Pre GE2025 Ni mambo gani yanawakwamisha Wanawake kuingia katika Siasa na Uongozi hapa Tanzania?

Pre GE2025 Ni mambo gani yanawakwamisha Wanawake kuingia katika Siasa na Uongozi hapa Tanzania?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Katika ulimwengu wa kisiasa, wanawake wanakutana na vikwazo vingi vinavyozuia ushiriki wao kamili. Na sio tu kwa nafasi kubwa kama Ubunge na Urais, kuanzia huko kwenye Uwakilishi wa Serikali za Mitaa na Udiwani

Upendeleo wa kijinsia na ukosefu wa rasilimali ni baadhi ya changamoto kubwa zinazowakabili.

Hali hii inawazuia wanawake wengi wenye uwezo kuingia na kushiriki kikamilifu katika nafasi za maamuzi.

Tunahitaji kufikiria kwa kina na kuchukua hatua madhubuti ili kubadilisha hali hii.

Haki ya kushiriki katika siasa ni ya kila mtu, bila kujali jinsia.

Ni wakati wa kuweka usawa wa kijinsia kuwa kipaumbele na kuhakikisha kwamba sauti za wanawake zinasikika na zinathaminiwa

Unadhani changamoto zipi zinakwamisha wanawake kuingia kwenye siasa?
 
Pamoja na kupigiwa chapuo, favour mnazopata mnataka nini tena??
Wanawake wafuatwe majumbani kuombwa wagombee nafasi mbalimbali .

Mimi naona ni muamko mdogo, kutojiamini na wanawake wengi kutovutiwa na siasa hasa kuongoza watu.
 
Natamani sana kuona wanawake wanakuwa viongozi ila najiuliza nitajisikiaje siku Moja nikienda nyumbani Kwa kiongozi wangu wa kike nikamkuta anakaangwa makofi na mume wake kisa ameunguza mboga?
 
Mipaka ya kijinsia Bado ipo kwenye jamii zetu. Na mbaya zaidi wanawake Bado wanazingatiwa kama watu wa makundi maalumu.

Mwanamke kuzingatiwa kama mtu wa kundi maalumu ndilo jambo linaloendeleza uwepo wa mipaka ya kijinsia katika fursa mbalimbali za kijamii ikiwemo fursa ya uongozi.

Ukianzia kwenye ngazi ya shule watoto wa kike mara nyingi wanapatiwa misaada ya kujisitili na mambo mengine kuliko watoto wa kiume kwahyo hizo Hali zinaendelea kuwafanya wanawake waonekane kwamba wao ni wa makundi maalumu hivyo wanahitaji zaidi uangalizi wa wanaume na taifa Kwa ujumla.

Usawa hautakiwi kuwa wa upendeleo Bali kila binadamu anayetakiwa kuwa sawa na binadamu mwenzake basi awe sawa kiasili. Asili ndo itumike kuweka usawa lakini ikiwa kila siku tutaimba kuhusu kulazimisha fursa Kwa wanawake basi tutakuwa tunaendelea kuwafanya wanawake waonekane wao ni watu dhaifu kiasili.

Ili kuondoa changamoto zote zinazominya ushiriki wa wanawake kwenye masuala mbalimbali ya kijamii tuhakikishe tunaondoa misingi yote inayowaweka wanawake kwenye makundi maalumu na nafasi za upendeleo.

Hakuna haja ya kulazimisha mada Bali kila jambo liwe kiasili na mabadiliko yaanzie kwenye familia zetu.

Hakuna namna mwanamke anaweza kuwa na nguvu kama mabadiliko hayataanzia kwenye familia yake.

Wanawake kama wanataka kuwa kama wanaume na wawe sawa kwenye mambo yote ya kijamii na kitaifa basi waache unyonge na wasiwe wanapenda penda misaada na kuonekana kama wao ni kama watu wa makundi maalumu. Je wataweza?? Kazi kwao.

Uwezo kiakili na utendaji wa shughuli mbalimbali, wanawake wamekuwa wakionesha ufanisi mdogo sana na wengi wao wamekuwa wakiamini na kuwategemea wanaume katika kufanikisha shughuli hizo.
Wanawake wenyewe wanawaamini sana wanaume kuliko wanavyojiamini wao wenyewe kwenye mambo mbalimbali yanayotegemea nguvu na akili.

Iwe shuleni au kazini wanawake wengi wanaamini sana wanaume katika kutimiza ufanisi wao (Fanya utafiti juu ya Hilo).

Mfano wa kuhitimisha: mwanamke wa miaka 60 au 50 anaweza kumuamsha kijana wake wa kiume wa miaka 10 usiku ampeleke nje kukojoa. Kwahyo wanawake wenyewe ndo wanaweza kuamua Nini Cha kufanya ili wasionekane kama wao ni wa makundi maalumu.
 
Katika ulimwengu wa kisiasa, wanawake wanakutana na vikwazo vingi vinavyozuia ushiriki wao kamili. Na sio tu kwa nafasi kubwa kama Ubunge na Urais, kuanzia huko kwenye Uwakilishi wa Serikali za Mitaa na Udiwani

Upendeleo wa kijinsia na ukosefu wa rasilimali ni baadhi ya changamoto kubwa zinazowakabili.

Hali hii inawazuia wanawake wengi wenye uwezo kuingia na kushiriki kikamilifu katika nafasi za maamuzi.

Tunahitaji kufikiria kwa kina na kuchukua hatua madhubuti ili kubadilisha hali hii.

Haki ya kushiriki katika siasa ni ya kila mtu, bila kujali jinsia.

Ni wakati wa kuweka usawa wa kijinsia kuwa kipaumbele na kuhakikisha kwamba sauti za wanawake zinasikika na zinathaminiwa

Unadhani changamoto zipi zinakwamisha wanawake kuingia kwenye siasa?
Wanawake ni machawa.
 
Back
Top Bottom