Ni kweli pilau lina sumu zaidi ya 10?

Kwahiyo NyaniNgabu huamini kua mpikaji
ndo unaweza kuifanya pilau kuwa sumu / harmful kwa
mambo yafuatayo:- ??? kama alivyosema mchangia mada aliepita

1.kuweka mafuta mengi sana...watu
wengi wanapopika pilau huweka mafuta
mengi sana kwa madai ya kwamba ndo
linanoga .

2.Uwekaji wa viungo vingi sana ......watu
wengine hupendelea viungo vingi
kwamba ndo linakuwa tamu,hii
hupelekea kuleta shida kwa wengi kwa
kupata gas tumboni au kuharisha pia
mafuta ni sababu.....pia gas ikizidi sana hupelekea vidonda vya tumbo.

3.Wengine hupika lile pilau la vitunguu
maji ambavyo huunguzwa sana na kuwa
vyeusi kabisa .....hii direct kwa kufanya
hivi ni sumu tosha.
 
Last edited by a moderator:

Ushawah kuckia mtu kafa kwa kula pialau?
 
mwengine atakuja sema chai ya rangi kwa mkate ni sumu pia!
 
Ushawah kuckia mtu kafa kwa kula pialau?

Hujawah kuckia mtu ana mrundikano wa sumu mwilini na bado yupo hai? hata kama hufi haraka ila chamoto utakiona kwa hzo sumu unazozipa hifadh mwilin
 
mwengine atakuja sema chai ya rangi kwa mkate ni sumu pia!

:becky: ndio, Kwani hulijui hilo? majani hasa haya ya dukani (viwandani) yana caffeine Chai ya rangi NI SUMU.
 
TFDA .....wako na wanakula pilau pale external
CHEF ......wapo wazuri saana kwa pilau pale Zahir ...Chef pride na Indian dishes hotels..Mimi bado nadhani mtoa mada anaongelea kitu kingine kabisa na siyo PILAU.Hichi kitu naendelea kukitafuta bado au kwa huruma yake atusaidie ili tuendelee kuchangia ubaya wake na au uzuri wake
 
Najifunza hapa. Na nalipenda pilau sanaa
 

Ni pilau la kula, wala usiumize kichwa.
 
Dawa yoyote ikizidi mwilini ni sumu. Kama viungo ni dawa basi vikizidi mwilini vitadhuru huo mwili!
 
Ni pilau la kula, wala usiumize kichwa.

Sawa kabisa...kwa sasa niko juu ya ANDAS na SHISHA...nikuombe tuendelee na mjadala kesho panapo majaaliwa yake Mola.Nimependa saana unvyojenga na kutetea hoja yako....keep it up.
 
Sawa kabisa...kwa sasa niko juu ya ANDAS na SHISHA...nikuombe tuendelee na mjadala kesho panapo majaaliwa yake Mola.Nimependa saana unvyojenga na kutetea hoja yako....keep it up.

ok Karibu tena wakati ujao tukijaaliwa.
 
Dawa yoyote ikizidi mwilini ni sumu. Kama viungo ni dawa basi vikizidi mwilini vitadhuru huo mwili!

hili wazo zuri pia, ubarikiwe kwa maoni mazuri haya.
 

Huyo Daktarı wa Hebalist Feki mimi ni Mzizimkavu ni Daktari wa Hebalist ninasema chakula cha Pilau hakina sumu mbona mimi ninakula pilau zaidi ya miak 50 iliyopita sijadhurika? na lait iPilau ingelikuwa ni Sumu akina Saidi Bakhressa wanaopika Mahotelini mwao Serikali ingesha wapiga marufuku wasiuze Pilau. Usipende tu kila kitu kuikisia na kuamini fanya uchunguzi au uliza kwa wanaojuwa je pilau inapikwa kwa viungo gani? utajibiwa

Mapishi ya Pilau

Karibuni tujifunze kupika pilau.

Mahitaji:
? Mchele kilo 2
? Nyama ya mfupa kilo 2
? Vitunguu maji 2 na karoti kubwa 2
? Viungo vya pilau vilivyosagwa pakiti moja(saizi ya kati) Bizari ya pilau ,mdalasini, hiliki na zabibu
? Viungo vya pilau visivyosagwa
? Chumvi kiasi
? Mafuta ya olive
? Njegere glasi
? Viazi ulaya nusu kilo
? Vitunguu Saumu

Haya kati ya hivyo vifaa vya kupikia hiyo Pilau niambie kipi chakula cha sumu hapo mkuu tomjelly ? Huyo Daktari wa hebalist aliye kuwa anazungumza kwenye TV alikuwa ni Daktari feki tena anatoka mji wa bara hajuwi faida ya kula hiyo chakula cha pilau.


 
Last edited by a moderator:

😎 Asante sana mkuu MziziMkavu kwa ufafanuzi wako na waganga njaa wanaojiita tiba mbadala.

Naomba kujua faida kuu za kula pilau enyi wataalamu.

Mimi nimlaji wa kila aina pilau kuliko maelezo na sijaona hasara yake kwa miaka yangu yote. Na chakula changu migahawani ni pilau au biriani au pizza.
 
Last edited by a moderator:
ahsante sana MziziMkavu kwa kunitoa tongotongo.

Sasa ntaanza kulila kwa fujo, hasa pilau lilioandaliwa vizuri (kitaalamu). Ili nsisumbuliwe tumbo.
 
Last edited by a moderator:
Wataalam wa kiswahili.... vipi niko sahihi "kuila pilau au kulila pilau"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…