Ni lazima Wakuu wa Mikoa wakusanyane Dodoma kwenye bajeti ya TAMISEMI?

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Hii nchi ina matumizi ya anasa sana, kwamba ni lazima hawa jamaa wasafiri kote huko kutoka Kona za Tanzania kwenda Dodoma kushuhudia bajeti ya Tamisemi ikisomwa?

Sina kumbukumbu kama hu utaratibu ni wa wakato wote au umeanza awamu ya kula kwa urefu wa kamba,

Kwamba hawawezi fuatilia mkutano kwenye Tv zao ni mpaka wawepo pale Dodoma.

Hizi taratibu za kijamaa na za kishamba huwezi zikuta popote pale Duniani.
 
haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

Wangebaki kwenye vituo vyao na kufuatilia kupitia tv au hata njia nyingine za kiteknolojia wange epuka gharama za mafuta, malazi, posho n.k.

Inaonekana baadhi ya viongozi wetu hawaumizwi na umasikini wa wananchi

Tunalia Hali ya kiuchumi mbaya lkn wakati huohuo tunafanya matumizi ya ovyo kama haya!!!!
 
Pole sana maana ujui unalofikiri kuwa sio sahihi , kaka Kuongoza Nchi ni tofaut kubwa na kuongoza kaya , kwahiyo ili wewe upate haki yako na mwenzako apate aki yake ni lazma wanao waongoza wakutane pamoja kujua wapi kuna mistake
 
Hao wanaolalamika wangekuwa kwenye nafasi hiyo,wangekaataa [emoji1]
Ndiyo kwanza wangekuwa wale wale

Ova
Yaani hapo 250,000 anaenda kaa Dodoma hadi Bunge liishe akisikikiza hotuba akitoka huko ana 21milkwa siku 90
 
Lissu alisema hivi vyeo ni vya kikoloni CHADEMA tukishika hatamu tunavifutilia mbali.
Nakushauri umuamini Mungu wako tu aliekuumba lkn sio binadam mwenzako. Leo anakwambia hivi na kesho anakwambia vile.

Kipimo cha uadilifu wa mtu ni njaa yake. Akiweza kusimamia anachoamini kwenye njaa huyo ndo shujaa wa kweli jambo ambalo wachumia tumbo wetu wa siasa hawaliwezi.

Wote wakifika kwenye kibuyu cha asali huwasahau walio nyuma yao.
 

Attachments

  • images.jpeg
    11.5 KB · Views: 3
  • images (1).jpeg
    6.5 KB · Views: 4
  • images (2).jpeg
    12.4 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…