Ni kweli Rais Samia akataa uwanja wa Nzuguni kuitwa kwa jina lake au kuna sababu za kimkakati

Ni kweli Rais Samia akataa uwanja wa Nzuguni kuitwa kwa jina lake au kuna sababu za kimkakati

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Rais Samia Suluhu Hassan ameutunuku jina la Dkt. John Samuel Malecela uwanja wa Nzuguni mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya Nanenane yanayofanyika mkoani humo.

Akihutubia katika hafla ya maonesho ya 32 ya kilimo, mifugo na uvuvi, Rais Samia amesema awali Wizara ya Kilimo ilipendekeza uwanja huo uitwe kwa jina lake, lakini alikataa na badala yake akapendekeza uwe na jina la kitaifa au kutunukiwa jina la kiongozi mstaafu huyo, kutokana na mchango wake mkubwa kwa taifa.
6
Soma pia: Mbunge wa Busega Simon Lesengekile ataka Kariakoo Dabi ibadilishwe jina na kuitwa Samia Dabi



“Wizara walipendekeza uwanja huu uitwe jina langu lakini nikasema hapana… nina heshima kutangaza jina la uwanja huu kuwa Uwanja wa Dkt. John Samuel Malecela,” amesema Rais Samia.

Malecela alikuwa Waziri Mkuu wa Saba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipokea nafasi hiyo kutoka kwa Jaji Joseph Sinde Warioba. Alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kuanzia tarehe 9 Novemba, 1990 hadi tarehe 5 Desemba, 1994 akifuatiwa na Fredrick Tluway Sumaye.

Chanzo: Jambo online tv
 
Nawaza tu kwa sauti,

Utaratibu huu ungekuwepo kipindi kile mikoa inagawanywa, hakika mikoa yetu hii ingeitwa kwa majina ya viongozi,

Mkoani Nchimbi,
mkoani Kikwete,
Mkoani Makamba,
mkoani ....

Hahahaa, dah!!

Hivi hakuna ujanja mwingine wa kuita jina la mahali/eneo jipya isipokuwa jina la viongozi kila mara?
 
Kuita kila kitu jina lake ni kebehi sio sifa. Hao machawa waache kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Waliosomea Cuba wanajua motives behind. Jaji Warioba amerushwa roho kiaina kama mstaafu. Mawaziri wakuu wastaafu ni Warioba, Malecela, Sumaye na Pinda ambao wapo hai hadi Sasa. Kwanini asipewe Warioba kwanza? au sababu ya kuongea kwake ukweli? Sawa tu assume ni kwa sababu Malecela nyumbani ni Dodoma. Tutasubiri wakati mwingine kama Warioba atapewa heshima ya jina!!
 
Sasa hivi unaitwa uwanja wa Le Mutuz
 
Back
Top Bottom