Ni makosa makubwa mno kwa mtawala wa nchi kuwachagulia wananchi wawakilishi wao

Ni makosa makubwa mno kwa mtawala wa nchi kuwachagulia wananchi wawakilishi wao

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,842
Reaction score
31,076
Hivi Leo Taifa letu limeshuhudia maajabu katika vituo vya kupiga kura katika kile kinachoitwa uchaguzi wa Serikali za mitaa, kwa vituo hivyo ambavyo huwa kawaida vinafurika watu, hivi Leo kuwa "vyeupe" kabisa!

Vyama vya upinzani 8, vikiongozwa na chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema, vilitangaza kuususia uchaguzi huo baada ya kubaini hila kubwa zilizoandaliwa na wasimamizi wa chaguzi hizo, ambao ni makada kindakindaki wa CCM, na kushuhudia wagombea wake, zaidi ya asilimia 95 wakiwa disqualified, katika sababu za kipuuzi kabisa!

Moja ya maajabu waliyoyafanya wasimamizi wa chaguzi hizo, ni kuwa-disqualify wagombea wa upinzani kuwa hawajui kusoma na kuandika, wakati wengine wao wamehitimu vyeti vya diploma katika vyuo mbalimbali nchini!

Wakati huo huo kwa maajabu ya dunia, eti wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi, asilimia 100, waka-qualify kuwa wagombea halali wa uchaguzi huo, hivyo kufanya maeneo mengi nchini, wagombea wa CCM kupita bila kupingwa!

Hila za uchaguzi huo zilianzia katika kufanya "siri" kubwa tarehe ya uchaguzi huo, wakati nchi hii ni ya mfumo wa vyama vingi, ambapo ni wajibu kushirikisha vyama vyote, vinavyoshiriki uchaguzi huo katika mchakato mzima wa uchaguzi huo

Lakini cha ajabu zaidi ni kitendo cha Rais wa nchi kuandaa kikao cha watendaji wa kata nchi nzima, kikao kilichofanyika jijini Dar, mwanzo wa mwezi wa September mwaka huu, ambacho sisi wananchi hatujaelezwa nini ilikuwa madhumuni yake ya kuitishwa, karibu kabisa na kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa

Hivi kwa wizara ya TAMISEMI kuwa katika ofisi ya Rais, hivi kitendo cha kuwaita watendaji wote wa kata wa nchi nzima, kitendo ambacho hakijawahi shuhudiwa kufanywa na watangulizi wake, hivi haiwezi kuwa "circumstantial evidence" kwa yaliyofanyika "gizani" katika kikao hicho, yame-reflect, uchaguzi huu uliofanyika leo nchi nzima kwa kuwanyima fursa wagombea wa upinzani na kufanya upendeleo maalum kwa wagombea wa chama chake cha CCM??

Hivi Rais anaona sawa kwa "kuwachagulia" wawakilishi wao, kwenye maeneo mbalimbali nchini??

Nijaribu tu kutoa mifano miwili ya namna Rais anavyo-influence wananchi wachague chaguo "lake" katika chaguzi zinazoendelea nchini

Alipokuwa kwenye ziara ya mikoa ya Kusini, Rais ali-influence wakazi wa jimbo la Tandahimba, wamchague msanii Harmonize awe Mbunge wa jimbo lao, eti kwa sababu ametunga wimbo wa kusifu utendaji kazi wa Rais!

Alipokuwa ziarani kwenye jimbo la Kongwa, alipokuwa akihutubia wakazi wa eneo hilo akawaambia kuwa Mbunge wao, Job Ndugai, anafaa sana, hususani kwa kuwadhibiti wabunge wa upinzani Bungeni na hivyo akawaambia wakazi wa jimbo hilo wamchague tena Mbunge huyo kwani"anatosha" kuliwakilisha jimbo hilo na hakuna mwingine anayefaa kuliwakilisha jimbo hilo!

Kwa Rais kuingilia uchaguzi wa maeneo mbalimbali nchini kumevunja mno ari ya wananchi walio wengi kujitokeza kwenye vituo vingi, mfano halisi ni uchaguzi wa Leo wa serikali za mitaa, ambapo vituo vingi vilikosa wapiga kura

Tutambue kuwa zoezi la kufanya chaguzi zilizo huru na za haki, ndiyo njia pekee, itakayotuhakikishia AMANI na UTULIVU wa kudumu ndani ya nchi yetu

Watawala wetu kuingilia kati sanduku la kura na "kutuchagulia" viongozi wao ili wawe wawakilishi wetu ni hatari mno kwa amani iliyodumu nchini mwetu kwa miongo kadhaa, na kwa hakika watawala wetu watakuwa wanakaribisha machafuko hapa nchini kwetu

Mungu ibariki Tanzania
 
Tusimlamu Rais kwa wapinzani kujitoa

Na hata hivyo si wapinzani wote waliojotoa
 
Tusimlamu Rais kwa wapinzani kujitoa

Na hata hivyo si wapinzani wote waliojotoa
Wewe kila topic inayoanzishwa humu JF unakuwa miongoni ya wa kwanza kureply...........

Hakika unaitendea haki hiyo buku 7 unayoipata huko Lumumba!
 
Hata ukichunguza nchi nyingi ziozoingia kwenye machafuko nchini mwao, chanzo kikuu ni kwa watawala wao kutaka kuchezea haki ya wananchi kwa kuchezea sanduku la kura
 
For the first time in Katika historia ya Tanzania kunafanyika “Sharm Election”

Jiwe amejinyea kabisa legacy yake!

Sijui vitabu vitakuja kuandika madudu gani ya huyu mtu?
 
For the first time in Katika historia ya Tanzania kunafanyika “Sharm Election”

Jiwe amejinyea kabisa legacy yake!

Sijui vitabu vitakuja kuandika madudu gani ya huyu mtu?
Wewe ndiyo unasema kuwa Jiwe amejiabisha, lakini yeye mwenyewe anaona kilichotokea ni sawasawa kabisa!

Hakika safari hii watanzania tumepatikana!
 
Nimecheka sana kuona vituo vyeupe utafikiri kuna sindano ya chanjo mitaani
 
Watu wameshachoka na hz sanaa za siasa na uchaguz umepoteza maana yake

So mtu haoni umuhim wa kwenda kupoteza mda wake kupanga folen apige kura while mshindi anajulikana
 
Mlikimbia sasa kelele za nini ?mlitaka uchaguzi urudiwe mkashtukiwa watu wamepiga kura na ushindi wa kishindo

Fanyeni maasi tuwaponde

State agent
 
Mtamlaumu mzee wa watu bure
mngewalaumu vionozi wenu kwanza kwanini waliamua kujiengua kwenye mchakato
 
Kwanini mnalalamika sana au uamuzi wa kususa ni wakukurupuka au matarajio ya kususa yalikuwa ni nini pengine ni ili kupata cha kusema
 
Mlikimbia sasa kelele za nini ?mlitaka uchaguzi urudiwe mkashtukiwa watu wamepiga kura na ushindi wa kishindo

Fanyeni maasi tuwaponde

State agent
Usiombe hivo tunajua mmetumwa kuvuruga amani yetu lkn kumbukeni mlango Wa the hague uko wazi.Akiumaliza upinzani ataimaliza ssm ataunda mfumo wake mtaelewa mkiwa mshachelewa,makamba alikenua meno Leo analia,mwingine kaandika kitabu cha kuwaomba radhi watz
 
Back
Top Bottom