yaani kama hivi:
Mafuta ya taa [mafuta taa?]
mafuta ya kupikia [mafuta kupikia?]
mafuta ya kula [mafuta kula?]
mafuta ya kujipaka [mafuta kujipaka?]
mafuta ya ndege [mafuta ndege?]
bado sijashawishika!. Lugha, hasa majina, sio lazima iwe na mantiki! Lugha ni mazoea (ya muda mrefu?) tu baina ya wanajamii katika kuwasiliana.
Hata jina la mafuta ambayo tumezoea kwa kiingereza kuyaita 'diesel' (dizeli kwa kiswahili), kimsingi linatoka na matumizi kama ilivyo 'mafuta ya taa'. Kilichoanza ni diesel engine (diesel likiwa jina la mvumbuzi wa aina hiyo ya injini ya gari)....hivyo mafuta ambayo yanatumika kwenye aina ya injini ya gari iliyovumbuliwa na diesel, wakaanza kuyaita diesel! ('dizeli' ukipenda 'mafuta ya dizeli'). Hata hivyo aina zote hizo za mafuta bado zina majina yake ya kitaalamu.