Ni maboresho gani yaliyofanyika daftari la mpiga kura

Ni maboresho gani yaliyofanyika daftari la mpiga kura

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Wakuu !

Habari zenu, siku ya leo hapa kwenye kata yetu nimeona majina ya wapiga kura Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani yamebandikwa.

Chakushangaza hata majina na sura za Marehemu waliokwisha fariki kabla ya uboreshaji wa taarifa za mpiga kura yapo kwenye orodha ya wapiga kura.

Kuna wazee ambao waliokwisha kufa nimeona Sura zao na majina yao kwenye vitambulisho vya mpiga kura yapo yamebandikwa.

Hawa wazee nilikuwa nawafahamu na walifariki kitambo sana kabla hata uboreshaji wa daftari la mpiga kura haujafanyika hapa Jijini Dar.

Hii imekaaje wakuu mbona janja janja nyingi sana?

Kimsingi Tundu Lissu kwenye mikutano (No Reforms No Election) yake alikuwa analizingumzia kwa ufafanuzi mzuri tu.

Ina maana Tume hawakulizangatia na kulifanyia kazi? Najiuliza haya maboresho mbona no danga toto.

Kweli bado hatujaamua kuwa siriazi kwa mustakabali mwema wa Maendeleo ya Taifa letu.
 
Ni wapiga kura wenyewe ndio wanatakiwa kupeleka ombi la kufutwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura hao watu unaosema wamekufa na umekuta taarifa zao zimebandikwa, waandishi na BVr operator hawana mamlaka ya kufuta taarifa zao bila ndugu au watu wa karibu wanaoweza kusaidia Hilo..sema Elimu Kwa wapiga kura ni ndogo sana
 
Back
Top Bottom