This is called reverse psychology. Makolo wanajua wameshafikia kikomo. Hawana timu ya kumfunga Al Ahly. Timu yao sasa hivi ni mbovu kuliko ile ya mwaka jana walipocheza na Ahly. Mioyoni nwao wanajua kuna uwezekano mkubwa wa Yanga siyo kuvuka robi final tu but hata kufika final. Kwa sababu akimfunga Mamelodi atakutana na Esperance au Asec ambazo ni timu za kawaida sana. Na akifika final timu ambayo ni likely kukutana nayo ni Ahly. Wanajua kwamba Yanga katika ubora wao wanaweza kumfunga Ahly na kuchukua uningwa CAFCL.
Sasa kwa nini hawa ndugu zetu wanaweweseka hivi? Wanajua katika msimu mmoja Yanga atafyeka vichaka vya kufika robo, kumfunga Mamelodi, kufika nusu final, kumfunga Ahly, na kuchukua ubingwa wa CAFCL.
Kihoro kitakachowapata ni kikubwa.
Kwa hiyo mashabiki wa Yanga waoneeni huruma ndugu zetu. Si mmeona walivyonywea baada ya Yanga kufika final ya CAFCC kichaka chao cha kwanza. Halafu wakapigwa hamsa kama wamesimama kichaka chao cha pili wakamfukuza na kocha.
Sasa hivi vichaka vilivyobaki vikifyekwa watabaki uchi.
Kwa makolo nawashauri kuweni na akiba ya maneno. Hii Yanga itawaumiza sana. Wengi wenu mtahamia Fei Toto FC.
Kwa mara nyingine niwape sifa mashabiki wa Yanga kwa utulivu wenu na maturity yenu mliyoonyesha tofauti na upande wa pili ambao utafikiri ni watoto wa chekechea.