Flat screen zinakula umeme sana tu asikudanganye mtu.
Chogo ilikuwa ile kubwa i akuwa na watts 60. Ukiwasha masaa 10 flulizo kwa mtindo wa kitanzania tunaoacha mabeki 3 nyumbani wanashinda kwenye TV, masaa 10 ingekula 0.6 units.
Lkn hizo flat screen ni kitu kingine kabisa. Nina hisense ya kisasa kabisa toleo la mwaka 2022.
Inakula 150w per hour
Hii inahtaji masaa 6 tu na dakika 30 kula unit 1 ya umeme.
Nikimuacha house girl nyumbani akaiwasha masaa 12 tu mfululizo anapiga unit 2
Nikija usiku kuangalia taarifa ya habari imeisha hio. Hizi flat zinatumia bulb nyingi sana kumulikia picha. Ulaji wake sio Rafiki
Nna Sony nchi 32, ya kisasa pia inakula watts 60 per hour.
Naambatanisha energy lebel ya TV hii ya hisense ya 55" ipo rated bad karibu na worse
View attachment 2689718
Angalia hapo ipo level 4 wakati worse ni level 5. Kwa ufupi flat screen hasa vioo vikubwa inakula umeme sana.
Ukitaka inayokula vema kisasi hata energy level 3 bei yake ni kali kwakuwa technology yake pia itakuwa sio hii ya LED pengine mini-LEDs ndio energy sever