Ni kweli raia tunatakiwa kuhamia Burundi. Gharama za maisha zinazidi kupaa

Ni kweli raia tunatakiwa kuhamia Burundi. Gharama za maisha zinazidi kupaa

mwelemimmongo

Member
Joined
Feb 16, 2021
Posts
96
Reaction score
76
Jamani vitu vinazidi kupaa bei kana kwamba hatuna wa kutusemea,jmosi nilinunua cement kwa 20,000/=

Leo nimedamka tena kwenda kununua cha ajabu,imepanda na kufika 21000/=
Sasa najiuliza hii cement nayo inatoka ng'ambo ya nchi? Je shida ni material au mafuta au nini au serikali nayo imeongeza tozo?

Nenda sabuni B29 au mo29 kipande kimoja mia tano,
Mafuta yote juu
Bati juu
Sukari juu
Nondo juu
Kweli sasa naaza kuelewa maana ya tanzaniatozo,
Eti wadau shida nini?
 
Mchawi ni serikali kuchapisha sana pesa baada ya uchaguzi na kipindi cha corona
 
Nchi imeshakuwa ngumu sana hii kuishi. Hangaya mwenyewe muda wote anawazia uchafuzi wa 2025 na pia kuvizia visafari vya Scotland.
 
Nchi imeshakuwa ngumu sana hii kuishi. Hangaya mwenyewe muda wote anawazia uchafuzi wa 2025 na pia kuvizia visafari vya Scotland.

Mama Samia amkumbushe huyo wakili aliyepo hapo benki kuu kuwa kazi KUU ya BOT ni kuthibiti mfumuko wa bei; huko mtaani watu wanakufa njaa kila kitu bei yake inapaa!!! Hiyo sio ishara nzuri kwa hali ya nchi.
 
Back
Top Bottom