Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,649
- 4,786
- Thread starter
-
- #21
Enzi zetu Ilikuwa tunatamka Mafuta Taa kama neno moja. Ila ukilisikilza hilo neno toka kwa mtu mwingine utasikia akitamka MAFUTA YA TAA. Nahisi ndio chanzo cha hiyo YA.
Sijayaita makosa na kwa hakika sio makosa isipokuwa wewe ndiye unayetaka tuamini kuwa ni makosa. Makosa kwa nani ikiwa wenye lugha ndivyo wanavyokubaliana na kuelewana? Halafu neno au maneno yanaweza kuwa na maana zaidi ya moja. Kwa hiyo neno (kiunganishi) "ya" linaweza kuwa na maana "kwa ajili ya..." au "yaliyotokana na..." nk.Hayo mnaita makosa yaliyozoeleka...poleni
Mbona unakwepa kujibu maswali?huko kukua kwako kwa kiswahili ndio mnaondoa maantiki na kuruhusu makosa yazoeleke.
Kweli uongo ukijirudiarudia huwa ukweli
umenichekesha kweli. Ukisema mayai ya kuchemsha je? Au sweta la baridi?
yaani kama hivi:
Mafuta ya taa [mafuta taa?]
mafuta ya kupikia [mafuta kupikia?]
mafuta ya kula [mafuta kula?]
mafuta ya kujipaka [mafuta kujipaka?]
mafuta ya ndege [mafuta ndege?]
bado sijashawishika!. Lugha, hasa majina, sio lazima iwe na mantiki! Lugha ni mazoea (ya muda mrefu?) tu baina ya wanajamii katika kuwasiliana.
Hata jina la mafuta ambayo tumezoea kwa kiingereza kuyaita 'diesel' (dizeli kwa kiswahili), kimsingi linatoka na matumizi kama ilivyo 'mafuta ya taa'. Kilichoanza ni diesel engine (diesel likiwa jina la mvumbuzi wa aina hiyo ya injini ya gari)....hivyo mafuta ambayo yanatumika kwenye aina ya injini ya gari iliyovumbuliwa na diesel, wakaanza kuyaita diesel! ('dizeli' ukipenda 'mafuta ya dizeli'). Hata hivyo aina zote hizo za mafuta bado zina majina yake ya kitaalamu.
Unaweza sema Nimekuta hayupo..Haya ni makosa yaliyozoeleka kwa mfano wa2 wengi husema nimemkuta hayupo kama alikuwa anamtafuta m2 so imezoeleka hivyo na anaeleweka.
TUNAUZA MAFUTA YA TAA ndio ipo sahihi mtoa mada alifail shule...
hapo kiunganishi ni ya Sasa yeye haweki kiunganishi hata mtoto mdogo ukiwa unamfundisha lugha hatokuelewa.
Mkuu nadhani ndio umeamka haya mambo yalishapitiwa zamani hizi yakajadiliwa hadi yakawekwa sawa mwishowe ikaonekana kuandika TUNAUZA MAFUTA YA TAA ndio ipo sahihi..
hapo ulipolalia wenzio waliamkia.
Wacha kupotosha Lugha kama huelewi omba msaada ueleweshwe.
Mi nakumbuka wakati tuko wadogo tukitumwa na bi mkubwa dukani tunatamka ''MAFTATAA" maybe kama kuna innovation iliofanyika apo katikati ila so far nakubaliana kabisa na wanaosema mafuta taa.......
Haswaa ndivyo ilivyokuwa......Tatizo vijana wa .com wamelinyambulisha siku hizi. Na kwa vile hawakuwepo enzi hizo sidhani kama hapa wanaweza kutuelewa!Mi nakumbuka wakati tuko wadogo tukitumwa na bi mkubwa dukani tunatamka ''MAFTATAA" maybe kama kuna innovation iliofanyika apo katikati ila so far nakubaliana kabisa na wanaosema mafuta taa.......
Unaweza sema Nimekuta hayupo..
Waingeleza Husema I Found Nothing....
Ahsante ka kuongeza sosi, tazama posti namba 36By, INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM,
kerosene n kerosini, mafuta ya taa.