A
Anonymous
Guest
Wakuu, habari za muda huu.
Ni lini Jeshi la Polisi na mamlaka nyingine zinazohusika zitachukua hatua kuhusu hali ya malori yanayosafirisha mizigo kutoka bandarini kwenda bandari kavu, maarufu kama “Trip Town”?
Malori mengi katika eneo hili yanaonekana kuwa katika hali isiyoridhisha kiusalama. Baadhi yana matairi yaliyoisha kabisa, huku mengine yakiwa na changamoto katika mifumo ya umeme na vifaa vya usalama kwenye matela.
Kuna pia matela ambayo hayana lock za kutosha za kufungia na kuimarisha kontena. Kwa mfano, kwenye picha niliyoweka, tela hilo linaonekana kuwa na usajili mpya, lakini upande wa kushoto halina lock ya kufungia kontena.
Hali hii inaweza kuhatarisha usalama wa madereva, watumiaji wengine wa barabara na mali zinazobebwa.
Swali ni: Je, mamlaka zinasubiri tukio gani litokee ndipo zichukue hatua?
Ni muhimu ukaguzi na hatua za kisheria zichukuliwe mapema kabla ya kutokea ajali kubwa au kupoteza maisha.
Tuchukue hatua kabla ya janga, si kusubiri janga litokee ndipo tuanze kutafuta chanzo na kuwajibishana.