Ni malengo gani ambayo umejiwekea na unaamini utafanikiwa kuyatimiza?

Ni malengo gani ambayo umejiwekea na unaamini utafanikiwa kuyatimiza?

King Jody

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
1,834
Reaction score
3,456
Habari za kutwa wanajukwaa?,

Kwenye maisha kila mtu ana malengo yake aliyojiwekea kutokana na kile ambacho anatamani kutimiza maishani lakini kwa sababu ya changamoto mbalimbali za maisha unashindwa kutimiza kwa wakati lakini unakuwa na imani iko siku ndoto yako itatimia.

Kwa upande wangu mimi kutoka moyoni natamani sana kujenga nyumba ya Ghorofa, na tangu nilipokuwa mdogo niliwahi kumwambia mama yangu, siku nikiwa mkubwa nitapambana hadi nijenge nyumba ya ghorofa.

Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu ambaye namuamini kwa ailimia 100 najua nitafanikiwa, ni swala la muda tu.

Vipi kwa upande wako unapambania kutimiza ndoto gani?

NB. Mungu kwanza.
 
Back
Top Bottom