Kama mtu humuamini kiasi cha kitokumshirikisha kipato basi usioane naye.
Maana kwa mfano unamwambia mwenzi wako kuwa unapokea mshahara
Mume= laki 3 badala ya milion 1 labda. Huoni kama hamtaweza kupanga malengo kulingana na kipato? Yani hapo unamdanganya nani?
Hiyo kufichaficha huwa mnaenda mbali mtu anajenga mpaka nyumba kwa kificho halafu Mungu anakuita wakati mwenzi wako hajui kama ulijenga sehemu. Mtakuja kupoteza assets bila sababu za msingi....
Mke naye akijua kuna pesa unamficha...naye anaanza kuficha au kujenga kwao yani sasa mume anafichia huku mke naye anafichia kule....Wajinga wawili mnashindana kutawanya mali na mwisho mkifa watoto wadhulumiwa mali zenu...ovyo kabisa