Ni maamuzi gani unayajutia yaliyokupotezea muda

Ni maamuzi gani unayajutia yaliyokupotezea muda

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Nilipokuwa na miaka 21 Najutia kulazimisha penzi na mwanamke ambae hakunipenda, nilipoteza almost mwaka mzima kulazimisha kisichowezekana, nilijifunza kwa uchungu zaidi mapenzi hayalazimishwi nilipoona ana mimba na kaenda kutolewa posa.

Nakumbuka niliwahi kupoteza mwaka mzima kujaribu kuzitafuta pesa za mtandaoni, nilishasoma mambo ya blogs, affiliate, n.k. lakini niliambulia laki 3 tu muda wote huo, yani hata bando nililotumia lilizidi. nakuja kustuka mwishoni kwamba kuna michezo michafu inahusika ili kupiga pesa kuna wizi wa account za fb ili kushea picha za uchi ili blog itembelewe, hivyo ukikutana na account ya mama yako inashea picha za uchi ujue kuna uwezekano tayari ishabebwa.
 
Kwenda kwenye chuo cha ualimu kwa miaka 3,then mwaka 1 jkt, miezi 6 ya ufundishaji, muda huu nikiukumbuka nasikitika sana, eti waiter anatengeneza mshahara wangu within 5 day's!!
 
Back
Top Bottom