Ni mambo gani ungependa yazingatiwe katika Katiba Mpya?

MaweSaba

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2024
Posts
416
Reaction score
641
Ni reforms zipi au mambo ungependa katika mpya izingatie?

✅️ Mamlaka ya Riasi yapunguzwe na Uhuru wa mihimili yote
✅️ Zuio la mwenyekiti wa chama tawala kua Raisi wa Nchi
✅️ Ardhi ya Tanzania iwe mali ya wananchi, si Raisi, kasoro mali asili
Serikali imiliki 70% ya ardhi huru na kuwapa waeekezaji wazawa 80% na foreigners 20%
✅️ Uraia pacha, serijali uruhusu uraia pacha kwa maendeleo ya kielimu, na kadhalika
Cap ya mishahara ya wabunge na watumishi serikalini kuondokana na ubadhirifu wa pesa na mianya ya Rushwa, walipwe 2M wabunge
✅️ Kuondoa Wakuu wa Mikoa, Ma DC, hawana kazi ni vyombo vya kisiasa tu, wabaki Meya na team ya madiwani na wakurugenzi
✅️ Raisi aweze kushtakiwa

Ongeza za kwako
 
Mtu yeyote anayetaka nafasi ya kuchaguliwa au kuteuliwa iwe ni Ubunge, Urais au Uwaziri ni lazima aweke mali na biashara zake zote chini ya uangalizi wa kisheria au aziuze kabisa kabla ya kuingia madarakani. Huwezi kuwa mtunga sheria huku wewe ndio mfanyabiashara mkubwa nchini.

Katiba mpya iunde Mahakama Maalum ya Katiba inayoshughulikia mafisadi tu, na mtuhumiwa akipatikana na hatia, mali zake zitaifishwe.

Ilani ya chama na ahadi zote anazotoa mgombea jukwaani ziandikishwe kisheria. Mbunge au Rais akishindwa kutekeleza angalau 60% ya ahadi zake ndani ya miaka mitatu ya kwanza, wananchi wawe na haki ya kikatiba ya kumng'oa madarakani bila kusubiri miaka mitano iishe.
 
1. Waziri asiwe mbunge au mwanasiasa mwenye cheo katika chama chochote cha siasa.
2. Waziri mkuu asiwe mbunge
3. Spika asiwe mbunge
4. Viti maalum bungeni vifutwe
5. Rais asiwe na mamlaka yoyote juu ya bunge, awe mtazamaji kama sisi raia.
6. Mawaziri wapigwe interview na bunge kabla ya kuthibitishwa na pia bunge liwe na mamlaka ya kumng'oa waziri.
7. Elimu ya mbunge angalau degree iliyonyooka, elimu ya waziri angalau masters vivyo hivyo elimu ya Rais angalau masters iliyonyooka.
8. Kusiwe na wabunge wa kuteuliwa na rais.
9. Mikoa iwe na mamlaka ya kutumia pesa zao za mapato kwa shughuli za kimaendeleo sio kila kitu kusubiri kutoka serikali kuu.
10. Waziri mkuu achaguliwe na wabunge na sio jina litoke kwa rais.
11.Meya achaguliwe na wananchi na asiwe diwani,awe mtu mwingine na majukumu yake yajulikane kiuwazi sio sasahivi majukumu ya meya hayaeleweki.
 
Napingana na wewe katika hoja zifuatazo:

1. Sikubaliani na wewe katika hoja ya kupunguza mamlaka ya Rais na wengi wanaotoa hoja hii wanaitoa kimihemko tu. Ili Taifa liwe imara ni lazima awepo kiongozi mwenye mamlaka na ukuu, ukipunguza mamlaka ya Rais utasababisha mamlaka ndogo ndogo zijivike ukuu na hapo ndio tunaona matukio ya ajabu ajabu nchini.

2. Hoja ya kuzuia Mwenyekiti wa Chama kuwa Rais imekaa kishabiki. Mwenyekiti wa Chama ni kiongozi kwenye Chama na Rais ni kiongozi kwenye nchi na mamlaka zao ni tofauti. Rais hata asipokuwa Mwenyekiti wa Chama halisi anakuwa Mwenyekiti wa Chama kivuli ,ukinielewa utanishukuru.

3. Ardhi ya Tanzania ni mali ya Serikali na sio Rais ndio maana hakuna Rais aliyejipa umiliki ila Rais ni msimamizi tu na hakuna mwekezaji anayemiliki ardhi ila anaitumia tu kwa maslahi ya nchi.

4. Suala la uraia pacha hata katiba mpya isiruhusu kwa sababu za kiusalama na utaifa wetu. Kuna siku utakuja kuongozwa na mchina ,ndo utakuja kulia na kujuta.

5. Wakuu wa mikoa na wilaya ni nafasi muhimu katika kuratibu shughuli za Serikali na wanafanyiwa vetting nzuri. Meya ni kiongozi ambao anaweza asiwe na uzoefu wala ujuzi , uratibu wa shughuli za Serikali utakosa mratibu mzuri.

6. Kushtakiwa kwa Rais kuelezewe kwa upana zaidi.
 
3. Hata sasa spika sio lazima awe mbunge ila kwa naibu spika ni lazima.
5. Hata sasa bunge ni chombo huru chenye mamlaka yasiyoweza kuingiliwa na Rais.
9. Mikoa ikiwa na mamlaka hayo Kuna mikoa itarudi nyuma sana kiuchumi na kimaendeleo.
10. Wabunge watamchaguaje bila kupendekezwa?
11. Labda wewe ndio huelewi majukumu ya meya
 
Kwani katiba si ilishaandikwa na Warioba, nchi ikatumia mabilioni ya shilingi na wananchi wakaulizwa wakasema wanachotaka sasa katiba gani tena unaulizia mkuu
 
Iwekwe kwamba" spika asiwe mbunge" na sio " spika sio lazima awe mbunge", vivyo hivyo kwa naibu spika, asiwe mbunge.
Bunge ni huru wakati rais anateua wabunge wake humo? Vipi kuhusu mamlaka ya kuvunja bunge rais hana??( nieleweshe). Namaanisha rais asiwe na wabunge wake wa uteuzi na asiwe na mamlaka ya kuvunja bunge( kama anayo kwa sasa).

Mikoa itarudi nyuma!!, irudi nyuma mara ngapi mkuu? Geita kuna dhahabu ya kumwaga lakini hata stendi yake ya mkoa tu inatia kichefuchefu, Morogoro kuna sehemu wanalima sana na mazao yanatoka ila barabara zipo hoiiiii. Kuna sehemu kati ya Mpwapwa na Iringa panaitwa Kinusi ,vyakula vinavyotoka kwenye hiyo ardhi ya Kinusi ukila hausahau,yaani pamebarikiwa, ila miundombinu na huduma za kijamii ni sifuri. Mikoa ipewe mamlaka zaidi.
Huyo wa kupendekezwa apendekezwe na wanachama wa vyama sio rais.
Kingine kuhusu majukumu ya Meya,tunakuwa hatuyaelewi kwa sababu let say Ubungo,kuna mkuu wa wilaya,kuna mbunge,kuna meya. Kama vipi basi mkuu wa Wilaya asiwepo .Vivyo hivyo kwa majiji, kuna mkuu wa mkoa,halafu kuna meya,basi mkuu wa mkoa atolewe nafasi yake ichukuliwe na Meya. Haya ni maoni yangu tu na naweza nisiwe sahihi
 
Wewe ni kada wa chama ndo maana unapinga kila zuri ili muendelee kutuibia.ardhi ni mali ya serikali siyo rais na serikali ni nani.je rais akitaka kuchukua ardhi yoyote ile nani atamzika?Marc na mada hata mimi sioni kazi yao so ni budi wakiwepo.naumgana na wewe kwenye swala la uraia pacha tu.rais wetu ana mamlaka makubwa mno hivyo ni budi apunguziwe mfano kwenye mamlaka ya uteuzi nk
 
Kingine Internet iwe haki ya kikatiba kama haki zingine, kusiwe na mtu yoyote mwenye mamlaka ya kuzuia upatikanaji wa Internet au kufungia mtandao wowote wa kijamii kisa tu amejisikia. Na mwisho mgombea huru, kuna watu wanatamani kuwa viongozi ila mambo ya wajumbe yanawakatisha tamaa. Ukihonga wajumbe baadae ukipata uongozi huwezi kukemea rushwa maana hata hiyo nafasi ya uongozi umeipata kwa kutoa rushwa. Mgombea huru ni muhimu.
 
1. Jaji mkuu asiteuliwe na Rais. Umoja wa majaji upendekeze majina matatu kwa Rais, mmojawapo ateuliwe kuwa Jaji Mkuu.

2. Majaji wote wasiteuliwe na Rais, bali Jaji mkuu apeleke mapendekezo kwa Bunge, kisha Bunge lipitishe majina kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, kisha Rais awatangaze.

3. Kwenye uwekezaji wowote wa nje, ni lazima 30% imilikiwe na wawejezaji wazawa.
4. Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Polisi, Mjuu wa TISS, wasiteuliwe na Rais, bali Rais ayapeleke majina mawili Bungeni, na Bunge lipitishe jina moja katika wanaopendekeza, kama wote hawafai, wawakatae wote, kisha Rais alazimike kupeleka majina mengine.
5. Kuwepo chombo kitakachoundwa na Bunge, na kupitidhwa na mahakama kuu kwaajili ya kufuatiliaji maafili ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi, TiSS na Magereza. Chombo hicho kiwe na uwezo wa kumshtaki mhusika yeyote aliyekiuka maadili ya kazi, kama vile kubambikia watu kesi.
6. Kitiba itamke kuwa kutakuwa na sheria inayozui utekaji na upotezaji watu, ambapo atakayepatikana na hatia hiyo, atafungwa maisha.
7. Kila mamlaka katika utendaji wake kazi itazingatia sheria inayolinda haki za binadamu, uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari, na demokrasia ya uchaguzi. Yeyote atakayedhihirika kukiuka, adhabu yake iwe kwenda jela kwa kipindi kisichopungua miaka 5. Hii iwahusu tume ya uchaguzi, polisi, TISS, wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri.
 
Bunge ni chombo huru kwa misingi ipi ikiwa jina la waziri mkuu linapendekezwa na Rais, mawaziri wanateuliwa na Rais, huoni kama hao wanabaki kuwa watetezi wa Rais hata penye madudu. Kutwa wanamwaga sifa kama Rais ni Mungu wao.
 
Kila hoja umepinga... kama una akili timamu na hauna ushabiki... hali ya sasa ya taifa letu kumejawanna hofu na wananchi tunajihisi watumwa wa watawala. Taifa lolote la kidemokrasia linapaswa kua na VIONGOZI sio watawala.

Kwa Tanzania ukimsikia Mkuu wa Mkoa wa Dar kama mwananchi utajihisi mdogo sana wakati mamlaka yalipaswa kutoka kwa wanqnchi kwenda kwa kiongozi
 
Madikteta wengi walitokana na mfu,o huu wa uongozi. Mwenyekiti kua Raisi kunaleta uchawa na kinyima uhuru wa mihimili kutokana na kutoka chama kimoja na kiongozi wao wa chama kua Raisi. Angalia Bunge la sasa lilivyo dhaifu na halipendwi, wanayoyazungumza pale ni sifa ni utukufu sio uwakili wa wananchi
 
Ardhi ya Tanzania ni mali ya Serikali na sio Rais ndio maana hakuna Rais aliyejipa umiliki ila Rais ni msimamizi tu na hakuna mwekezaji anayemiliki ardhi ila anaitumia tu kwa maslahi ya nchi.
Hujui sheria wewe, kwa nchi za wenzetu wananchi ndio wamiliki wa Ardhi. Miji yetu haijengwi vizuri kwa sababu ya haya mambo. Hamna mwananchi mweny uhakika wa umiliki ndio maana tunalipia kodi ya Ardhi. Hatuna umiliki wa nchi yetu licha ya kusema tupo kwenye nchi yetu
 
Usalama upi unaosema wewe? Kipindi cha AFCON, issue za UTALII basi zisiwepo kwa sababu ya usalama. Acha ushamba brother

Dunia ya sasa ni kijiji, nchi zilizoendelea za kiafrica zinatambua umuhi,u wa wananchi wao kuelimika na kufika ulimwenguni.
superpower zote hazikupata nguvu kwa kujifungia, walitoka nje ya nchi zao na kujifunza nje ya nchi zao na kurudi nyumbani au kupata mali na kujenga nchi zao
Suala la uraia pacha hata katiba mpya isiruhusu kwa sababu za kiusalama na utaifa wetu. Kuna siku utakuja kuongozwa na mchina ,ndo utakuja kulia na kujuta.
 
Wakuu wa mikoa na wilaya ni nafasi muhimu katika kuratibu shughuli za Serikali na wanafanyiwa vetting nzuri. Meya ni kiongozi ambao anaweza asiwe na uzoefu wala ujuzi , uratibu wa shughuli za Serikali utakosa mratibu mzuri.
Huna uelewa na maswala ya uongozi, una UCHAWA.

Watu kama ninyi kwneye issue za kujenga Taifa letu muhamie Burundi pamoja na yule alietuambie tuhamie huko kwa issue za tozo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…