Ni mbegu gani za mahindi zinafanya vizuri katika mkoa wako?

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Katika mkoa ninaoishi( Iringa) mbegu ya mahindi inayofanya vizuri sana ni Dk 777, ikifuatiwa na DK 9089, japo mbegu za kampuni ya seedco namba 409 na 403 zinajitahidi pia. Hii ni kulingana na utafiti wangu binafsi.Vipi katika mkoa unaoishi ni mbegu zipi zinafanya vizuri?
 
DK 777
20220501_171001.jpg
 
Duh Baadhi yamaeneo Mbeya DK 777 tunaiita MAPACHA ila naona hii 9089 ipo vzr zaid sijawahi kuijua kabla.
Ubarikiwe kwa kushea nasi
DK777 -Hukomaa kwa siku 130-150, hukupa magunia 40-44 km shamba ni zuri na utazingatia kanuni zote za kitaalamu
-Uzuri wa hii mbegu hata km shamba halina rutuba ya kutosha bado hujitahidi kuzaa tofauti na mbegu zingine.

DK9089 Hukomaa kwa siku 110-120,hukupa magunia 40-44.

Tatizo la DK 9089 mimea yake inaathiriwa sana na ugonjwa wa kuoza shoots au mimea "ku- misbehave" km picha zinavyoonyesha hapo chini. Mimea ikiathiriwa na huu ugonjwa hushindwa kuzaa kabisa au kuzaa mhindi mdogo na mbovu km picha namba 1 inavyoonyesha.
20220425_175602.jpg
20220221_104505.jpg
20220221_104439.jpg
20220221_105559.jpg
 
DK777 -Hukomaa kwa siku 130-150, hukupa magunia 40-44 km shamba ni zuri na utazingatia kanuni zote za kitaalamu
-Uzuri wa hii mbegu hata km shamba halina rutuba ya kutoshambegu hii hujitahidi kuzaa tofauti na mbegu zingine.

DK9089 Hukomaa kwa siku 110-120,hukupa magunia 40-44.

Tatizo la DK 9089 mimea yake inaathiriwa sana na ugonjwa wa kuoza shoots au mimea "ku- misbehave" km picha zinavyoonyesha hapo chini. Mimea ikiathiriwa na huu ugonjwa hushindwa kuzaa kabisa au kuzaa mhindi mdogo na mbovu km picha namba 1 inavyoonyesha.
View attachment 2207811View attachment 2207814View attachment 2207816View attachment 2207821
Upo vzr mkuu hongera sana kwakudadavua vyema ..vp umeshawahi kuzifutilia mbegu za uyole binafs ndio nazipendelea hasa UH 6303 licha ya bei yake kuwa chini kuliko mbegu nyingine mana tunanunua kg2@ 9000/= hali yakuwa hizi nyine ni kg2@ 12000 .pia punje zake zikikauka ni nzito naningumu na hayabunguliwi kwa urahisi mana kuna mbegu unakuta zinaanza kubunguliwa zingali mashambani
 
Mbegu nyingi za Uyole zinakomaa siku 150-160 au zaidi. Hivyo zinafaa sana maeneo ya nyanda za juu zenye mvua nyingi za mda mrefu km Tukuyu,Maeneo ya jirani na Mbeya mjini,Mufindi,Mafinga au Wilaya ya Kilolo na maeneo yanayofanana na hayo.
 
Kea wanao lima bonde la mto Ruvu naomba kujua spacing nzuri maana kuna mdau kaniambia ukibananisha hayazai
 
General spacing ya mbegu nyingi za mahindi ni 75cmx30cm. Mbegu zingine recommended spacing ni 75x25,60x30, 70x30,n.k kwa mbegu moja moja. Ni vema unaponunua mbegu usome maelekezo. Kila mbegu ina spacing yake kutegemea km ni mbegu fupi, wastani au ndefu.
 
Uzi nimechelewa kidogo japo si sana, nimejaribu kupanda mbegu za mahindi ya njano kwenye kifuko chake huwa ni kama kuna unga(dawa) mwekundu hivi, nasubiri matokeo yake.
Jina la mbegu nimesahau, nitaitafuta niseme hapa
 
Meru VAH 517
JPEG_20220510_152632_4823359214730542449.jpg
 
DK777 -Hukomaa kwa siku 130-150, hukupa magunia 40-44 km shamba ni zuri na utazingatia kanuni zote za kitaalamu
-Uzuri wa hii mbegu hata km shamba halina rutuba ya kutosha bado hujitahidi kuzaa tofauti na mbegu zingine.

DK9089 Hukomaa kwa siku 110-120,hukupa magunia 40-44.

Tatizo la DK 9089 mimea yake inaathiriwa sana na ugonjwa wa kuoza shoots au mimea "ku- misbehave" km picha zinavyoonyesha hapo chini. Mimea ikiathiriwa na huu ugonjwa hushindwa kuzaa kabisa au kuzaa mhindi mdogo na mbovu km picha namba 1 inavyoonyesha.
View attachment 2207811View attachment 2207814View attachment 2207816View attachment 2207821
Hili tatizo la kuoza unalitatuaje?
 
Back
Top Bottom