Ni kweli smart TV zinatumia Umeme Mwingi?

Ni kama simu ya tochi na SMART Phone. Ipi inakaa na chaji mda mrefu
Hapa umechemka na huu mfano wako tafuta mfano mwingine. Smartphones zinakata moto sana ukiwasha data lakini usipowasha data inakaa na moto the same kama simu ya kitochi. Kwa upande wa tv ni tofauti, kwanza kwa kukuchallenge tu ni kwamba tv haitumii battery.
 
Yeah kiwango cha umeme kinaongezeka, lakini kidogo bado , unaweza usimalize hata unit moja kwa siku..

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Smart tv au hizi flat tv hazitumii zaidi umeme ukifanisha na matoleo ya awali.

Tv za zamani zilikuwa na technology ya halogen, kule nyuma kwenye chogo kulikuwa na bulb [emoji362] kubwa tu tena ukiwasha tv unaiona ukichungulia.

So matumizi ya umeme ya tv zile yalikuwa juu zaidi ukifananisha na hizi sasa ambazo ni flat so technology yake ni latest. Zinatumia led lights kufanya mwanga wa screen plus hazina energy consumption ya juu. Kimsingi consumption yake ipo chini sana.
 
Sawa mjomba Arnold Schwarzenegger.
 
Very true. Haya matv ya mtumba mengi ni ya zamani.
 
Uko sahihi katika hili. Safi dana kwa malezo mazuri.
 
Hapa ndipo tunahitaji utaalam sasa!! Bado kiza kwetu sie wengine
kuna input na output. kwenye mziki kwa mfano wanasema mziki wangu ni watt5000 hii ni output. ukichungulia kule nyuma huwa wanaandika voltage ya umeme 240v na 65w. sasa hiyo 65w ndio input na ndio nguvu ya umeme. kwenye hesabu zako tumia hii 65w, achana na ile output 5000w
 
Nadhani hapa kwenye “Watts” panachanganya

Kuna Watts za speaker na Watts za umeme zinazotumika

Sidhani kama zile watts zinaonekana kwenye subwoofer ndio consumption ya umeme
Maana bili zingekuwa balaa

I stand to be corrected
upo sawa, nimeeleza input na output power hapo juu. zile za kwenye speaker ni output power. Au nguvu ya mdundo,
 
pia na mfumo wa nyaya unaotumia. taa ya waya mrefu itatumia zaidi kuliko taa ya waya mfupi. pamoja na ubora wa taa
 
Flat screen zinakula umeme sana tu asikudanganye mtu.

Chogo ilikuwa ile kubwa i akuwa na watts 60. Ukiwasha masaa 10 flulizo kwa mtindo wa kitanzania tunaoacha mabeki 3 nyumbani wanashinda kwenye TV, masaa 10 ingekula 0.6 units.

Lkn hizo flat screen ni kitu kingine kabisa. Nina hisense ya kisasa kabisa toleo la mwaka 2022.

Inakula 150w per hour
Hii inahtaji masaa 6 tu na dakika 30 kula unit 1 ya umeme.

Nikimuacha house girl nyumbani akaiwasha masaa 12 tu mfululizo anapiga unit 2

Nikija usiku kuangalia taarifa ya habari imeisha hio. Hizi flat zinatumia bulb nyingi sana kumulikia picha. Ulaji wake sio Rafiki

Nna Sony nchi 32, ya kisasa pia inakula watts 60 per hour.

Naambatanisha energy lebel ya TV hii ya hisense ya 55" ipo rated bad karibu na worse

Angalia hapo ipo level 4 wakati worse ni level 5. Kwa ufupi flat screen hasa vioo vikubwa inakula umeme sana.

Ukitaka inayokula vema kisasi hata energy level 3 bei yake ni kali kwakuwa technology yake pia itakuwa sio hii ya LED pengine mini-LEDs ndio energy sever
 
Dah, ila kuna ukweli.
Sijawahi hata kuchunguza kua eti ina kula umeme wakati ni kifaa cha umeme[emoji41] alitaka itumie nini, akachomeke waya kwenye tank la maji[emoji2960] napo lazima alalamike " inakunywa maji kuliko ngamia "

Huwezi tumia, achana nacho, usilazimishe kua na vitu usivyo vimudu ni kama umemkumbatia nyuki
 
E3 ni 4k 120hz pia zimekua designed ku operate outdoor hivyo zina Nits nyingi, tv ya Nchi 55 inakula watts 60 mpaka 80 kawaida.


Na Chogo inakula watts 60 kioo kidogo inch 14 mpaka 21. Ukitumia flat ya led atsame size hata watts 30.
 
Kuna smart tv na android tv mkuu. Inawezekana uliyonunua dukani ni mtumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…