Je wanaharakati wa ukombozi wa Afrika ya Kusini walikuwa wamoja na utawala wa makaburu - hapana; je wanamapinduzi walioongoza uasi dhidi ya utawala wa Mfalme George wa Uingereza kule Marekani walijaribu kuwa wamoja na ndugu zao ng'ambo ya atlantic? la hasha!
Kugawanyika tunakokupendekeza siyo kugowanyika kunakotokana na chuki binafsi, wivu, husuda au vitu ambavyo kimsingi havina uzito wa hoja. Kugawanyika tunakopendekeza kunatokana na kile wengi wameshakisema hapa yaani "tofauti". Wapo wale wanaotaka tuamini kwamba tofauti zetu zinatuunganisha badala ya kwamba zinatugawanisha.
Unapokuwa na kundi la watu ambao wameweka chama chao mbele kuliko taifa, mgawanyiko ni lazima!
Unapokuwa na kikundi cha watu ambao wanaamini wawekezaji wa kigeni ndio wataleta maendeleo ya taifa letu; mgawanyiko ni lazima!
Unapokuwa na watu wanaoamini kuwa katika taifa zima hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kuongoza isipokuwa mmoja basi mgawanyiko ni lazima!
Unapokuwa na mfumo wenye kuzalisha utawala wa kifisadi ambapo kundi la watu wachache wamekuwa ni walaji wakuu wa ile keki ya taifa na wengine wakibakia kutamania toka mbali, basi mgawanyiko ni lazima!
Mgawanyiko ninauzungumzia ni kutenganga kiitikadi, kimkakati, kimtazamo, na kimwelekeo wa utatuaji wa matatizo yanayokabili taifa letu. Ni mgawanyiko ambao lengo lake ni kuhakikisha kuwa wanaotawala sasa hawapati nafasi hiyo tena na badala yake kutafuta watawala wengine ambao watakubalina na yale tunayoyapendekeza kama tiba ya matatizo yetu kama taifa. Ni mgawanyiko ambao hauna uwezekano wa upatano, umoja, urafiki, au kwa namna yoyote ile.
Kukubaliana na hilo yaweza kuwa ni group thinking, kutamani jambo hilo hilo laweza kuwa ni group thinking.. but well.. ninapokubaliana na ukweli ambao wengi nao wameukubali siwezi kuomba radhi kwamba tunakubaliana na ukweli huo.
Lakini uzuri wa demokrasia ni kuwa wale wanaopinga na wenyewe wanaweza na wanapaswa kusema kwanini tuungane na kwa nini tusigawanyike mbele ya uovu!.