Ni kweli TISS hawafahamiani na hawaaminiani?

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Wanabodi, weekend hiyooo na kamvua kwa mbali hapa Arusha!

Nipo Triple A hapa. Kuna jamaa yangu ananiambia eti wana usalama/TISS hawafahamiani na hawaaminiani kabisa!

Yaani kila mmoja ana majukumu yake na mahala pa kureport. Hawana mazoea ya mwenzangu uko wapi, unafanya nini!

Hawaaminiani, hawajuani kivile!

Hii kitu ni kweli au ni mfumo kama tu wa TAMISEMI au taasisi zingine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamanieee hao usalama ni watu wa kawaida tu (hususani hawa wa hapa kwetu)

Tofauti kubwa iliyopo ni kwamba wanafanya shughuli zao kwa SIRI. Hapo ndio nguvu yao ilipo.

Hata wewe ukiweka maisha yako PRIVATE watu watakuwa wanakuogopa kwa kuwa hawakujui vizuri.

Hata Secret Societies kama Illuminati, Freemasonry, Klu Kla Klux et al zinatumia USIRI kama mbinu mojawapo.

Sababu nyingine: Kwa kuwa CCM inawatumia sana, hivyo imewapa nguvu fulani ( kuwaweka juu ya sheria kwa raia ) kiasi kwamba hata akikuonea huwezi kumfanya chochote.

Suala la kutoaminiana ni kawaida tu kwenye mambo ya ulinzi na usalama, hata walinzi hawaaminiani.

Na kuhusu kutojuana ni kawaida pia, hata mwalimu hajuani na walimu wote nchi nzima unless mmekuwa assigned sehemu moja.

Wanaruhusiwa pia kuwa na vifaa/silaha ambazo wewe raia huruhusiwi kuwa nazo kitu kinachowapa nguvu dhidi ya raia!

Mambo mengine yote ni yale yale.

Kwa kuongeza, nimewahi kuwa lindo moja na Hawa jamaa kwanza walikuwa wanalala tu, maana walikuja na tent na kitanda kikawekwa ndani. Bastola walikuwa wanakabidhiana ( taking and handing over ).
 
Sasa wakijuana na kutengeneza mtandao usalama utakuwepo kweli? Lazima wasijuane! Na kila mtu anareport kwa bosi wake mmoja na anapokea maelekezo kutoka chanzo kimoja!

Kwenye utendaji wanaweza kujuana lakini wachache sana labda 2 au 3 na tena ujui nani anamchunguza nani?

Tena unakuta mwingine kazi yake ni kuchunguza mienendo ya mwenziwe na kureport basi! Hata hivyo kwa ngazi za chini maslahi hakuna na unatakiwa huwe mzalendo na kujitolea kwasaana!

Ngazi za juu familia yako inaweza kutumiwa kukuwajibisha kama utazingua na unakuwa unajua hilo! Kwa ufupi sio kazi nzuri kama watu wanavyodhani! Sikushauri!
 
Kuna wanaojuana, kuna wasiojuana, kuna wanao-wafanyia ujasusi wenzao uku nao wakifanyiwa ujasusi bila kuwajua wanaowafanyia ujasusi, kuna wanaofanyishwa kazi za usalama bila wao kujijua, iwe kwenye siasa, biashara, dini kote wapo majasusi.

Tatizo la ujasusi wa bongo umejikita kwenye kukusanya taarifa zaidi za mambo mbali mbali kusaidia utawala uliopo madarakani tofauti na wenzetu ambao wanajikita sana kwenye kuzuia hatari zote mbaya zizazohusu uchumi na siasa bila kuegemea upande wowote wa kisiasa.

TISS wanatakiwa kujikita kwenye ujasusi wa kiuchumi jinsi ya kutengeneza mabilionea, jinsi ya kupigana vita ya kiuchumi na mataifa jirani, kuhakikisha taarifa za kiujasusi wanazokusanya zinafanyiwa kazi haraka bila kuegemea upande wowote.
 

Ndugu zangu, kwa vipaumbele vya maisha sasa mnapata wapi mda wa kujadili mambo yasiyokuwa na faida kwa kiwango hiki?
 
Wewe kama maisha yako magumu usigeneralize.

Kilicho na faida kwako sio lazima kiwe na faida kwa mwengine.

Watoto wa mjini tunasema usifosi tufanane!
Ndugu zangu, kwa vipaumbele vya maisha sasa mnapata wapi mda wa kujadili mambo yasiyokuwa na faida kwa kiwango hiki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…