Ni lini tutaacha Kumsimanga Hayati Magufuli na kumuonesha kuwa hakuwa Rais mpenda Watanzania?

Ukiona wanajitahidu kumchafua sana maana yake alikuwa amewazidi sana. Hakika Mwendazake (JPM) hakuwa malaika ila katika ubinadamu wake alijitahidi kuishi nje ya maigizo. Alipochukia tuliona na alipofurahi tuliona.
................................................
Kama walishindwa kupambana kimwili, kiroho ni hatari zaidi. Kwa sasa ni tunaosema na mwendazake tupo katika mawanda tofauti "different dimensions or realms".
 
Mpaka utakapomleta ajibu shutuma.
 
Kwakweli nchi hii , imepitia na itapitia kila aina ya kiongozi, lkn kwangu mm mpaka sasa Marehemu BENJAMIN WILIAM MKAPA na Marehemu JOHN JOSEPH POMBE MAGHUFULI kwenye upande wa WAFANYAKAZI !! Mwenyezi Mungu Mwenye Enzi AWAREHEMU .

RAHA YA MILELE UWAPE EEEH BWANA WAPUMZIKE KWA AMANI. MWANGA WA MILELE UWAANGAZIE.

Marehemu BENJAMIN WILLIAM MKAPA alipoingia madarakani, kwanza aliongeza muda wa kustaafu utumishi kutoka miaka 55 mpaka 60.

Pia ndiye aliyeinua Viinua mgongo vya utumishi kwa kuanzisha mifuko ya hifadhi ya jamii na kuwajumuisha watumishi wa serikali. Hapo ikasaidia walau wale watumishi wa serikali waliokuwa wakiambulia pension ndogo kutokana na mishahara yao serikalini kuwa kidogo kujikuta wanapata fedha za kutosha hii kwako MAREHEMU MKAPA ulitoa SADAKA SAFI. pumzika kwa amani.

TAABU ikaanza kipindi cha MAREHEMU JOHN JOSEPH POMBE MAGHUFULI ikazungumzwa habari ya KIKOKOTOO kidogo kifanye kazi lkn akasikia kilio cha wafanyakazi AKAZUIA Neema kwa wafanyakazi ikaendelea Marehemu pumzika kwa amani kwa SADAKA YAKO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…