Ni Makosa kufikiri Musonda ni sawa na Phiri!

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Yanga leo wametambulisha top striker kutoka Zambia Kennedy Musonda ambaye pia ndio kinara wa magoli ligi ya Zambia.

Wapinzani wetu wamesajili mshambuliaji hatari na mbadala wa Fiston Mayele lakini ni vizuri tuwakumbushe kuwa huyu Musonda ni msimu huu ndio aliofanya vizuri na hatuwezi hata kujaribu kumfananisha na Moses Phiri ambaye amekuwa mmoja wa vinara wa magoli wa ligi ya Zambia mara kadhaa.

Sasa mashabiki wa Kibongo msishangae aka floppy huyo Musonda msiamini kama mlivyofikiri kwa Kambole. Pia msipende kufananisha wachezaji kienyeji, Moses Phiri si level ya Musonda hata kidogo. Phiri ni mchezaji hatari kwasasa kwenye ligi yetu na ame prove hilo tayari.

Musonda hana rekodi zaidi ya kuongoza kufunga kwenye ligi ambayo bado mbichi na tena msimu huu ndio kafanya vizuri, hana rekodi zaidi ya hii.

Uto tulieni acheni kelele nyingi na vi clip viwili tu vya Musonda visivyo na tija [emoji1787]

#nguvumoja

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Nimeona clip yake kwenye page ya muwatwalibu ikiwa na caption kapiga chenga uwanja mzima

Kum rate mchezaji kupitia clip ya sekunde 15 na kumjaza sifa tele kuwa ni hatari wala sio mchongo

Zipo clip za kina Kambole na yule waliyemtoa depo ya SBC huko majuu ambazo zinawaonesha wakiwa na viwango vya kutisha

Lakini leo hii wana Yanga hakuna ambaye anaweza kuridhishwa na maamuzi ya uongozi kama wakiafiki kuwabakiza kikosini.
 
Shida ni kuwa mnaanzishaga hizi nyuzi Kisha mnazikimbia baadae.

Ni mapema Sana ku conclude ulivyo conclude blaza. Ingelikuwa heri ungeliweka akiba ya maneno.

Yule blaza ako alifunguaga uzi wa kumponda Mayele Vs Kibu saa hizi hata haelewi sijui aufute sijui aseme account yake ilidukuliwa hakuwa yeye

Kuna namna nyingi Sana za kujipa moyo na kujiondolea machungu, Hakuna ulazima kujipa moyo kwa kuwaponda Yanga.
 
Nimeona clip yake kwenye page ya muwatwalibu ikiwa na caption kapiga chenga uwanja mzima...
Halafu hakuna clip ya maana zaidi ya hiyo na ile ya Priva! Hata Kibu ana matukio kuliko Musonda! Ukiniambia nichague kati ya Kibu na Musonda bora tubakie na Kibu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…