Habari zenu wana JF.
Mimi ni Muathirika wa tatizo la Vidonda vya Tumbo Almost Mwaka sasa lakini kutokana na kuutibu huu ugonjwa bila mafanikio nimepata comment mbali mbali ambazo nyingine zimenipa khofu...
Tatizo la vidonda vya tumbo ukikaa nalo mda mrefu unapata complications kuu tatu(ya nne na ya tatu zinafanana kimantiki na kidalili).
1. Hemorrhage/Utaanza kutapika damu au kunya kinyesi cheusi au chenye damu(Vidonda vinakua vinachimba zaidi kuta za tumbo/utumbo na kupasua mishipa ya damu).
2. Perforation(Uchimbaji ukiendelea tundu litatokea na uchafu(Vyakula na enzymes) utaingia kwenye peritonium(Mfuko uliobeba viungo vya tumboni).
3. Gastric Outlet Obstruction/ Chakula kushindwa kutoka nje ya tumbo na utakua unashiba haraka na kutapika mara kwa mara.
4. Gastric cancer(Sana sana kama vidonda vyako vimesababishwa na Helicobacter Pyroli).
Katika hizo complication hakuna ambayo inaweza isikuondolee uhai iwapo hautachukua matibabu mapema, mfano ukitapika damu unaweza kufa kwa sababu zilizo wazi, kuta za tumbo zikitoboka vyakula na enzymes zikaingia kwenye peritoneum, viungo vyote vitaathrikika na usipofanyiwa upasuaji unakufa ndani ya siku chache tu.
Complications mbili za mwisho zina kuua taratibu(utaacha kula sababu chakula hakiondoki tumbo unhisi umeshiba, kutapika mara kwa mara, cancer itakunyonya na inaweza kusambaa na mwisho utakufa) ila mbili za mwanzo unaweza kufa mara moja.
Mimi ni daktari mjasiriamali nimefungua Medical clinic mwezi mmoja wa kwanza nimekutana na wagonjwa 14 wako Positive na
Helicobacter Pyroli ambae ndo cuprit zama hizi na anawapa dalili zote za vidonda vya tumbo wagonjwa hao.
Kati ya hao kumi na nne, wagonjwa watatu ndo wamekubali kuanza dose na Mmoja tu ndo amendelea na dose mpaka stage ya mwisho hao wawili walipopata haueni kidogo katika week ya kwanza wakaacha dawa, na ambao hawakuanza dawa wanasema eti watatibu kwa miti shamba, wengine eti watafata masharti ya chakula wengine wanasema huo ni ugonjwa wao wameuzoea.
Watanzania tuache hii dhana ya kijinga ya kusema mm ni mgonjwa wa vidonda vya tumbo na kuishi na vidonda vya tumbo kama vile ni ugonjwa usiotibika, asilimia zaidi ya 90 ya wagonjwa wenye vidonda vya tumbo husababishwa na Bacteria(Helicobacter Pyroli) na huyu bacteria anaweza kuuliwa kwa dawa na sio masharti ya chakula.
Tuache ujinga wa kufata dhana za mitaani kutanenI na madaktari wanaolewa medicine wawape dynamics mpya za Gonjwa hili, madaktari wengi wa zamani wametuachia dhana mbaya na ugonjwa huu.
Tuachane na dhana za kizamani pia kuwa vidonda vya tumbo husababishwa na kutokula kwa wakati na nyingine nyingi zilizopitwa na wakati.
Vidonda vya tumbo vinatibika hospitalini ni wewe kumeza dawa utakazo pewa, kulingana na vidonda vyako unaweza kuitaji kumeza dawa hata miezi miwili na wengine mpaka kwenda kufanyiwa kipimo cha OGD.
ukiacha dawa bila kumaliza dose utatengeneza usugu wa dawa kwa huyo bacteria na itakua ngumu kukutibu na itabidi ufanye vipimo vya culture and sensitivity na dawa zake lazima zitakua expensive kama za mwanzo zilikushinda