Ni kweli pilau lina sumu zaidi ya 10?

Ni kweli pilau lina sumu zaidi ya 10?

Kwa bandiko lako hilo hapo juu naona kama vile na wewe umeanza kuelewa ninavyo elewa mimi hasa pale ulioosema siyo lazima ufe au udhurike mapema.

eti eeh, Basi sauuuwah! ila nahisi tu unachowaza japo sina hakika. kwanin usiwe muwaz mkuu.
 
Kumbe unazungumzia uwezekano huko mbeleni!

Kwa maana hiyo si jambo la uhakika kuwa kweli pilau ni sumu bali ni suala la ubashiri tu.

Halafu, shida ni sehemu ya maisha hususan uzeeni.

Sijawahi kukutana na mtu mwenye umri mkubwa asiye na matatizo ya kiafya.

Hivyo, uepuke kula pilau usiepuke...matatizo ya kiafya yatokanayo na umri kuwa juu yatakuwepo tu.

Bado siamini pilau ni sumu.

we kubali kataa ila kuchukua tahadhari ni jambo muhimu sana. kuna uzee wenye shida nying na uzee wenye shida chache za kiafya.
 
Mkuu mimi niliwahi sikia ila pia nikasikia inategemea na namna pilau linavyopikwa.

Nasikia upishi unaotumika sana mitaani wa kuunguza viungo sana ndio sababu ya pilau kuonekana sio chakula chenye kujenga afya.

Pia nasikia kuna michanganyiko ya viungo inayoweza kuzalisha sumu baada ya kula. Mfano inashauriwa usitumie kitu kichachu halafu hapo hapo ukala kitamu ili kutozalisha sumu mwilini. Hapo unajiuliza mbona vyote ni vilaji vya asili, kwanini viwe na madhara?

Kuhitimisha tu, niseme kwamba, uunguzaji wa viungo vya kupikia pilau ndio chanzo cha kudhuru tumbo.

Ahsante kwa ufafanuzi huu murua. ILA MWENZENU hapa na leo Tena wamepika pilau maharage. KARIBUNI.
 
we kubali kataa ila kuchukuatahadhari ni jambo muhimu sana. kuna uzee wenye shida nying na uzee wenye shida chache za kiafya.
o

Kuna ushahidi unaohitimisha kuwa pilau ni sumu au kilichopo ni hisia tu?
 
o

Kuna ushahidi unaohitimisha kuwa pilau ni sumu au kilichopo ni hisia tu?

99% ya style ya uandaaji wa pilau ndo husababisha chakula hichi kiwe sumu. ni wapish wachache sana wanaoweza kupika pilau lisilo na madhara.
 
Elimu elimu elimu,sio unaweza pilau tu

hahahah hujui kua unaweza ukawa unajua mambo makuubwa afu ukashindwa kujua vitu vidogo sana. hii haijawah kukutokea. elimu haitakufanya ujue kila kitu bali itakufanya ujue vingi.
 
99% ya style ya uandaaji wa pilau ndo husababisha chakula hichi kiwe sumu. ni wapish wachache sana wanaoweza kupika pilau lisilo na madhara.

May be lakini pilau ni bora zaidi kuliko wali rosti ukitizama ubora wake kwa nutrients
 
Hujaweka ushahidi wowote ule.

Unasema tu.

vitu vingine sio mpaka uthibitishiwe bali unatumia "common sense" tu. hivi wewe hata kwa kufikiri tu! hujui kua pilau lenye mafuta meng tena yenye lehemu na viungo ving vilivyounguzwa litakudhuru?
 
May be lakini pilau ni bora zaidi kuliko wali rosti ukitizama ubora wake kwa nutrients

Hii ni kweli endapo tu hivyo vinavyoleta hizo nutrients havitaunguzwa (pengine had kua mkaa) kama wafanyavyo wapish wengi.
 
vitu vingine sio mpaka uthibitishiwe bali unatumia "common sense" tu.

Sasa kama hakuna uthibitisho kuwa pilau ni sumu kwa nini udai kuwa ni sumu? Msingi wa hilo dai lako ni nini? Uhalisia/ ukweli au hisia tu?

Huwezi kusema kitu fulani ni sumu halafu ukiombwa uthibitisho/ushahidi kwamba ni sumu, unakosa jibu.

Kumbuka kuwa hisia zako si lazima ndo ziwe uhalisia wa jambo.

hivi wewe hata kwa kufikiri tu! hujui kua pilau lenye mafuta meng tena yenye lehemu na viungo ving vilivyounguzwa litakudhuru?

Pilau ina madhara gani?

Nani keshawahi kudhurika na alidhurikaje?

Na una uhakika gani alidhurika na pilau na si kitu kingine?
 
Sasa kama hakuna uthibitisho kuwa pilau ni sumu kwa nini udai kuwa ni sumu? Msingi wa hilo dai lako ni nini? Uhalisia/ ukweli au hisia tu?

Huwezi kusema kitu fulani ni sumu halafu ukiombwa uthibitisho/ushahidi kwamba ni sumu, unakosa jibu.

Kumbuka kuwa hisia zako si lazima ndo ziwe uhalisia wa jambo.

Pilau ina madhara gani?

Nani keshawahi kudhurika na alidhurikaje?

Na una uhakika gani alidhurika na pilau na si kitu kingine?

duh! huu ni zaidi ya ubishi.
 
ndio mimi hapa. mara nying nkila pilau tumbo hunisumbua sana.

Hilo huenda ni tatizo lako wewe tu.

Huenda una mzio na viungo flani flani vitumiwavyo kwenye pilau.

Lakini haimaanishi kwamba pilau ina sumu.

Hata mimi nikinywa maziwa bila kuyachemsha tumbo langu huvurugika.

Lakini hiyo haimaanishi maziwa yana sumu.

Kuna watu wengine wakila mayai wanaugua. Lakini haimaanishi mayai yana sumu na watu waache kuyala.

Kama wewe pilau husumbua tumbo lako basi acha kulila. Mimi halinisumbui na ntaendelea kulila hadi siku yangu ya mwisho.
 
Back
Top Bottom