Ni mambo yapi ya kuzingatia katika uanzishwaji wa kiwanda?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Habari wakuu

Natumaini wote tulisoma kwenye zile shule zetu mambo mbali mbali, ikiwemo mambo ya kuzingatia katika uanzishaji wa kiwanda.

Inawezekana yale tuliyoyasoma shule, tumeyaacha kule kule na sasa tupo miaka zaidi ya kumi kwenye kuajiriwa, bila kuwa na hata karakana ya kunolea mapanga na visu.

Kupitia uzi huu, tutajie yale mambo ya kuzingatia, na utujulishe umekwama wapi katika kufanikisha lengo husika.

Kumiliki kiwanda au karakana inawezekana.​
 
fahamu ukubwa wa kiwanda unacho taka kuanzisha.
Vibali
Unakumbuka kule shuleni waliovyokuwa wakitufundisha ''Factors affecting the location of industries''?
Majibu ndio yako hapo, kama tutaamua kufanya kwa vitendo; si lazima uanze na kikubwa, kama unaweza kuwa na mkopo wa gari kwa nini huku ushindwe?​
 
Mkuu mimi hata shule sija wahi kwenda, so stop trying to make me remember things that I don't even know.
 
-Mtaji wako
-Wateja unaowalenga
-Aina gani ya bidhaa unataka kuuza
-Vibali na leseni
-Eneo unalotaka kuweka kiwanda
Consult SIDO,BRELA,TRA,TIC,EPZA utapata muongozo mzuri
 
Niliwahi chungulia file la kampuni moja

Kiwanda chako kinazalisha nn?

Ukishajua utaelewa kuna issue za regulators kwenye sekta utakayokuwako hao ndo wenye vibali ukianzia TRA, TBS, NEMC, OSHA, TIC, TMDA, AU KAMA NI UJENZI WANA ORGANIZATION YAKE, HAPA LAZIMA VIBALI VIWE VINAVYOHITAJIKA ILI UWEZE KUFANYA BIASHARA........

MTAJI,

ENEO LILIPO KIWANDA,

WAFANYA KAZI, SKILLED AND UN SKILLED

WADAU WENGINEO
 
-Mtaji wako
-Wateja unaowalenga
-Aina gani ya bidhaa unataka kuuza
-Vibali na leseni
-Eneo unalotaka kuweka kiwanda
Consult SIDO,BRELA,TRA,TIC,EPZA utapata muongozo mzuri
Tuanze na malighafi kwanza, ulishawahi kwenda sehemu ukakuta bidhaa toka shambani ziko nyingi mpaka zikatupwa na kuoza?
 
Tuanzie kwenye upatikanaji wa malighafi kama sababu ya kwanza, ya pili tuangalie nguvu kazi, alafu hizo zingine zifuate.
 
Kuzoeana na wanasiasa na wakuu wa nchi ili kusaidiwa mchakato wako kuwa haraka.

Kuwa chaguo la ccm ili wasije kukupa hasara.
 
Kuzoeana na wanasiasa na wakuu wa nchi ili kusaidiwa mchakato wako kuwa haraka.

Kuwa chaguo la ccm ili wasije kukupa hasara.
Kwa mfano, umeenda kutembelea kijiji x, ukakuta wakulima wanalima labda alizeti; wakakuambia tumelima kiasi kikubwa sana na hatuna sehemu za kuzipeleka; kwa mazingira hayo, utategemea chama ndio kikuambie ufanye nini?​
 
Figisu za mtwara umezisahau na korosho kipindi cha magufuri.

Hii nchi kuna mambo mengine unaweza ukapoteza pesa kama nilivyokueleza.

Kuna tajiri mmoja kahama shinyanga kiwanda kilinyanyuka kwa ajili ya magufuri tu.
 
Nakubaliana na hoja yako, ata siasa imekuwa ni sehemu ya kizuizi na pia ni kitu cha kuzingatia. Lakini isiwe sababu kuu ya kuzuia kile unachotaka kufanya, kwa sababu kuna taratibu za kufuata ili kupata vibali.
Mfano, umeenda sehemu ukakuta kuna malimao mengi mpaka yanaoza; lakini kichwani mwako una ujuzi wa kuyageuza yale malimao kuwa sabuni; ungekuwa wewe ungefany anini?​
 
Shida utakula vikwazo na sababuni zako mpaka akili zikukae sawa.
Kuna jamaa yangu alitaka kufungua kiwanda kikubwa cha bidhaa X baada ya kuona kama ulivyo sema.

Kama ushuzi ulipata wajambaji kuanzia ngazi za serikali na kwengine wote wakitaka pesa kwanza wakati mtu anataka kukuza sekta na fursa kwanza.
 
Tatizo linaweza kuwa nini hasa, chuki au kutokufuata utaratibu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…