Druggist
JF-Expert Member
- Nov 10, 2010
- 439
- 528
Habari wadau wa JF.
Natoa wito huu kwa Kamishna Msaidizi wa Ardhi Tabora, maofisa wengine wa kitaalam, na viongozi wa kisiasa, akiwemo Waziri mwenye dhamana ya Ardhi, Mkuu wa Mkoa, na Mkuu wa Wilaya.
Mwaka 2009, kulifanyika zoezi la upimaji wa ardhi katika eneo la Kitongoji cha Sagara, pembezoni mwa barabara inayotoka roundabout ya Singida kuelekea Uchama.
Viwanja vingi vilipimwa na kuuzwa kwa wananchi kwa kufuata taratibu zilizopo.
Kwa wamiliki wa ardhi wa kimila, walitakiwa kulipwa fidia au kupewa viwanja sita kati ya kumi, huku viwanja vinne vikichukuliwa na serikali kwa ajili ya kuuza.
Hata hivyo, eneo lenye ukubwa wa takriban ekari 50, lililopo karibu na stendi, limekumbwa na changamoto kubwa. Eneo hili lilipimwa, hati zikatolewa zikiwa na majina ya wamiliki (wengi wakiwa maofisa wa ardhi na halmashauri ya Wilaya ya Nzega), lakini wananchi hawakulipwa fidia.
Kutokana na hali hii, wale waliopatiwa hati hawakuweza kuendeleza maeneo hayo kwa sababu ya upinzani kutoka kwa wananchi, ambao wakijaribu kupita maeneo hayo hukutana na upinzani wa kutumia silaha za jadi.
Wananchi wameendelea kulima mpunga kwenye eneo hilo kwa miaka mingi, huku mgogoro huu ukiendelea. Mwaka 2015, serikali iligawa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kuwa halmashauri mbili: Halmashauri ya Wilaya na Halmashauri ya Mji. Mgogoro huu ulibaki kuwa urithi wa Halmashauri ya Mji.
Eneo hili, ambalo lingekuwa na thamani kubwa kutokana na ukaribu wake na stendi, limebaki katika hali ya sintofahamu. Kutokuendelezwa kwake kumeleta changamoto zifuatazo:
Amkeni! Ni wakati wa kuchukua hatua!

- Usalama: Eneo limekuwa hatarishi, hususan nyakati za usiku, kwa sababu ya matumizi ya wavuta bangi na watumiaji wa mihadarati.
- Thamani ya Ardhi: Kutokuendelezwa kwa eneo hilo kumeathiri thamani ya maeneo jirani ambayo tayari yameendelezwa.
- Lini mtaandaa kliniki za ardhi ili kutatua mgogoro huu?
- Lini haki itatendeka kwa wananchi waliostahili fidia?
- Kwa kuwa masharti ya hati yanahitaji eneo kuendelezwa ndani ya miaka mitatu, kwa nini hati za umiliki kwa waliokosa kutimiza masharti hayo zisisitishwe?
Amkeni! Ni wakati wa kuchukua hatua!