinga vilivyo salia serikalini vinavyofanya kazi kwa mazoe mjinga wewe toka staafu mbwa wewe pisha vijana
 
Mimi kaka yangu amesoma 4m1 mpk 4m4 private na 5na 6 serikali mbn anakula boom lake lakin wanaangalia na karo ya shule uliyo soma kama n zaid ya million 4 Hapati mkopo lakin chini y hapo anapata mkopo kwo Hio shule isiwe na karo ndefu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe na mzee wangu mko sawa. Hadi leo sijawahi elewa kwanini alinilazimisha nisome shule ya kata. Yani ningesoma private ningekuwa mbali vibaya mno, namanisha mbali kweli. Hivi unajua tofauti ya shule ya kata na private inayoeleweka au unaongea tu. Wewe si unaamini kufaulu mitihani ndo kuwa na akili? Exposure hainaga mtihani, tutaiona kwenye output zako ukiingia mtaani. Private wengi wanakuwa more advanced zaidi ya kina nani wengine. Ngoja nipate hela nitalipiza kisasi.
 
Ni kweli mtoto akisoma private kwa awamu hii hapati mkopo ,awamu zilizopita walipewa. Mm mtoto Wangu kwasoma private olevel na A-level aka apply mkopo na jina likatoka ktk kundi lililohakikiwa na kuwa sahihi kupata mkopo,sasa yuko chuo mpaka sasa ajawahi kupokea hata sumni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono serikal kukata pesa iwe kwa maskin au tajir
Nchi yetu bado ni maskin na kiwango cha ufaulu kinaongezeka kila siku
Wanaotakiwa kusomeshwa wanaongezeka kila kukicha
Labda serikal ipunguze ukataji wa makato katika kufidia deni na ipunguze riba pia hiyo ndo njia sahihi ya wote kufaidika serikal na mkopeshwaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uhamisho si upo? Lakini pia hizo shule ulizozitaja zina hostel pia kwa gharama ndogo ni wewe kuwa attention machaguo yakitoka kuwahi nafasi za bweni hata kwa kuhonga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najiuliza sipati majibu, kama mkopo anapewa mwanafunzi ili pindi atakapomaliza chuo arejeshe huo mkopo, sasa kwanini kuwe na ubaguzi wa kutoa hiyo mikopo!? Mimi nazani mikopo wangepewa wote wenye vigezo vya kwenda chuo kikuu bila kubagua shule aidha ya serikali au binafsi.
 
Sahvi si naskia Kuna selform wanajazia online ajaze shule ya bweni inayoendana na ufaulu wake.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…