Ni matokeo ambayo 'JF Football Pundits' na wenye 'Maono Makali' tuliyatarajia, ila Msimu ujao Simba SC isajili Wachezaji wa uhakika hasa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kama Uongozi wa Simba SC na 'Scouting Team' ya Simba SC itakuwa tayari basi itupe Sisi JamiiForums Football Pundits na Watu wenye Maono Makali Jukumu la Kuwaambia ni Wachezaji gani Wazuri na Mahiri wanafaa Kuichezea Simba SC yetu kwa Msimu ujao.

Wengine uzuri wetu hatuishii tu Kuuchambua au Kuuroga au kuufanyia Umafia Mpira wa Bongo ( Tanzania ) lakini pia hata Mpira wenyewe nao tumeucheza, tunaujua na enzi zetu tulikuwa Mahiri hivyo tukikuambia kuwa Mchezaji fulani anafaa na fulani hajui tuamini kwa 99.9999%.

Niliwahi kuja hapa na Uzi wa kwanini Simba SC iliachana na Said Ndemla na Kumsajili Saido Kanoute sikueleweka na wasioujua Mpira na leo ukosoaji wangu kwa Kanoute ndiyo unaeleweka.

Niliwahi kuja na Uzi hapa hapa kuwa hakukuwa na haja ya kuachana na Mchezaji Perfect Chikwende na Kumsajili Kinda Peter Banda kama kawaida sikueleweka ila leo baadhi ya Watu wanaanza Kunielewa.

Niliwahi hapa hapa JamiiForums kuja na Uzi wa Kumsema Beki Henock Inonga Baka kuwa ana Utoto mwingi, Upuuzi, Sifa za Kijinga, mtaka Attention za Kipumbavu, ana Dharau na kwamba pamoja na kwamba ana Kipaji Kikubwa ila aambiwe upesi ili abadilike kwani atakuja Kutugharimu sikueleweka lakini baada ya Kuchomesha mechi kadhaa za Ligi na hata Mchezo wa jana Kucheza vibaya sasa baadhi ya Watu wanaanza Kunielewa kwani Jicho langu la Kiuchambuzi halijawahi Kukosea pale nikizungumzia Jambo fulani.

Vile vile kabla ya Usajili wa Msimu huu na hata Kipindi cha Usajili wa dirisha Dogo nilionya kuwa Mwekezaji wa Simba SC Mohammed Mo Dewji afanye Usajili wa maana na siyo tu wa Kibahili na wa 'shaghala bhaghala' kama walioufanya sikueleweka lakini kwa muenendo wa Simba SC wa sasa ( hasa Kimashindano ) iwe ni ya Ndani au ya Nje naamini sasa naanza Kueleweka.

Kwa ilikofikia Simba SC Wachezaji kama Pascal Wawa, Saido Kanoute na Chris Mugalu ( kwa Wageni ) hawakutakiwa kuendelea kuwepo Simba SC ila kwakuwa bado Simba SC kuna ule Uswahili wa 10% Wachezaji hawa bado wapo Klabuni na Kuonekana kuwa wana Umuhimu wakati binafsi Umuhimu wao Simba SC sijauona.

Nilishauri hapa hapa JamiiForums kuwa Uongozi wa Simba SC ama uachane na Kipa Namba Mbili Beno Kakolanya na imtoe kwa Mkopo Kipa wake Kinda Ally Salim ili nafasi zao waletwe Makipa Wawili mahiri wa Kigeni na Mzawa ila kumpa Ushindani Kipa Aishi Manula na pia kumfanya awe na 'back up' nzuri pindi akipatwa na dharula lakini halikufanyika Matokeo yake sasa Wana Simba SC wote Siku Kipa Aishi Manula akikosekana na Wakadaka wengine Sisi Mashabiki muda wote Roho zetu huwa zinadunda tu huku ama tukibana au tukishika tu Pumbu zetu kwa Imani ya Kipumbavu kuwa ndiyo hatutofungwa wakati Kiuhalisia Kufungwa kupo pale pale.

Sitaki kuwataja Wachezaji wa Ndani kwani nitapatwa tu na Hasira bure ila itoshe tu kusema kuwa 75% ya Wachezaji Wazawa walioko Simba SC hii ya sasa hawana Hadhi ya Kuichezea Simba SC na hawatakiwi hata kuendelea kuwepo, ila wameachwa kwa Uwoga wetu wa Kipuuzi kuwa Simba SC ikiwaacha ( ikiwatema ) basi Watahamia kwa Mahasimu wetu Yanga SC na watakuja kuwa Mwiba Mchungu Kwetu.

Namalizia tu kwa kusema kwamba kuna tofauti moja tu ya Kiufundi kati ya Usajili uliofanywa na Yanga SC na wa Simba SC. Yanga SC wamesajili Wachezaji wa Kazi na Matokeo huku Simba SC imesajili Wachezaji wa Kimazoea, wa bahati nasibu na wa Kupiga Selfies huku wakishinda Mitandaoni muda wote kutafuta Followers tu.

Simba SC inawahitaji Wachezaji wa Kigeni wenye ama Uwezo sawa na Mchezaji Victorien Adebayor wa US Gendamarie FC ambao ni 'Complete Players' na kanwe si hawa wa 10% na wa Kubahatisha.

Na Sitoshangaaa Yanga SC wakiwa Mabingwa wa 2021 / 2022 NBC Premier League kwani wana Wachezaji ambao hata kama ukiwa ni mwana Simba SC lia lia kama Mimi utavutiwa nao na utafurahi pia Kuwatizama wakiwa Wanaupiga mwingi kama Aucho, Bangala, Saido na Mayele.

Simba SC tulikosea sana katika Kusajili.

Cc: Daudi Mchambuzi
 
Kweli sisi wabetiji ndio tunajua utabiri wetu wa hali ya juu zaidi hata wa mfalme Zumaridi
 
Nimesoma neno kwa neno mwanzo hadi mwisho,ushauri mzuri wa kiufundi wenye uzalendo wa kishabiki ndani yake

Nikisummarize nilichokielewa ni kwamba
1.Simba iacha kusajili kwa mazoea,kusiwe na uswahili wa 10%

2. Simba iachane wachezaji wazawa wote isipokuwa A.Manula Apate changamoto ya makipa wawili wa kigeni pia isaidie kumpa backup anapopata dharura.
na simba iondokane dhana ya kuwa wakiwaacha wachezaji hao watakimbilia timu pinzani

3. Rais wa heshima boss Mo dewj awekeze pesa za kutosha kusajili wachezaji wa kigeni wenye kariba ya akina Victory Adebauor


Ila shida sasa huyo Mo atakubali kuwekeza fedha zote hizo? Maana naona kama kinachotakiwa ni new generation of simba SC.
 
Tatizo lingine ambalo hujaligusia ni kuwa simba hatuna full backs.

Hawa kina shabalala na Kapombe hawana uwezo wa kupambana na wingers wenye kasi na pia uwezo wao wa kupiga crosses ni mdogo sana. Chunguza sana hizi game za kimataifa na hata za ndani jinsi wanavyochemka wakikutana na timibzinazoshambulia kupita pembeni.Tujiandae kisaikolojia kwaa game ya derby ya kariakoo..nahisi tunaweza tukapigwa .
 
Yaani leo tu game moja ndiyo tayari hawajui kupiga cross!? Tuwe wakweli bana hao ndiyo wachezaji bora wa pembeni nchini hawawezi kuwa perfect kwa kila kitu

Ila nilichokiona mimi ni kwamba Simba ni timu ambayo ukiitazama kwa undani utagundua imeathiriwa mno na wachezaji wa kule mbele ambao ni butu ila kudefend wako vizuri tu.
Kocha wetu hajiamini ndiyo maana kila mechi anabahatisha tu
 
Akiwepo Yakuba kushoto na Chiko Ushindi kulia, pale kati kuna Sure Boy.

Hakika itakuwa game ngumu mno kwa Simba. Achana na Derby, hata hawa Berkane hapa Bongo watacheza kwa umakini wa hali ya juu, mpaka sasa naiona Droo pale kwa mkapa kama sio kipigo.
 
Pia game zetu huwa tunacheza kwa temple ya chini sana...wachezaji hawakimbii wakiwa na mpira ama wasipokuwa na mpira tofauti na yanga wanavyocheza unaona muda wote timu ina kasi.
Morison na Kibu ndio wings pekee zenye kasi na skillz pale Simba. Siku hawa wote wakakosa mechi, na hiyo game simba icheze na timu nzuri, hesabu kilio.
 
Hebu pendekeza wachezaji husika wanaotakiwa kuja pale Simba afu utuambie gharama utalipia sh ngapi

Maana mimi naona ni lawama tu ila kiuhalisia wachezaji hao wa juu sana hata pesa yao ni nyingi sana mfano yule cirkovic si tuliambiwa analipwa milion 151 sasa Simba tulete wale watano per month hiyo bill tunaimudu kirahisi?
 
Ofkoz simba ina backline nzuri. Lakin yule Inonga utoto mwingi pamoja na sifa.

Kapombe na Zimbwe ni wazuri endapo wakakutana na upinzani wa kawaida, lakini ikija game inayohitaji watu wapambanaji utagundua hamna watu hapo.

Kwa ile kasi ta Berkane ya jana, hapa Taifa naiona droo kama sio kipigo kwa Simba.
 
Ngoja na huyu jamaa atoe maoni yake Cc😡 Mightier
 
Hali ya hewa pia ilikuwa barid
Sie huku ni tropical area uwez amini hata mwarabu akija huku hali ya hewa ni mushkelii

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Upumbavu mtupu.

Timu ikishinda mnaisifia, ikifungwa mnaanza kusema wachezaji wabovu. Acheni ujinga hakuna timu isiyofungwa duniani.
 
Afadhali ya kapombe ila shabalala anashambulia anachelewa kurudi pia anapiga pasi za uchonganishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…