JET SALLI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 2,392
- 1,578
Ninaamini viongozi wengi mnapita humu Jamii Forums, naamini hata mbunge wa eneo hili la Mbozi anasoma humu. Nimepita barabara hii wiki iliyopita na kufanya utafiti na nikagundua kwamba barabara hii iko busy muda wote, ila haijatendewa haki, na sijasikia mbunge wa eneo hili akiizungumzia. Barabara hii inasafirisha mazao mengi ya biashara kama vile kahawa, mahindi, karanga, na mpunga.
Nimeona mazao haya yakisafirishwa kwenye barabara hii, lakini vumbi lililopo kwenye barabara hii ni tatizo kubwa. Barabara hii ina mchango mkubwa katika uchumi, na sielewi kwa nini mbunge anakaa bungeni na kushangilia mambo ya kijinga tu, huku akisahau barabara hii ambayo ni muhimu sana. Mbunge anapaswa kuizungumzia na kupiga kelele ili serikali yake ya CCM imsikie.
Nimeuliza watu wanasema mbunge hafiki kabisa maeneo hayo, sasa unajiuliza, je, hawa wabunge tulionao wanajua wajibu wao? Watu wa serikali ya CCM, tembeleeni barabara hii mjionee jinsi ilivyo busy na jinsi mazao yanavyosafirishwa, mtajifunza kitu.