Ni mbegu gani za mahindi zinafanya vizuri katika mkoa wako?

DK777 -Hukomaa kwa siku 130-150, hukupa magunia 40-44 km shamba ni zuri na utazingatia kanuni zote za kitaalamu
-Uzuri wa hii mbegu hata km shamba halina rutuba ya kutosha bado hujitahidi kuzaa tofauti na mbegu zingine.

DK9089 Hukomaa kwa siku 110-120,hukupa magunia 40-44.

Tatizo la DK 9089 mimea yake inaathiriwa sana na ugonjwa wa kuoza shoots au mimea "ku- misbehave" km picha zinavyoonyesha hapo chini. Mimea ikiathiriwa na huu ugonjwa hushindwa kuzaa kabisa au kuzaa mhindi mdogo na mbovu km picha namba 1 inavyoonyesha.
View attachment 2207811View attachment 2207814View attachment 2207816View attachment 2207821
Mkuu unaweza ku share na mimi ni kanuni zipi za kilimo napaswa kufuata ili nipate hizo gunia 40-45 kwakua hua napata 10-15 kwa ekari mbegu natumia dk space natumia 75 kwa 30 situmiagi mbolea kwa kua eneo nililopo kuna rutba ya kutosha

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Ili uweze kupata magunia 35-40 inabidi ufanye yafuatayo:-

1.Shamba lako liwe bora yaani liwe na rutuba nzuri. Km hali ya udongo si nzuri basi hakikisha unalirutubisha kwa samadi msimu wa kiangazi kabla ya msimu wa mvua kuanza. Kwa ekari moja weka trip zisizopungua 4 za roli la kawaida.

Lundika samadi maeneo ya shamba yaliyochoka zaidi na umalizie kusambaza maeneo yasio na changamoto kubwa. Lengo ni kulifanya shamba lote liwe sawa kwa rutuba. Hii itayafanya mahindi yako shamba zima kuwa na muonekano mzuri unaofanana.

2. Panda mapema mwanzoni mwa msimu Kwa mbegu fupi panda kwa nafasi ya 70cmx30 au 70cmx25cm lengo kuongeza idadi ya mimea kwenye shamba. Kumbuka mavuno ni mimea. Maximum population kwa zao la mahindi ni mimea 21,000 kwa ekari.

3. Wakati wa kupanda simamia vzr wapandaji ili kila shimo liwekwe mbegu kulingana na utaratibu. Km ni mbegu moja au mbili basi utaratibu uzingatiwe.

4. Fanya palizi ya kwanza mapema wiki ya 3 toka kupanda.

5. Weka mbolea kwa wakati.
Kwa kifupi sana ukifanya haya hizo gunia 30-40 utazitafuta na km hutozipata basi walau 25.

Nb. Gunia ni wastani wa debe 6 ndio hufanya kg100.
 
Mkuu naomba kujua,kwa shamba lenye rutuba ya asili, Je nahitaji kuweka DAP kisha CAN kwa kiwango kilekile sawa na shamba lisilo na rutuba? Wenyeji wanasema hupiga gunia 15 kwa ekari bila mbolea.
 
Kwa Singida,
DK 777 ukilima kikanuni na mvua zikawa hata za wastani tu kama mwaka huu mbona utaipenda

Muhimu ni kuwahisha palizi ya kwanza na ya pili na kuweka mbole kama shamba ni dhaifu
Kama zinafaa kwa singida naamini hata kwa Dodoma zitafaa
 
Mkuu Kamgomoli DK 777 haishambuliwi na wadudu au kuoza shina ?
Kwa uzoefu wangu DK 777 haina historia ya kushambuliwa na ugonjwa wa kuoza mashina. Hilo tatzo hutokea sn kwa DK 9089. Kwa upande wa wadudu kila mbegu inashambuliwa na wadudu hapo lazima upige viuatilifu km Mult Afa,DK Rufa n.k mahindi yakiwa na mwezi mmoja toka kuota. Ukichelewa sana mazao yataathirika
 
Mkuu naomba kujua,kwa shamba lenye rutuba ya asili, Je nahitaji kuweka DAP kisha CAN kwa kiwango kilekile sawa na shamba lisilo na rutuba? Wenyeji wanasema hupiga gunia 15 kwa ekari bila mbolea.
Km udongo unarutuba unaweza usiweke mbolea ya kupandia. Ila nakushauri ili kuongeza mavuno ni vema ukaweka mbolea ya kukuzia km CAN,YARA CEREAL,UREA n.k
 
Katika mkoa ninaoishi( Iringa) mbegu ya mahindi inayofanya vizuri sana ni Dk 777, ikifuatiwa na DK 9089, japo mbegu za kampuni ya seedco namba 409 na 403 zinajitahidi pia. Hii ni kulingana na utafiti wangu binafsi.Vipi katika mkoa unaoishi ni mbegu zipi zinafanya vizuri?
huku usukumani ni mbegu za asili
 
Kwa uzoefu wangu DK 777 haina historia ya kushambuliwa na ugonjwa wa kuoza mashina. Hilo tatzo hutokea sn kwa DK 9089. Kwa upande wa wadudu kila mbegu inashambuliwa na wadudu hapo lazima upige viuatilifu km Mult Afa,DK Rufa n.k mahindi yakiwa na mwezi mmoja toka kuota. Ukichelewa sana mazao yataathirika
Mkuu. Dk 777 na Dk 9089 ipi inatoa mavuno mengi? Na ipi Ina punje kubwa?
 
Km udongo unarutuba unaweza usiweke mbolea ya kupandia. Ila nakushauri ili kuongeza mavuno ni vema ukaweka mbolea ya kukuzia km CAN,YARA CEREAL,UREA n.k
Habari ya leo mkuu.
Naomba kufahamu makundi ya mbolea za kukuzia na kuzalishia, yaan mbolea zipi nibza kukuzia na zipi za kuzalishia.
 
Back
Top Bottom