Ni lazima Simba atinge Robo Fainali katika Kundi D

mpiga vichwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
2,376
Reaction score
3,811
Ukifuatilia msimamo ulivyo katika Kundi D utakubaliana na mimi kuwa Simba SC ndiyo itakayokuwa ya kwanza kutinga hatua ya robo fainali katika kundi lake.

Katika kundi hili Simba na Asec Mimosas ndizo timu zitakazokuwa na michezo miwili nyumbani na mchezo mmoja ugenini katika mzunguko wa pili.

Rs Berkane na US Gendarmaree watakuwa na michezo miwili ugenini na mchezo mmoja nyumbani.

Ni hivi ; kama kila mmoja atashinda mechi zake za nyumbani, Simba mwenye pointi 4 + 6 atakuwa na point 10. Asec Mimosas mwenye point 3 +6 atakuwa na pointi 9.

Rs Berkane mwenye pointi 6 + 3 atakuwa na pointi 9. Us Gendarmaree mwenye pointi 4 + 3 atakuwa na pointi 7.

Hivyo, Simba ana nafasi kubwa ya kutinga robo fainali kama atashinda mechi zake za nyumbani zilizobaki. Na hapo utagundua kwamba, sare aliyoipata dhidi ya Gendarmaree ugenini ilikuwa na maana kubwa zaidi.

Tahadhari, unaweza kupigwa hata ukiwa nyumbani.

 
Mkuu , lakini nimetoa tahadhari kwamba waweza kupigwa hata ukiwa kwako. Au una hasira ya kukurupushwa chooni na wanao
Haaa haa haaa, umeniombea kheri angalau nipate hata hao watoto wa kunisumbua. Angalau kolo wewe una akili kidogo kuliko kolo Scars yeye ni sifuri kabisa.
 
Naamini simba hawezi kurudia makosa waliyoyafanya kwa galaxy
Suala la robo fainali hilo halina ubishi wala mjadala mpana bali kwasasa tumejikita kucheza fainali yenyewe na hilo linaweza kutimia iwapo tu Simba watarekebisha makosa ya over confidence ambayo yalitugharimu kwa Galaxy.
 
Mpira haupo hivyo,Simba wanatakiwa kukaza na kutobweteka kwani ndiko kulipowaponza wakatolewa na wabotwsana. Hawatakiwi kumdharau mpinzani wowote anayekutana nae
 
Suala la kushinda match zote za nyumbani kwa simba ni kawaida na tutafanya hivyo.. asiyetaka shauri yake
 
Haaa haa haaa, umeniombea kheri angalau nipate hata hao watoto wa kunisumbua. Angalau kolo wewe una akili kidogo kuliko kolo Scars yeye ni sifuri kabisa.
Dah! Soka limetekwa na watu wasiojulikana. Sijui tukimbilie wapi masikini!
 
Mpira haupo hivyo,Simba wanatakiwa kukaza na kutobweteka kwani ndiko kulipowaponza wakatolewa na wabotwsana. Hawatakiwi kumdharau mpinzani wowote anayekutana nae
Kwani kuna sehemu mtoa mada amesema Simba anatakiwa kuwadharau wapinzani wake ?
 
kwa mwaka huu Simba hana uwezo wa kuingia robo fainali.
Namtabiria kuwa wa mwisho kwa hili kundi lake.
Huu mwandiko kama wa mzee mpili. Hizo tunguli zako zimechoka mzee. zinakupa majibu yasiyo sahihi. Bora tu ukazipiga moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…