Ni kweli vitabu vya dini havituruhusu tutukane viongozi wetu; je, vinaruhusu viongozi watuibie na wawe mafisadi wa kutupwa?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
"Kama Vitabu vyetu vya Dini Quran na Biblia vinatufundisha kuwa na Maadili, kuheshimiana, kuvumiliana, Kusameheana na Kutotukanana iweje Wewe Mwanadamu uende navyo Kinyume kwasababu tu ya Maslahi yako ya Siasa?" amesema Rais Mmoja wa duniani ambaye kwa sasa GENTAMYCINE nimemsahau Jina ila najua Alifura (Alifoka) hivi Jana akiwa mita chache tu na Nyumba yake, Zinakotuzwa Hela za Walipa Kodi nchini na Wizara husika ya Mawokoto hayo.

Ukitaka Wananchi wa Barani Afrika wasikuseme au wasikuchukie jitahidi sana ufanye 'Walk the Talk' katika Utendaji wako (kwa yale ya Kimaendeleo unayoyahubiri Kwao Kutwa) na siyo 'Talk the Walk' ili Uwapumzishe Kukushambulia kwa Ukpsoaji ambao Wengine tuna (wana) PhD (Doctorate) yake.

Kwa mfano ukisema kuwa hupendi Rushwa na Ufisadi basi Waafrika (Wananchi) waone kuwa hata Wewe Mwenyewe huibi, hujengi Mahekalu na hufichi Fedha zako Ulaya, Asia na Uarabuni.
 
Yesu mwenyewe aliwachana watawala mafisadi akiwaita majina mabaya. Hali kadhalika Yohana mbatizaji alimchana mtawala kwa kumpa makavu. Watawala wanakosea sana tu katika jamii hutokea wa kuwapa maneno makali dhidi ya mienendo mibaya ya utawala wao
 
Vinaruhusu kuwaonya viongozi mafisadi lakini sio kuwatukana...

Matendo ya Mitume 24:22-26

Utasoma vile Mtume Paulo alivyoteswa na Gavana Feliksi ambaye aliona kuwa hana hatia ktk kesi yake ila aliahirisha kesi ya Mtume Paulo ili apewe Rushwa...

Ila Mtume Paulo alisema naye wazi wazi kuhusu uadilifu na kujidhibiti...
 
bible yangu inanambia mamlaka za duniani zinatoka kwa Mungu,NDIO.
maana Mungu ndiye hurusu kila kitu kiwe,lakini sio tiketi ya kutufanyia uharamia.
 
Mamlaka ya Adolf Hitler iliyoua mamilioni ya Waisrael ilitoka kwa mungu yupi?
 
"Kama Vitabu vyetu vya Dini Quran na Biblia vinatufundisha kuwa na Maadili, kuheshimiana, kuvumiliana, Kusameheana na Kutotukanana iweje Wewe Mwanadamu uende navyo Kinyume kwasababu tu ya Maslahi yako ya Siasa?" amesema Rais Mmoja wa duniani ambaye kwa sasa GENTAMYCINE nimemsahau Jina ila najua Alifura (Alifoka) hivi Jana akiwa mita chache tu na Nyumba yake, Zinakotuzwa Hela za Walipa Kodi nchini na Wizara husika ya Mawokoto hayo.

Ukitaka Wananchi wa Barani Afrika wasikuseme au wasikuchukie jitahidi sana ufanye 'Walk the Talk' katika Utendaji wako (kwa yale ya Kimaendeleo unayoyahubiri Kwao Kutwa) na siyo 'Talk the Walk' ili Uwapumzishe Kukushambulia kwa Ukpsoaji ambao Wengine tuna (wana) PhD (Doctorate) yake.

Kwa mfano ukisema kuwa hupendi Rushwa na Ufisadi basi Waafrika (Wananchi) waone kuwa hata Wewe Mwenyewe huibi, hujengi Mahekalu na hufichi Fedha zako Ulaya, Asia na Uarabuni.
Juu ya mafisadi na wezi wa hela za umma hawakamatwi ila anayekosoa anakamatwa, hii kweli inaingia akilini. Only in Africa! Hata ukitukana kwani tusi linamnyofoa kiungo, ila huyu anayeiba billions za huduma kwa wananchi anawakosesha huduma muhimu na wengine kufa hapa nani aadhibiwe?
 
Vinaruhusu kuwaonya viongozi mafisadi lakini sio kuwatukana...

Matendo ya Mitume 24:22-26

Utasoma vile Mtume Paulo alivyoteswa na Gavana Feliksi ambaye aliona kuwa hana hatia ktk kesi yake ila aliahirisha kesi ya Mtume Paulo ili apewe Rushwa...

Ila Mtume Paulo alisema naye wazi wazi kuhusu uadilifu na kujidhibiti...
Ukiwaonya ndipo unaambiwa umemtukana maana hawataki kuonywa

Sent from my TECNO B1c using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom