Braza......u are missing something here! hujaelewa Philosophy nzima ya ''KUGAWANYIKA'' aliyoisema MM hapo juu mkuu!
Hivi, wamarekani walivyoamua kugawanyika na kuwa na camp mbili - Obama vs John M......kulimwagika damu? Umesema upo nje, umeona huko Ukraine kilichotokea juzi, wale jamaa wamemwaga damu kumpata Yonkovich? (sorry spelling)?
Mwanakijiji, ingekuwa vema kama ungeelezea kidogo 'kugawanyika' ulikokukusudia na kwa nini hutoi suggestion bali unarule kwamba ni lazima tugawanyike.
Ama baada ya hapo, ueleze jinsi tutagavyogawanyika. Sio sahihi kusema tugawanyike bila kutoa muongozo wa huko kugawanyika, at least hata kwenye hitimisho.
Kwa independent thinker, inakuwa vigumu kuunga mkono au kuyakataa mawazo yako ya kulazimisha watu wagawanyike.
Kuna tofauti kati ya kugawanyika na kutofautiana. Tunatofautiana. Hatujagawanyika. Wala hatutagawanyika kamwe. Umoja na mshikamano ni urithi wa Chama kilichotukomboa.Tuuenzi na kuulinda umoja na utulivu. Kwa pamoja, Mwanakijiji, Mwanajiji, Mkulima, Mfanyakazi, Mfanyabiashara na Mwekezaji, tujenge Taifa letu changa.
Umoja ni Nguvu!
Exactly!
Kutofautiana kwa mapato, mawazo, elimu, dini si kugawanyika hiyo ndio hazina ya maendeleo katika jamii..kwani sisi si kondoo!
Kugawanyika ni upotofu wa fikra na dalili za kukata tamaa kihoja
Si tabia njema ku-advocate kugawanyika badala yake tunatakiwa ku-advocate kutofautiana katika mambo na kuwa pamoja katika kuheshima mawazo ya wengi na wachache ata the time!
kuna kila dalli kuwa hapa jamvini kuna watu wana kazi ya kumpigia makofi mwanakijiji hata kama hawajaelewa ametoa mawazo gani!!!!!!!!!!!
jamani jaribuni kuthink critically, kama ni kutofautiana kimtazamo, matakwa, itikadi nk. mbona tayari tunatofautiana? tutofautiane mara mbili? au mara ngapi???
ishu ni "kugawanyika" nipeni mfano wa nchi kama yetu hususani ya kiafrika "iliyogawanyika" halafu hapakutokea mapigano/umwagaji damu na badala yake waka[pata maendeleo..............
nakubaliana na hoja za tumaini na companero..............
kwamba mbuzi na chui wakubaliane kutofautiana kuwa nani kati yao amle mwenzake; halafu wanatakiwa kuheshimu "tofauti hiyo".!
Samahani sana, kuhubiri uhasama wakati uko mbali na un owaambia wahasimiane ni sawa na na sungura kumdanganya nyani kuwa wote wakaue wazazi wao kisha sungura kwenda kuleta damu kutoka kwenye magome ya miti wakati mwenzanke nyani ameshamuua mama yake.MM ni mtaalamu wa lugjha na wengine wote hapa tunapaparuka tu. ukweli utabaki kwa historia humu kwamba VITA INAPIGANWA PALIPONA NA MGOGORO NA SI PENGINE. majirani walio mbali watakwambia tu mbinu na wakati mwingine watakukosoa.
Lugha za MM hapa jamvini zina utata. YAANI NI TUNGO TATA zenyee maana zaidi ya moja na yeye hajawahi kuwa mfafanuzi wanaofanya ufafanuzi ni wana JF. kwa imani huu ni mtego au ni ujanja wa kujua wengine wan fikiri nini. WIZI WA BUSARA NA HEKIMA.
MM anaushawishi mkubwa sana hapa jamvini lakini hajatupeleka hatua ya kupata elimu ya kweli. Tangu vyama vingi vikubaliwe sijawahi kuipigia CCM kura. Jee huku siyo kugawanyika? wewe hatujui kama unapiga kura! Kama mgawanyiko unouongelea ni wa amani kama ulivyojibu basi ungetshawishi tuliokopiga kura upinzani tuendelee.
Mimi ni mwana CCM lakini sikuwahi kuwaamini tangu enzi za Mwinyi..
Nafikiri inatosha , si vizuri kuweka busara yote hapa.
Web,
Kama chui ni fisadi (kumbe hana makucha anakula majani kama tumain) then wako sawa kimaumbile tunaweza kuendelea na hoja
Tutafoutiana na huyo fisadi na tutamnyaganya anachokula ambacho si chake sisi kina tumain bila kugawanyika
Usitake kudanganya watu eti kutofautiana kwa elimu na mapato ni hazina ya maendeleo shule gani ulisoma hayo na mwalimu gani alikufundisha kuwa tofauti ya mapato ni maendeleo this is nonsense thinking kwa nchi changa kama yetu
Hili ni jibu tosha kabisa kwa Akili kichwani Tumain na Campanero wanajua chui ni nani na mbuzi ni nani halafu eti tushikamane mshikamano wa kinafiki hatuutaki never on earth wazanzibari wameshituka bado sisi huku na si mbali
Acha emotions wewe, tunaongelea kutofautiana siyo kushikamana kinafiki hiyo inaonyesha hujui tofauti ya kutofautiana na kushikamana? kasome dictionary
Hypothesis ya chui na mbuzi ni null and void, hakuna chui wala mbuzi kuna either mbuzi tu au chui tu (binadamu kimaumbile) tukianzia hapo tutajadili mada kwa hoja zilizo sawa..lakini ikishaweka statement mfu (kama hii ya mwanakijiji) utatoa hoja mfu na supporters kama wewe wenye mawazo mfu vilevile
Tunaongelea taifa la watu ambao watatofautiana bila kugawanyika si mataifa mawili ya chui na mbuzi hapo hakuna mfano ili ni kuhalalisha vurugu na upuuzi
Hakuna taifa wala halitatokea taifa lemye watu walio sawa kielimu kwasababu watu wengine hawatapenda kusoma hataki kwa kupigwa hii ndio maana tuko tofauti wako watu lazima wawafanyie wengine kazi lakini wote ni binadamu kila moja anamheshimu mwingine kwa nafasi yake..hizo ni facts hakuna anayekudanganya ndugu..
Tofauti ya mapato ni facts ambayo hakuna binadamu anaweza kurekebisha kwasababu kupata ni matokeo ya juhudi binafsi, elimu na majaaliwa ya mwenye kugawa riziki..usiniulize mwalimu aliyenifundisha mimi mwenyewe mwalimu nasoma naona hali halisi pia (experience)
Kutofautiana kwa mapato, elimu, dini, rangi , mila etc ndio maendeleo yenyewe nimeseama hapo juu sisi si kondoo "kutofautiana na kuheshimiana bila kugawanya ndio msingi wa maendeleo ..rudi shuleni ndugu..kichwa ngumu
Acha emotions wewe, tunaongelea kutofautiana siyo kushikamana kinafiki hiyo inaonyesha hujui tofauti ya kutofautiana na kushikamana? kasome dictionary
Hypothesis ya chui na mbuzi ni null and void, hakuna chui wala mbuzi kuna either mbuzi tu au chui tu (binadamu kimaumbile) tukianzia hapo tutajadili mada kwa hoja zilizo sawa..lakini ikishaweka statement mfu (kama hii ya mwanakijiji) utatoa hoja mfu na supporters kama wewe wenye mawazo mfu vilevile
Tunaongelea taifa la watu ambao watatofautiana bila kugawanyika si mataifa mawili ya chui na mbuzi hapo hakuna mfano ili ni kuhalalisha vurugu na upuuzi
Mbuzi tu ama chui tu binadamu kimaumbile maana yake nini?Nani anazungumzia maumbile hapa?
Je wanaharakati wa ukombozi wa Afrika ya Kusini walikuwa wamoja na utawala wa makaburu - hapana; je wanamapinduzi walioongoza uasi dhidi ya utawala wa Mfalme George wa Uingereza kule Marekani walijaribu kuwa wamoja na ndugu zao ng'ambo ya atlantic? la hasha!
Kugawanyika tunakokupendekeza siyo kugowanyika kunakotokana na chuki binafsi, wivu, husuda au vitu ambavyo kimsingi havina uzito wa hoja. Kugawanyika tunakopendekeza kunatokana na kile wengi wameshakisema hapa yaani "tofauti". Wapo wale wanaotaka tuamini kwamba tofauti zetu zinatuunganisha badala ya kwamba zinatugawanisha.
Unapokuwa na kundi la watu ambao wameweka chama chao mbele kuliko taifa, mgawanyiko ni lazima!
Unapokuwa na kikundi cha watu ambao wanaamini wawekezaji wa kigeni ndio wataleta maendeleo ya taifa letu; mgawanyiko ni lazima!
Unapokuwa na watu wanaoamini kuwa katika taifa zima hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kuongoza isipokuwa mmoja basi mgawanyiko ni lazima!
Unapokuwa na mfumo wenye kuzalisha utawala wa kifisadi ambapo kundi la watu wachache wamekuwa ni walaji wakuu wa ile keki ya taifa na wengine wakibakia kutamania toka mbali, basi mgawanyiko ni lazima!
Mgawanyiko ninauzungumzia ni kutenganga kiitikadi, kimkakati, kimtazamo, na kimwelekeo wa utatuaji wa matatizo yanayokabili taifa letu. Ni mgawanyiko ambao lengo lake ni kuhakikisha kuwa wanaotawala sasa hawapati nafasi hiyo tena na badala yake kutafuta watawala wengine ambao watakubalina na yale tunayoyapendekeza kama tiba ya matatizo yetu kama taifa. Ni mgawanyiko ambao hauna uwezekano wa upatano, umoja, urafiki, au kwa namna yoyote ile.
Kukubaliana na hilo yaweza kuwa ni group thinking, kutamani jambo hilo hilo laweza kuwa ni group thinking.. but well.. ninapokubaliana na ukweli ambao wengi nao wameukubali siwezi kuomba radhi kwamba tunakubaliana na ukweli huo.
Lakini uzuri wa demokrasia ni kuwa wale wanaopinga na wenyewe wanaweza na wanapaswa kusema kwanini tuungane na kwa nini tusigawanyike mbele ya uovu!.