Ni kweli Robertihno kocha?

Ni kweli Robertihno kocha?

Kuna Vitu Vinafikirisha Sanaa, hasa Ukiangalia Namna Kocha Mkuu wa Simba anavyo ongoza Timu. Nahisi Kocha Wa Simba Anabebwa na Matokeo zaidi kuliko uwezo wake. Najiuliza Maswali Mengi sana

1. Kwanini Kocha wa Simba Anacheza Na Timu as If ina Wachezaji 11 tuu? Kwanini Hafanyi Rotation ya Wachezaji Pamoja na Utitili wa Mechi tulizo nazo?

2. Ndani ya Mwezi wa 10 Simba Imecheza Mechi 6, Mechi za Karibu zaidi ni za Tarehe 20, 24, 28 na Tarehe 05 katika hizi mechi 4 Kocha ameanza na kikosi kile kile, Na Sub Zile zile bila kujari anacheza na nani? Hapa sio Kwamba Kuna Ulakini wa Mbinu?

3. Mechi ya Leo, Kwa Kocha Mwenye Akili Timamu unawezaje Kumuingiza Aishi Manula Ambaye alikuwa majeruhi kwa Muda wa Zaidi ya Miezi 3 halafu unakuja kumuweka Direct kwenye Derby? Yalikuwa maelekezo ya Viongozi au ni Mahitaji ya Kocha? Nje una Ayoub na Una Salim.

4. Saido Alionekana Kuchemsha hii mechi toka Kipindi cha Kwanza, Kwa Kocha mwenye Uwezo unawezaje Kumuacha huyu mchezaji amalize Dakila 90?

5. Inakuwaje kwa wewe kocha Ambaye ni mtaalamu, Timu inatatizo la Beki za Kati kwa miezi 6 sasa, na Hakuna Improvement, Kwanini Usiwajaribu mabeki wengine ulio nao benchi?

6. Kapombe na Zimbwe kwa macho ya kawaida wanaonekana wamechoka, Angalia Magoli ya Leo yaliko tokea, Lakini Kwanini Kocha Umeendelea kuwa King’ang’anizi?

7. Unacho Mpendea Baleke Kwenye Derby ni Nini? Unaogopa kwasababu Phiri hana Rotation nzuri kwenye Kikosi? Baleke Kama Saido na Chama hawako vizuri Baleke ni Pazia tuuu, Kama Kapombe na Zimbwe Hawapigi Cross Baleke Hana Faida Mbele ya Phiri

8. Kama Kocha Kwanini huwaambii wachezaji waachr kurogana? Kramo Angekuwa Mbali Kiasi Gani?

9. Sijaona Mbinu wala Falsafa Ya Mpira wa Robertihno zaidi ya Juhudi Binafsi za Wachezaji.

10. Viongozi wa Simba Kama Mtaenda na Robertihno Makundi ya CAF CL sitashangaa tukiishia hatua ya Makundi.

TUSHINDE AU TUFUNGWE ROBERTIHNO SIO KOCHA SAHIHI WA SIMBA HASA HII yenye wachezaji wengi Wazuri
Mnapojidanganya ni kuamini simb ina wachezaji wazuri!! Umeandika point nyingi lkn mwisho umeharibu.

Simba ni mbovu haina wachezaji wa maana zaid ya majina majina.
 
Timu Mbovu zilizofungwa na Yanga Msimu huu 2023/2024 mpaka sasa;

1. KMC - Goli 5
2. JKT Tanzania - Goli 5
3. AZAM - Goli 3
4. SIMBA - Goli 5
 
Propaganda fc.

Timu haijifunzi aisee.

Ila na wachezaji wa simba ni wazee aloo. Kina Saido, M. Hussein, Kapombe, Bocco.

Haya hawa wengine walikataliwa huko nyie mmebeba chama na miquison.

Na hapo hamjakutana na mume wenu Azam ambae nae lazima awakande.
 
Kuna Vitu Vinafikirisha Sanaa, hasa Ukiangalia Namna Kocha Mkuu wa Simba anavyo ongoza Timu. Nahisi Kocha Wa Simba Anabebwa na Matokeo zaidi kuliko uwezo wake. Najiuliza Maswali Mengi sana

1. Kwanini Kocha wa Simba Anacheza Na Timu as If ina Wachezaji 11 tuu? Kwanini Hafanyi Rotation ya Wachezaji Pamoja na Utitili wa Mechi tulizo nazo?

2. Ndani ya Mwezi wa 10 Simba Imecheza Mechi 6, Mechi za Karibu zaidi ni za Tarehe 20, 24, 28 na Tarehe 05 katika hizi mechi 4 Kocha ameanza na kikosi kile kile, Na Sub Zile zile bila kujari anacheza na nani? Hapa sio Kwamba Kuna Ulakini wa Mbinu?

3. Mechi ya Leo, Kwa Kocha Mwenye Akili Timamu unawezaje Kumuingiza Aishi Manula Ambaye alikuwa majeruhi kwa Muda wa Zaidi ya Miezi 3 halafu unakuja kumuweka Direct kwenye Derby? Yalikuwa maelekezo ya Viongozi au ni Mahitaji ya Kocha? Nje una Ayoub na Una Salim.

4. Saido Alionekana Kuchemsha hii mechi toka Kipindi cha Kwanza, Kwa Kocha mwenye Uwezo unawezaje Kumuacha huyu mchezaji amalize Dakila 90?

5. Inakuwaje kwa wewe kocha Ambaye ni mtaalamu, Timu inatatizo la Beki za Kati kwa miezi 6 sasa, na Hakuna Improvement, Kwanini Usiwajaribu mabeki wengine ulio nao benchi?

6. Kapombe na Zimbwe kwa macho ya kawaida wanaonekana wamechoka, Angalia Magoli ya Leo yaliko tokea, Lakini Kwanini Kocha Umeendelea kuwa King’ang’anizi?

7. Unacho Mpendea Baleke Kwenye Derby ni Nini? Unaogopa kwasababu Phiri hana Rotation nzuri kwenye Kikosi? Baleke Kama Saido na Chama hawako vizuri Baleke ni Pazia tuuu, Kama Kapombe na Zimbwe Hawapigi Cross Baleke Hana Faida Mbele ya Phiri

8. Kama Kocha Kwanini huwaambii wachezaji waachr kurogana? Kramo Angekuwa Mbali Kiasi Gani?

9. Sijaona Mbinu wala Falsafa Ya Mpira wa Robertihno zaidi ya Juhudi Binafsi za Wachezaji.

10. Viongozi wa Simba Kama Mtaenda na Robertihno Makundi ya CAF CL sitashangaa tukiishia hatua ya Makundi.

TUSHINDE AU TUFUNGWE ROBERTIHNO SIO KOCHA SAHIHI WA SIMBA HASA HII yenye wachezaji wengi Wazuri
Huu uzi umeuanzisha saa 8:37.
Ni sawa, hauko sawa kiakili kwa sasa.
Ukiamka andika na ya viongozi kwanini mnaiba wachezaji AIRPORT, na mna scouting master
 
Back
Top Bottom