Ni maswali yapi ntambana huyu mtu kisheria.

Ni maswali yapi ntambana huyu mtu kisheria.

scientificall

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2015
Posts
457
Reaction score
328
Kuna jamaa kanisingizia eti nimemuibia na kudai kuwa usiku aliniona kwa mbali nkikimbia na mali yake.

Pia mtu huyu katoa maelezo yanayotafautiana zaidi ya mara 3.

Akidai alishuhudia mali yake ikiibiwa kupitia dirishani usiku wa saa saba ikichukuliwa simu kwanza na baadae computer, na akaja kustuka asubuhi saa 1:30 na kutoa taarifa kwa majirani kuwa kaibiwa na kuntaja mimi eti nlikuwa miongoni.

Nilipigwa search mda huohuo hakunikuta na mali yake yoyote wala kielelezo,
Mimi naishi na mdogo wangu hivyo ni shahidi wa kutosha.

Mwanzo alitaka nimlipe hata nusu ya gharama za mali yake ili kesi iishie polisi lakini kwakuwa mimi sikufanya hivyo nikakataa na kutaka twende mahakamani.
Kesi yetu ipo mahakama ya mwanzo na tunasubiri kusikilizwa.

Je ni maswali gani ntamuuliza huyu anaenituhumu ili nimnyooshe maana kanidhalilisha sana.
NAWASILISHA.
 
Kwangu nimelala na alikuja kuripoti tukio asubuhi saa 1:30 toka saa saba usiku nyumba ni moja ila vyumba tofauti
muulize alichukua hatua gani ya papo kwa papo wakati wa tukio alipokuona kama anavyodai.
 
Unacho takiwa ni kutia dosari ushahidi au maelezo yake.
 
Back
Top Bottom