Si lazima tuganyike ili kufikia malengo,tunaweza kutofautiana kimawazo,tena kwa muda tu,lakini inapofika kwenye maslahi ya taifa ni lazima tuache tofauti zetu,nani kawaambia Warekani huwa wanagawanyika,ninachojua hutofautiana kwa hoja tu lakini inapofika kwenye swala lenye maslahi ya wamerekani hakuna cha democrats au republican they all join hands,mfano mzuri ni vita ya Iraq aliyoianzisha Bush,alipowaambia Wamerekani sababu ya vita ni kupigania maslahi ya marekani wengi waliamua kumuunga mkono hata kama mioyo yao ilikuwa dhaifu,..kwa hiyo tupingane kwa hoja lakini tusigawanyike hasa linapokuja kwenye swala la uchagua amani au vita,ufisadi au uadilifu,..ni lazima sote tuungane kutetea amani na uadilifu na tusigawanyike kwa hili,eti liwepo kundi la watetea ufisadi halafu pia liwepo kundi la wapinga ufisadi...