A
Anonymous
Guest
Naomba kuwasilisha kero hii
Ni takribani mwaka mmoja sasa tangu kuahidiwa kwa muundo mpya wa kada za afya, hususan kada ya uuguzi, lakini utekelezaji wake bado haujaanza.
Tunaomba mamlaka husika kuliangalia suala hili na kutupatia majibu kuhusu ni lini muundo mpya utaanza kutumika, kwa kuwa muundo unaotumika sasa ni wa mwaka 2009, wakati tunahitaji utekelezaji wa muundo mpya uliopitishwa mwaka 2023.
Muundo mpya unapendekeza Afisa Muuguzi Daraja la Pili kuanza kulipwa kwa daraja D1 kutokana na mafunzo ya miaka minne chuoni, badala ya daraja C1 linalotumika sasa. Pia unatambua nafasi ya Muuguzi Bingwa, tofauti na ilivyo kwenye muundo wa sasa.
Katika Mkutano Mkuu wa Wauguzi (Annual General Meeting) uliofanyika Iringa tarehe 10/04/2025, aliyekuwa Naibu Waziri wa OR-Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu, alisema muundo mpya wa kada ya uuguzi ulikuwa umepitishwa na ungeanza kutumika katika mwaka wa fedha 2025/2026. Hata hivyo, hakukuwa na utekelezaji wowote.
Cha kushangaza, katika Mkutano Mkuu wa Wauguzi uliofanyika Arusha mwezi Aprili mwaka huu, tuliambiwa kuwa suala hilo bado linafanyiwa kazi.
Mamlaka husika, hususan OR-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na Wizara ya Afya, tunaomba ufafanuzi. Mnasubiri nini katika utekelezaji wa suala hili, au ni nini kinachokwamisha utekelezaji wake?
Kwa nini ahadi ya kuanza kutumika kwa muundo mpya katika mwaka wa fedha 2025/2026 haikutekelezwa hadi sasa, wakati tayari tumeingia mwaka mwingine wa fedha 2026/2027?
Tunashindwa kuelewa kama kweli muundo mpya ulipitishwa au ilikuwa ni ahadi isiyotekelezeka. Maisha yamebadilika, lakini bado tunatumia muundo wa zamani ambao hauendani na mazingira ya sasa na una maslahi hafifu kwa watumishi.
Tunaendelea kufanya kazi kwa kujituma, licha ya changamoto ikiwemo kutolipwa malipo ya ziada (extra duties) na call allowance, hasa kwa watumishi waliopo chini ya OR-TAMISEMI.
Utekelezaji wa muundo mpya wa utumishi utasaidia kuongeza motisha kwa wauguzi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tunaomba usikie kilio chetu sisi wauguzi na kuhakikisha muundo mpya unaanza kutumika.