Ni kweli Rais Samia na Serikali hawakujua kuwa bilioni 100 haiwezi kuleta suluhu lolote kwenye hali ya mafuta na mfumuko wa bei? Tunakwama wapi?

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Kati ya Jambo linaloshangaza wengi hadi sasa ni kitendo cha serikali kushindwa kujua kuwa billion 100 isingekuwa Suluhu la ongezeko kubwa la bei ya mafuta ya petrol na dizeli.

Watanzania wengi wasiolewa mambo walidhani kuwa ikiweka billion 100 basi kila kitu kuanzia mafuta na bidhaa zingine zitakuwa nafuu au baadae zitakuwa nafuu lakini ukweli ni kwamba hali inaonesha wazi kuwa mafuta yataendelea kupanda na bidhaa zitaendelea kupanda!

Ni nani aliyemshauri na kumshawishi Rais Samia kuwa billion 100 ruzuku itakuwa suluhu na si kuondoa mlolongo wa tozo zilizopo kwenye mafuta?

Hivi Rais Samia na washauri wake kwanini hawakufikiri kwamba kupunguza mlolongo wa tozo zilizo jaa kwenye uingizaji wa mafuta inaweza kuwa suluhu kubwa kuliko kuchukua billion 100 pesa za walipa kodi na kuzipoteza bure?

Kuna ugumu gani kupunguza au kuondoa tozo za mashirika zaidi ya kumi kwenye mafuta?

Hivi kuwambia watanzania mafuta yamepungua kwa Tsh 150 si ni kuwatania na kuwafanya wajinga?

Kwanini tumetekeza billion 100 na hazijaleta suluhu yeyote?

Bidhaa zote zimepanda bei na zinapanda kila siku na hata bidhaa za stationary na ujenzi zinazidi kupanda na kila mtu anasema shida ni kupanda kwa mafuta!

Hii Tsh 150 itasababisha kushuka kwa nauli na hizo bidhaa? Kwanini tumepoteza tena billion 100 bila sababu?
 
Toxic mouthful mibongo on freak
 
Uwekaji wa 100 billion umeleta nafuu sana kwa bei ya mafuta. Punguzo la 300 Tshs kwa lita ni kubwa ingawa halijakidhi kiu yetu.

Kwa mujibu wa serikali kuondoa tozo kutaanza mwaka wa fedha July 1 baada ya bajeti.

Kwa sasa tozo zilishapangiwa matumizi so tungoje mwezi ujao.
 


[Ni nani aliyemshauri na kumshawishi Rais Samia kuwa billion 100 ruzuku itakuwa suluhu na si kuondoa mlolongo wa tozo zilizopo kwenye mafuta?]Hivi tozo ziliwekwa na rais au na bunge.
Halafu hebu rejea hotuba ya waziri Makamba kuhusu hatua zitakazochukuliwa:-


Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kutokana na mahitaji ya wananchi, maoni na ushauri wa Wabunge, maelekezo ya Chama cha Mapinduzi, na ujasiri wa Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais alitoa maelekezo kwamba mwaka ujao wa fedha ni mbali. Ahueni itafutwe mapema zaidi. Hivyo basi, kama hatua ya dharura, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwamba, katika kipindi hiki kabla hatujafikia mwaka mpya wa fedha, Serikali ijibane na ijinyime na zitolewe shilingi bilioni mia moja (Shilingi 100,000,000,000) kwa ajili ya kupunguza bei za mafuta hapa nchini. Ruzuku hii inatolewa kwa kupunguza matumizi ya Serikali katika kipindi kilichobaki cha mwaka 2021/22. Kutolewa kwa ruzuku hii hakutagusa miradi ya maendeleo ambayo inaendelea. Nafuu nyingine, inayotokana na mikopo niliyoieleza hapa awali, itakuja katika mwaka ujao wa fedha itaelezwa kwa kina zaidi na Waziri wa Fedha kwenye Bajeti ya Serikali mwezi ujao. Mheshimiwa Spika, ruzuku hii ya shilingi bilioni 100 itatolewa kwa ajili ya kupunguza bei kuanzia tarehe 1 Juni 2022. Hii ni kutokana na kuwa, wafanyabiashara wa jumla wamekwisha lipia gharama ya mafuta ambayo imejumuishwa katika bei hizi za Mei 2022 na wafanyabiashara wa mafuta katika vituo wamekwishanunua mafuta kwa bei hii inayotumika sasa. 10 Mheshimiwa Spika, hatua nyingine zisizo za kifedha zinazochukuliwa na Serikali ni pamoja na: (i) Kuruhusu watu wenye uwezo wa kuleta mafuta kwa bei nafuu kufanya hivyo. Wizara imekamilisha kufanya tathmini ya kampuni zote zilizoonesha nia ya kuweza kuleta mafuta kwa bei nafuu kwa lengo la kujiridhisha na uwezo wao wa kuleta mafuta hayo ili kuhakikisha uwepo wa mafuta nchini (security of supply). Mipango hii ikileta matokeo yanayotarajiwa, bei za mafuta zitapungua zaidi kuanzia mwezi Agosti 2022. (ii) Kuanzisha Mfuko wa Kuhimili Ukali wa Bei za mafuta (Fuel Price Stabilization Fund). Serikali imeandaa utaratibu wa kuanzisha mfuko maalumu utakaotumika kupunguza makali ya bei ya mafuta kipindi ambacho bei hizo zinaongezeka kwa kiasi kikubwa. Mpango wa kuanzisha mfuko huu uko katika hatua za mwisho. (iii) Kuanzisha Hifadhi ya Mafuta ya Kimkakati (National Strategic Petroleum Reserve). Serikali inakamilisha marekebisho ya Kanuni za kuanzisha na kuendesha hifadhi mafuta ya kimkakati ili nchi yetu ijihakikishie usalama wa upatikanaji wa mafuta na unafuu wa bei katika vipindi kama hivi. (iv) Kuwa na kituo kikubwa cha mafuta (Petroleum Hub). Serikali inakamilisha makubaliano ya kujenga maghala makubwa ya kuhifadhi mafuta kwa ajili ya kuuzwa ndani na nje ya nchi kulingana na uhitaji. Uwepo wa kituo hiki utawezesha nchi kupata mafuta yenye bei nafuu pale bei zinapopanda kupita kiasi. Mpango huu na utekelezaji wake unaweza kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu. (v) Kuanzisha upokeaji wa mafuta katika ghala moja (Single Receiving Terminal – SRT) kupitia maghala ya TIPER ili kupunguza au kuondoa gharama za meli kusubiri au kuchukua muda mrefu katika upakuaji wa mafuta katika maghala mengi. Gharama hizi nazo zina mchango katika bei ya mafuta (demurrage charges). Hatua hii itaondoa changamoto za udanganyifu na kuongeza ufanisi katika biashara ya mafuta hapa 11 nchini. Hatua hii inaendana na kuyafanya maghala haya kuwa Customs Bonded Warehouse ili kushamirisha biashara ya mafuta yanayokuja nchini na kwenda kwenye nchi nyingine. (vi) Kuiongezea uwezo TPDC kuagiza mafuta nje ya nchi, ambapo kwa mara ya mwisho ilifanya shughuli hiyo miaka 20 iliyopita. (vii) Kuimarisha utendaji na weledi wa taasisi za Serikali zinazoshughulika na biashara ya mafuta nchini, ikiwemo EWURA na PBPA (Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja).


Soma then uje na comments zako
 
Nimeona kwenye jedwali ni 154 kwa diesel.
 
Hivi nyie na akili zenu mlikua hizo pesa zimetolewa kusaidia mafuta??


Toka zimetolew Kuna ahueni ??

Hizo Pesa zimeingizwa kwenye mifuko ya watu ,wahuni waliumizwa miaka 5 ya JPM, Sasa ndo Pesa zao zinarudishwa .
Kna mtu nimemwambia hili suala...hiz pesa zimetafunwa ndio maana wanatumia sana nguvu kutushawishina kwenye document ya bei za ewura wameweka na heading kabisa "JINSI RUZUKU YA BIL 100 ILIVYOPUNGUZA BEI" upumbaaaav mtuup
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…